Juzi July 2nd, ilikuwa birthday ya hayatı Patrice Lumumba, kama angeishi mpaka hiyo July 2nd, 2024, angefikisha umri wa miaka 99.
Kuna watu wanamkumbuka kwa namna mbalimbali na kusheherekea birthday yake mpaka leo.
Kiufipi sana, si kweli kuwa viongozi wa Afrika ni wajinga au/na wana viburi tu hivi hivi. Tatizo kubwa nchi zetu zina uhuru wa bendera, amri zinatoka Washington na miji mikuu mingine ya Uropa magharibi. Kiongozi wa nchi ya Afrika akijifanya hataki kuwasikiliza, ana shughulikiwa kama ilivyokuwa kwa marehemu Lumumba enzi hizo, siku hizi kuna vikwazo, kuitwa dikteta kama alivyofanyiwa hayati JPM na mengi mengine.
Nchi za Ulaya na Marekani zinataka Afrika ibaki kama ilivyo, isiendelee kamwe wala kupiga hatua yeyote. Kazi ya Afrika kwa mtazamo wao ni kutoa malighafi mbalimbali na kubaki kama soko. Hii mentality juu ya Afrika, pia nchi za Asia kama uChina, Korea Kusini na kadhalika zina iona Afrika katika jicho sawa na la nchi za magharibi. Pamoja na mengine, mtego ni madeni….halafu IMF na WB wanakuja na marching orders kama kilichotokea Kenya. WTO wao wanakuja na story za free trade blah blah blah, wakati katika historia, hakuna industry yeyote katika nchi flani ilikuwa na kufanikiwa bila protectionism.
Wajinga wana discourage manufacturing, nchi kama Kenya mpaka diapers ni imported, bongo nadhani mpaka yeboyebo na zenyewe zinatoka zinapotoka. Hatuna kabisa manufacturing, hivi maendeleo yatayoka wapi? Hizo kodi atalipa nani? Una muongezea mwananchi kodi ya mkate kama IMF walivyo amrisha, lakini huyo mwananchi hana kazi, atatoa wapi hiyo pesa?
Mfano, Zambia na DRC walikuwa na mpango wa kufungua kiwanda cha Lithium batteries. Wamarekani wakaingilia kati kuwakwamisha, pamoja na mengine wakaja na gia ya Lobito corridor blah blah. Point, kama DRC wangefanikiwa kuwa na kiwanda cha lithium batteries, battery zao zingekuwa cheaper…kumbuka tunakoenda EV ndiyo habari ya mjini. Kwa utajiri wa DRC wa cobalt na lithium, easy DRC ingekuwa king 👑 wa lithium batteries humu duniani. Lakini ni kama hawaruhusiwi kunufaika na utajiri wao. Marekani anataka awe na final say, Zambia na DRC wakaufyata.
Mambo ni mengi, lakini kwa kumalizia tu, miye simtetei Ruto au kiongozi mwingine yeyote wa Afrika, ni kwamba kiongozi akijifanya kutaka kufanya kilicho sahihi kwa nchi na wananchi wake, hadumu madarakani na anakuwa na umri mfupi. Lazima wamshughulikie, viongozi wengi waoga, hawana pumbu kubwa, wanaamua kuwa puppets.
Kuna kiongozi mmoja wa zamani bongo, jina kapuni, alimpiga dongo hayati JPM kuwa ana “jimwambafai.”
God bless JPM (RIEP)