Laini moja ya simu inawezekana kumilikiwa na zaidi ya mtu mmoja na kuwa hewani?

Mimi simu yangu sio mtumba na sijawahi kuwa na simu hizo zilizotumika kabla nje au ndani ya nchi
Inawezekana we ulinunua kama simu mpya ila iliwahi kuwa refurbished before. Simu nyingi bongo zina sura hii ndiyo maana ukicheki actual price online na price za bongo unaweza jiuliza maswali yasiyo jibika.

Note:
A refurbished phone is not like a normal second-hand phone. It may have been returned by a customer for having a fault that the manufacturer has then repaired and sold it on as a refurb. The customer may have sold it back to the retailer orphone company so they can upgrade.
 
Hata Mimi lain yangu ya halotel inazigua ivo! juz mama ulikuwa ananipigia sim ikapokelewa na mdada yupo arusha! Jana tena dem wng ananipigia sim. sim ikapokelewa namdada uyouyo wa Arusha
 
Haiwezekani kabisa kuna shida ya kimtandao mahali..mimi pia nina shida na line yangu nikiwa offline tu ukinipigia unaambiwa huna muda wa maongezi na voda wameshindwa kabisa kulitatua hili tatizo
Zote hizo ni matokeo ya call forwarding.Wakati mwingine unafanya kwa kujua au bila kujua au watu wa mitandao wanakuwa wamejichanganya katika routing ila huwa namba hazifanani vinginevyo yule unayempigia angeshtuka kuona namba yake inampigia
 
Pia nmedumu na tatzo hilo kwa miaka miwili laini ya davo..hata hao davo huwa hawawez kugundua nn shdam. Kwa upande wangu tatzo liliondoka automatically
 
Mimi pia nina tatizo hilo halotel napigiwa na wasukuma mara kwa mara wanamtafta na kaka zangu siku nyingne wakipiga wanasema mbona simu alipokea mwingine..ngoja nije nijaribu na mimi kuopigia kwa namba nyingne.
Hata mimi nina tatizo kama hilo kea lakini ya halotel , wakati mwingine simu inaingia ikiwa na jina la mtu wa contact list yangu halafu anaongea mtu mgeni, ukikata ndo inaingia simu kweli ya mtu wangu lakini naye atalalamika kuwa akipiga simu na amepokea mtu mwingine
 
Call forwarding haifanyi kazi kama primary line haina hela, call forwarding haifanyi kazi kupitia vifurushi

Kuhakiki kuwa sio call forwarding hakikisha hakuna salio kwenye line yako halafu piga tena hiyo namba

Ukijua hivyo nenda kwa mtoa huduma ukiwa na ID iliyotumuka kusajili line. Unaoongea nao kwenye customer support line hawawezi kukusaidia kwa tatizo la aina hiyo
 
isije ikawa umedukuliwa na wenye-nchi?

Unafanya kazi gani? Angalia nyendo zako vizuri huenda umejiweka kwenye spot light!

Natania.
 
Line ni ya voda na haikuwa na salio wala kifurushi nimeipiga kwa halotel na jamaa akapokea. Ngoja niwatembelee ofisini.
 
Kabisa yani
 
Lakini mkuu, divert ni kuwa wakati haupo hewani simu zako zielekezwe katika namba nyingine uliyoiweka wewe kwenye settings

Yaani mfano mimi napiga kwako lakini vile haupo hewani simu inapokelewa kwa Mshana Jr ambaye namba yake umeiweka wewe kwenye setting za simu yako. Ili simu yangu mimi iende kwako kupitia kwa Mshana, simu yako wewe inahitaji kuwa na muda wa hewani.

Kwa ufupi, divert ni wewe mwenyewe unajipigia kwenda simu nyingine. Mpigaji hawezi kuambiwa hana salio sababu ya wewe kuweka namba ya kigeni sababu anayepiga namba ya kigeni sio yeye bali wewe ambaye hupo hewani. Hata aweke hela kiasi gani bado simu yake haiwezi kupokelewa ikiwa wewe huna salio.

Hivi ndivyo navyoelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…