Laiti mchaga angekuwa RAIS...maendeleo ya nchi yangekuwa mbali sana

Hivi wewe Mmakonde mbona uko myopic hivi? Nyie ndiyo mnaodhani kwamba kabila au ukoo fulani wamezaliwa hawana mapungufu au wale wengine wote hawafai. Uendeshaji wa nchi hautegemei tu yule aliyeko ikulu. Hapa kilichopo ni mfuomo wa utawala na utengenezaji wa vipaumbele katika uendeshaji wa taifa ndiyo siri ya maendeleo. Sasa wewe unampima mchagga anayeuza duka au ujenzi wa nyumba kijijini kama kigezo cha sifa ya utawala! No wonder unajiita Mmakonde! Kuongoza nchi ni zaidi ya kujenga nyumba au kumiliki duka na daladala. Mbona tulikuwa na mawaziri wachagga serikalini lakini wizara zao hazikung'ara na wengine kuishia kisutu mahakamani na huku akina Pombe Magufuli wakionyesha juhudi za dhati za kupambana na umaskini wa waTZ?
 

Tueleza huyu Magufuli amefanya nini cha maana!Yuko kwenye Chama cha kifisadi,nafikiri anajikosha kwa wananchi wasioelewa mambo.
Labda tuambiw unatoka wapi,at least mimi ni Mmakonde,umefika kwenye Mtwara?Kuhusu kufikishwa Kisutu,wata wengi tu hawajafikishwa.

Ujue Tanzania,hata kufikishwa mahakama ni political,wako wapi Kingpins kama akina EL,RA,Vijisenti etc
Kubali usikubali with due respect to makabila kama langu,Mmakonde na mengine mengi ,Wadengereko,Wazigo,Wazaramo,Wagogo,Wanyiramba,Wakerewe etc ukifika wilayani zao utachoka.Wasomi wao wamestuck jijini Dar na magorofa yao,lakini nenda vijijini kwao utaona.

SIMPLE LOGIC:Kama huwezi kuendeleza ulikozaliwa,unategemea nini kuliendeleza taifa as a whole!
 
MBOPO umenifuraisha sana tatizo la wachaga wakifungua vibanda vya kuuza mishikaki,supu,viduka vya jumla, basi kwao ni maendeleo makubwa sana wanafikiri nchi itakuwa na maendeleo kwa style hii,huo upuuzi wenu muuache siku hizi makabila yote yana wasomi watu wanataka maendeleo kwa nguvu
 
Mmakonde na kuunga mkono ila kwa kuwa utofauti na uonavyo wewe, mimi sikuzote naamini watanzania (hawana akili) za maendeleo! au mapinduzi au za kielimu, nasema hivyo nikimaanisha hata yale makabila yaliyoendelea sio watanzania!, nikianza na wahaya hawa ni waganda walisambaa wakati ule wa Buganda kingdom, Wachaga ni Wakenya, Wanyakyusa ni watu wa Zambia na Malawi, Wakurya na Wasukuma hawa wote ni Wakenya na hata waha huko kigoma ni Warundi na Wakongo kwani licha ya kunyimwa fursa wana akili za kimapinduzi ili wawe na uongozi utakaowaletea maendeleo. Tangu baada ya Nyerere tumekua tukipata viongozi waAswahili hawa sasa ndio watanzania wazawa kihistoria. Angalia maeneo yote ya waAswahili hawa utaona ni jinsi gani walivyo na uduni wa maisha ukitoa Dar es salaam ambayo imeendelezwa na wazungu, Wahindi, waarabu, wachaga, wahaya nk, leo hii ukiwatafuta Wazaramo katikati ya jiji utawakuta wachache na ndiyo wanaishi kwenye vijibanda huku wakiwa wamezungukwa na mahekalu baada ya kuuza viwanja, pia rejea DOKTA SLAA katika kampeni zake pale Bagamoyo alivyoshangaa maisha wanayoishi katika mbavu za mbwa.
Mimi nimefanikiwa kuishi dar es salaam, pwani, tanga, morogoro, iringa, mbeya arusha, kilimanjaro manyara na singida kwa kweli utofauti wa hawa ninaowaita waAswahili ambao ni wazawa na hawa wahamiaji ni mkubwa sana japo wengi wetu hatuoni, nilipoishi mbeya wanyakyusa wanavyowajibika kimaendeleo usipowasifu wewe utakuwa mkabila wa dhahiri, nguvu wanaoitumia katika kilimo mchele, mahindi, matunda nk halafu nilinganishe na wale niliowakuta Pwani, Morogoro, Tanga, Manyara na Singida ni tofauti sana.

