Laiti kama Ruto angeyafanya haya kabla ya maandamano ya gen Z angeimbwa kama shujaa wa Afrika. Afrika tunakwama wapi!?

Askofu Mwanamapinduzi ametoa hotuba mda mchache uliopita akiyasema haya uliyoyaandika hapa.
Tatizo nikuwa sisi ni Maiti, watawala wana uhakika kuwa maiti haziwezi kufufuka na kudai haki zao!
 
Tatizo waendesha nchi , hata yeye usikute kwanyuma alihusika kwanamna moja kuandamana na Gen z
 
Tulichojifunza watanzania wazalendo ni kuwa haki Huwa haiombwi kama inavyoombwa na watanzania Bali hupiganiwa.wtz tuchukue hatua maujinga ujinga aliyoyafuta mheshimiwa rais ruto na Tanzania yapo.mfano mke wa rais anadai eti na yeye apewe gari,nyumba,magari ya kifahari,pesa za mawasiliano,umeme Bure,maji Bure,chakula Bure wakati huohuo na mme wake anapewa Hivyo vyote na Bunge letu kibogoyo limepitisha Kwa kura ya ndiyoooooo.Wakenya wamemuadabisha ruto Hadi amefuta huo upuuzi lakini Tanzania Kwa kuwa ni wajinga wajinga wamekubali kukamuliwa Kodi za kuwapeleka wake wa Marais kwenda kubembea ulaya na kufanya vipimo vya mafua ulaya.
 
Ndugu Ynim kuna vitu wazungu wanaoweza kukutengenezea mazingira sikatai lkn hivi ni wazungu walimwambia Ruto awapangie mshahara wake za viongozi!?
Ni wazungu walimwambia apange kodi kubwa isuyolupika!?
 
Yaliyopingwa na wananchi wa Kenya huku kwetu yanafanyika Kila mwaka, na tumekaa kimya! Naona aibu kuwa raia wa nchi hii.
 
Mkuu una moyo kweli. Unajadiliana na robot bila kuchoka muda wote huu? Huyo yupo JF 24/7 kwa kazi ya kuzungushia kamba hoja za kipinzani hasa kuhusiana na CHADEMA. Ndivyo desperate CCM walivyo hivi sasa. Ukimuacha ndio kakushinda hivyo. Anasheherekea kumzima hasimu mmoja!
 
Kenya imepitia misukosuko mingi ya watawaliwa kudai haki zao, lakini watawala wameshindwa kujifunza.

Dec 2007 Kulizuka machafuko na mauwaji ya kutisha wakati wa uchaguzi mkuu,hadi wakatunga katiba mpya.
June 2024 Kutumia katiba hiyo kuwa wananchi ndio wenye madaraka na maamuzi ya nchi yao,lakini walipoandama wakidai Financial Bill Ifutwe kabisa,watawala walitumia excessive force kuzima maandamano hayo.

Ruto alishindwa kusoma alama za nyakati,hadi wananchi kupoteza maisha.
Masharti ya mikopo kutoka World Bank na IMF ni shubiri kwa mataifa maskini.
Lakini pammoja na masharti magumu toka kwa wahisani inabidi watawala kuwatumikia wananchi kwa uaminifu na kwa weledi mkubwa ili kujenga uaminifu kwa wananchi.

Wabunge wasiwe rubber stamp waache kubeba serikali wafanye kazi iliowaleta bungeni,ya kumwakilisha mwananchi.
 
''Masharti ya mikopo kutoka World Bank na IMF ni shubiri kwa mataifa maskini''.
Hili mimi sikubali. Ingekuwa ni shubiri basi tungeona viongozi wetu wanapigana kufa na kupona ili kuacha utegemezi. Wangepunguza utitiri wa viongozi na wabunge tulio nao, wangesafiri kwa madaraja ya kawaida kwenye ndege, wangenunua magari machache na ya nafuu, misafara yao ingekuwa na magari machache, wangepigana kufa na kupona na ufisadi nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…