Laini za simu kufungwa, akaunti za pesa kubaki

Laini za simu kufungwa, akaunti za pesa kubaki

Mi nina laini ya tigo waliifunga kwa kigezo ilikaa muda mreru bila kuweka vocha.
Hiyo laini haipokei msg ya aina yoyote, haipokei kifurushi, haiwezi kuongeza vocha pia. Ila incoming call zinakubali, nikipigiwa simu inaingia, nikitumiwa pesa inaingia bila msg na pia naweza kutuma pesa. Nikijinulia kifurushi, hela inakatwa ila baada ya masaa kadhaa inarudi kwenye tigo pesa.
Nadhani itakuwa namna hii kwa watakaofungwa.
watakaofungwa tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunajua laini za simu szisizosajiriwa ikifika 31Desemba Kisha 20Januari 2020, zitafungwa.

Tunajua serikali ilipitisha na kuridhia laini za simu kuwa akaunti za pesa pia

Tunajua simu ikifungwa akaunti ya pesa haiwezi kutumika, maana unaanza kuwa na laini ndio upate akaunti ya pesa na sio kinyume chake.

1. Hoja na swali langu kwa vile laini za simu zinafungwa kwa matatizo ya kimawasiliano na sio ya kipesa, je baada ya kuzifunga hapo 20 Jan 2020, wenye akaunti za pesa, pesa zao na akaunti zao zitakumbwa na kitu gani ama itakuwaje mtu kutumia akaunti yake ili hali simu imefungwa?

2. Zamani laini ikikaa miezi 3 kama sijakosema watoa huduma wanairejesha laini na kumpatia mtu mwingine muhitaji, je baada ya kusajiri laini yenye usajili wa mtu kwa alama za vidole, itaishi milele ama isipotumika itafungwa pia na kupewa mtu mwingine?

Naomba kuwasilisha kwa maelezo na maelekezo
uliona kazi kuanzisha uzi wako mpaka udandie wangu?
 
ÀCHA WAFUNGE TU NILIISHIA KUJAZA FOMU ZAO
 
Unapata safaricom kama ukiwa na mtandao wowote? Yaani ukiwa na Tigo, Airtel, halotel n.k?
Mfano, kama haupo Kenya, ukienda Kenya na laini yako ya Voda kwenye simu, uki-set roam, ukitua tu Nairobi (kama unatumia ndege), unapata mawasiliano kupitia Safaricom bila kuwa na laini ya Safaricom.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapata safaricom kama ukiwa na mtandao wowote? Yaani ukiwa na Tigo, Airtel, halotel n.k?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulivyosema kuhusu arrangement ni sawa, ila si lazima kupewa sim card ya kule uendako. Ila hao uliowataja husema kama wana huduma ya ku-roam na nchi ambazo waweza kupata huduma hiyo.
 
Mwisho wa siku itatulazimu roaming nyumbani kwa sim ya safaricom. Serikali ya ccm ama kweli imejua kumtesa mtanzania.
 
Ulivyosema kuhusu arrangement ni sawa, ila si lazima kupewa sim card ya kule uendako. Ila hao uliowataja husema kama wana huduma ya ku-roam na nchi ambazo waweza kupata huduma hiyo.
Hakuna mahali nilisema lazima uwe na line ya kule uendako, ni kwamba unapotoka kwenda nchi nyingine ili uweze kufanya roaming ni lazima mtandao wako uwe na ushirika na mtandao wa kule unakoenda ndio hao roaming partners. Kwa maana hiyo basi, mgeni akija kwetu na line ya mtandao wake anaotumia kwenye nchi yake ili aweze kufanya roaming lazima awepo roaming partner ambaye anaweza kuwa Voda, Tigo etc vinginevyo hatapata mawasiliano. Hivi ndivyo ninavyojua mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Minaona n Sawa tu wafungie matapeli yalikuwa meng at least itapunguza uhalifu
 
Back
Top Bottom