Huko Kilimanjaro nilishangaa sana mwaka 2000 kwa mara ya kwanza nilipita kuanzia Moshi mjini kwenda SANYA JUU niliona nyumba tatu tu ambazo ni za udongo tena nyumba hizo zilionyesha si za kuishi kwani pembeni kulikuwa na nyumba nzuri ya block. Mnaoishi huko mtalithibitisha hilo kwangu ilikuwa maajabu kwani nililazimika kuangalia nyumba hizo ili nione nyumba za nyasi lakini sikufanikiwa mpaka nilipofika tena kule vijijini kumejengwa vizuri karibia kulingana na mjini cha kushangaza Kilimanjaro hiyohiyo nenda kwa Wapare utashangaa na utaweza kumuunga mkono MMAKONDE kimaendeleo hawa WACHAGA hawana utani.

Kilichonishangaza zaidi kule suala la afya wanakimbizana na hapa DAR ES SALAAM kuna hospitali kubwa za rufaa mbili KCMC na KIBONGOTO-TB, MAWENZI HOSP, MARANGU HOSP, KIBOSHO HOSP, MACHAME HOSP, KILEMA HOSP, MOSHI ARUSHA HOSP, ROMBO MISSON HOSP hizi zote ni hospital kubwa katika kamkoa kadogo unachokiona kwenye ramani ya TZ na bado sijataja hospitali yoyote ya wilaya katika wilaya za mkoa huo.

Nilipoishi arusha kwa kweli hata wanaoishi pale wanisaidie kwasababu nilichora picha ya Dar na Pwani watu wazaliwa wa mkoa wa Pwani mpaka leo hawajaweza kuchangamkia fursa ya kuwepa kwa jiji la Dar es salaam karibu yao kwani ni maskini wa kutupa rejelea maisha ya kisarawe, bagamoyo, kibaha, chalinze na hata morogoro ni tofauti na wachaga walivyotumia fursa ya kuwepo kwa TANZANITE, NGORONGORO,TARANGIRE, KENYAN BOARDER, na utalii kwa ujumla. Leo hii pale Arusha 5*s hotel asilimia kubwa ni za wachaga na nyingine za kiwango cha kati the same COIN here in Dar nenda kwenye maduka pale kariakoo baada ya mhindi na mpemba utamkuta nani?

Hivi kweli kwanini mabasi yanayotoka DAR kwenda MOSHI/ARUSHA asubuhi ni mengi kuliko yanayokwenda mikoa mingine? au kuliko daladala zinazokwenda Kisarawe? au costa Morogoro? na kwanini basi linapofika MOSHI abiria karibia wote wanashuka linapakia wengine kwenda ARUSHA? je si hawa wachaga wanatumia fursa ya jiji la dar na arusha kimaendeleo kuliko WAARUSHA, WAIRAKI,WAKWERE, WASAMBAA na WAZARAMO walioko karibu zaidi na mikoa hiyo?

HIVI kwanini licha ya kuwa na shule nyingi (500) za sekondari kihistoria kabla la shule za kata hawakutosheka na hizo sasa hivi ziko (900 na)? na kiutafiti wangu wakati huo kwao maji, umeme, nyumba, kwao si tatizo hivyo walimu wakipangiwa huko wanakwenda bila kusita. je ukitoa dar nimkoa gani una vyuo vikuu vitano; MUCCOBS,KCMC, SMMUCO,MWUCE na MWIKA?.

Kwa kweli mimi nimeshalitafakari kwa muda mrefu kabila hili na ninaona hawa watu si wa kubeza na kupitia hilo limeshanipa changamoto nyingi kiasi kwamba na mimi kwa kiasi fulani nimefanikiwa kibiashara. Na siku nikiamua kuona nitaoa MCHAGA atakayenipenda ili wanangu wasiwe na elementi za uswaAhili jumla kama baba yao.

ILA SI LAZIMA KUWA RAIS KAMA ANAVYODHANI MMAKONDE.

NAWASILISHA.
 
