Laiti kama kule Hai angekuwepo mwanaume kama Saidy Mwamwindi

Laiti kama kule Hai angekuwepo mwanaume kama Saidy Mwamwindi

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Huwa nafuatilia tuhuma zote alizotuhumiwa Sabaya nabaki kujiuliza What if kingetokea kidume kama Mohamed Mwamwindi kule Hai kingebadili historia yote ya Hai na kila kiongozi akipelekwa Hai anakuwa na adabu kabisa.

Wale wasiojua historia zamani kidogo Serikali ya Mwl Nyerere ilikuwa inaogopewa sana na hata Ma RC na Ma Dc walikuwa wanaogopewa. Ingawa haikuwa serikali ya kufanya mabaya kwa wananchi tena wazi wazi kama alivyofanya Sabaya.

Sasa wakati fulani ilipitishwa Sera ya Vijiji vya ujamaa kwa mujibu wa Sera hii. Wananchi waliokaa mbalimbali walikusanywa wakae pamoja ..walime pamoja. Hii Sera ilikuja kufeli na kusababisha baa kubwa la njaa baadae kabla haijabadilishwa na kusitishwa.

Watu walikufa pia maporini inasemekana walipoelekwa bila mipango sahihi. Nyerere alikuwa anajaribu ku copy Vijiji vya kijamaa vya China ..lakin utekelezaji wake ukaishia kuleta shida sana.

Sasa kule Iringa kulikuwa na kidume kimoja chenye mashamba yake Makubwa analima hadi na matrekta yake mwenyewe ...anaitwa Saidy Mwamwindi huyu akawa na yeye anatakiwa kuacha shughuli zake kwenye mji wake aende akajiunge kwenye kijiji cha ujamaa..walime na wengine.

Watu wengi walikuwa hawataki kabisa hii Sera ..walipinga kimyakimya na wengine mgomo baridi. Kampeni za kuhamasisha zilisambaa na Ma RC na ma DC walikuwa mbele sana kwenye kuhamisha hamisha watu wapelekwe kwenye Vijiji vya ujamaa.

Iringa alikuwepo RC anaitwa Dk Kleruu ambae alikuwa mkali Sana akihimiza na hata kutumia nguvu kuhamisha watu kupeleka Vijiji vya ujamaa.

Inasemekana huyu jamaa alikuwa kila mara anakwenda kwa Ndugu Mwamwindi kumtishia kutumia nguvu ya kumhamisha aende kwenye kijiji cha ujamaa.

Siku moja Huyu RC alienda kwa Mwamwindi akafoka sana na mikwara mingi na kutishia sana. Mwamwindi inasemekana aliingia ndani akatoka na bunduki yake the rest is History. Kisha akaubeba na mwili wa Marehem kwenye gari yake akaupeleka yeye mwenyewe polisi akawaambia polisi chukueni 'mzigo wenu'kwenye gari.

Nimesikia kuna dada za watu na wake za watu zaidi ya 40 huko walikuwa wanabakwa na kulawitiwa kwa nguvu huko Hai ...nikawa najiuliza what if mtu kama Sabaya angekutana na mtu kama Mohamed Mwamwindi? Leo tusingepoteza kabisa muda wa kufuatilia kesi hii.

NB: Recollection ya history ya Mwamwindi na Kleruu inaweza kuwa na errors mbalimbali sababu nilisimuliwa zamani halafu kwa mdomo tu. Wanaojua history kamili wanaweza tuwekea hapa.
 
Ungeweka na mwaka maana hili tukio kila mtu ana hadithi yake. Wengine wanadai alikuwa anatembea na mke wa mkulima na wengine wanadai RC alikuwa anadaiwa. Nipo hapa kisasa shell nasubiria ukweli.
 
Recollection ya history ya Mwamwindi na Kleruu inaweza kuwa na errors mbalimbali sababu nilisimuliwa zamani halafu kwa mdomo tu..
Wanaojua history kamili wanaweza tuwekea hapa
Story yako ipo sahihi sana mkuu, mzee wangu alinisimulia hii mwaka 2003 nikiwa form 4.

Pia aliwahi kunisimulia kisa cha mhindi aliyemuua mkewe na kutaka kudai pesa nyingi sana za bima ikabidi waje wapelelezi wa Police (Scotland Yard) kutoka England.

Wazee ni hazina, tuwatunze.
 
Last time I checked, wasiojulikana walipigwa risasi tarime. Mpaka sasa hii rekodi haijavunjwa, walikutana na kichwa ngumu!
Mr zakaria yule michezo hiyo anaijua sana na hao alidili nao kimafia kama walivyo muibukia. Lakini si kuwabughudhi maafisa wanaojulikana.
 
Tarime siku hizi kama wanaume wa dar tu wenyewe ubabe wao upo kwenye visasi vya dhulma ukabila kuchukuliana ardhi n.k

Ila kwa maafisa wa serikali huwa wanaufyata.
Kabisa,
 
Back
Top Bottom