hearly
JF-Expert Member
- Jun 19, 2014
- 45,678
- 63,304
Haha unataka kumuita Shuniehivi zile cc zinafanya kazi vizuri niite mutu hapa!
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haha unataka kumuita Shuniehivi zile cc zinafanya kazi vizuri niite mutu hapa!
Mwambie apige chabo.Me mbona nimechungulia dirishani nimekuona.😂umegonga mlango WAP mkuu mbona mm nipo ndan?
Mwambie apige chabo.Me mbona nimechungulia dirishani nimekuona.
Mwingine kabisa naona unajihami.
Chief bwana ..haha najihami vipi sasa na mimi ni junior humuMwingine kabisa naona unajihami.
🙂🙂 kwa sentensi hizi bas kweli picha limeungua!!..
Jide alikuwa ni personal project ya Ruge from word go, kila aliyekuwa karibu analifahamu hilo. Tofauti zao zisimfanye aukwepe ukweli huo na pia ukaribu wao ulikuwa ni zaidi ya ukaribu back then.Msanii Lady Jaydee ameamua kufunguka jinsi alivyoanza harakati zake za kuingia kwenye muziki enzi hizo.
Akiandika mtiririko wa matukio kwa kadri ya kumbukumbu zake, amejikuta akikumbuka tukio la kuiba simu ya baba yake mdogo ili kupiga Radio One kwenye kipindi cha 'DJ Show' ambako kulikuwa na mashindano ya kusaka vipaji vya kuimba alikoibuka mshindi hapo baadae.
"Nilipata offer ya kurekodi wimbo wa kwanza baada ya kushinda shindano la Vipaji Halisi. Unapiga simu Radio One Stereo unaimba au ku rap kipindi “DJ Show” na Mike Mhagama. Na hapo ndio niliposikika rasmi. Sikuwa na pesa ya Studio ya kumlipa Master Jay", anaanza kusimulia Jide kupitia mtandao wa Twitter.
"Na nyimbo zilizonipa ushindi ni Keep On wa Mc Lyte, Stranded wa Lutricia McNeal na Gotta get you home wa Foxy Brown. Kulikuwa na awamu mbalimbali. Nikafanikiwa kuingia Top 3 na baada ya hapo kuibuka kidedea mshindi wa kwanza. Shukrani sana kwa Mike Mhagama" anaendelea kufunguka msanii huyo bora wa kike kwa nyakati zote katika tasnia ya muziki nchini.
"Kipindi hicho nilikuwa nafanya muziki just for fun tu, nothing serious. Nilikuwa naiba simu nyumbani kwa baba yangu mdogo ambapo nilikuwa naishi kipindi hicho ilipogundulika kuwa naiba simu kupiga radio eti naimba nilikula kibano pia. Ila sijutii wala nini".
"..Atleast sikuwa naiba pesa, nilikuwa naiba simu" anachombeza Komando kwa utani na kicheko juu.
"Kwa leo tuishie hapa. Story itaendelea siku nyingine kwa maombi maalum au kwa mapenzi yangu binafsi. Shukrani" amemalizia hivyo Lady Jaydee.
My take: Sikuwa nafahamu kwamba Jide alipata nafasi ya kwanza pale Radio One kutoka kwa kaka mkubwa Mike Mhagama (jamaa alikuwa peace sana huyu kwa wakongwe wenzangu mnaomkumbuka). Siku zote najua alianzia Clouds Media moja kwa moja.
NB: Akiendelea nitakuja kuweka hapa.