TAYARI................ mmeanza kujadili urais kwa KABILA la mgombea................... mlianza kwa kupokezana kati Mzanzibari......... na Mtanganyika.......... MKAJA ...................Muislamu kupokezana na mkristu.................. sasa Mmeanza Mchaga............hamtaishia hapo.........mtendelea mbele........mchaga wa wapi..........KIBOSHO...................MACHAME................ etc.
 

Duh. Umewahi kufika kwao au unawaona huko Kariakoo?
 
ukweli ni kwamba hawa jamaa hata huku dsm sehemu wanazokaa huwa wana mobilze nguvu kazi kufanya maendeleo fulani hili nimewaona mara kwa mara kama katika kuanzisha miradi ya maji, kutengeneza barabara, hata huyu mrema wao nilimona wakati akiwa waziri alikuwa machachari ati. Hawa jamaa ni watani zangu
 
THATHA .... hayo uloyasema umetania tu au......??
 
Ugonjwa wa UKABILA umekushika. Ni ugonjwa hatari sana, kama UDINI vile... Upone haraka...
 
So who is the best ? Mkwere ?
 
Mnaonaje tukiua ukabila halafu tujenge utamaduni wa mtanzania ambao utakuwa ni wa kupenda maendeleo. Kama kilichopelekea wachaga kuendelea ni utamaduni basi tuige /entrench utamaduni wao ili sote twende mbele maana hoja hii inaweza kuleta ufa wa umoja wa utanzania kwa kuwa na harufu ya ukabila
 
BARKMEI,umeeleza vizuri kabisa.Ila kuna watu hapa bado wako kwnye DENIAL.
Ukisema kitu wanakimbilia kusema eti udini na ukabila .Fact ni fact

Mimi si mchaga,ila nina akili ya kuobserve na kutoa maoni.

Kwa mara ya kwanza nilipokwenda Moshi O-level,niliona live TV ,na television kwa mara ya kwanza.Wenzetu walikuwa na madishi na kuona TV toka Kenya .Nishangaa sana.Ilikuwa big news ,wakati kijijini kwetu watu wana tembe na kulalia ngozi,wenzetu walikuwa na mabati na vigae.

Kumbe Reginald Mengi,alishaona miaka mingi huko kwao Uchagani.ITV ndio ikawa ya kwanza kwa majority ya Watz.

Credit kwa Kikwete anafanya Social Engineering kwa Waswahili wenzake.
TISS,CJ,Mambo ya Ndani,Afya, Ulinzi na JKT na Fedha.
 
Urais ni taasisi sio mtu binafsi. Mtalijua hili tukishapata katiba mpya, sio kwa hii iliyopo.
 
Sidhani kama nchi inaendeshwa na mtu mmoja, hivyo kuwa na raisi toka moja ya makabila yafuatayo Wahaya, Wachagga, Wanyakyusa siyo tiketi ya kusonga mbele kimaendeleo. Raisi anahitaji kuwa na washauri makini wenye utashi wa kuwaletea maendeleo wananchi wao, kinyume chake washauri wengi wapo wapo tu kujilimbikizia mali na matokeo yake ni kuwa na EPA, Kagoda, Richmond, Buzwagi, Rites, South Africa/ATCL, Net Group solution n.k.

Kinachohitajika sasa ni system"Overhaul" maana waliopo vitu kama rushwa kwao ni haki na sehemu ya vipato vyao.
 
 

Mmakonde:

Sio watu wapo kwenye denial. Hila unajenga hoja kwa kutumia fallacies. Mambo yote unayosema kuwa mchagga kayafanya, Muhaya ameyafanya. Wana majumba makubwa kwenye mashamba kama vile wachagga. Wamesoma kama vile wachagga. Sasa kwanini umependekeze Mchagga na sio Muhaya?

Na kama criteria za kumpata rais ziwe zinajumlisha kabila lenye watu wenye nyumba nzuri na TV, basi vipo vikabila vidogo vidogo vyenye kufikia mambo hayo. Wahindi wa Tanzania ni kabila na wana maendeleo makubwa kuliko mchagga, wapeni urais.

Unasema wewe sio Mchagga, lakini una akili ya ku-observe na kutoa maoni. Hii pia haifanyi maoni yako yawe sahihi. Kwanza unafanya generalization. Pili huko subjective. Tatu unakiuka kanuni za kiuchumi.
 
Hayo mahekaru ya Migombani wanaishi akina nani kama sio yanalindwa tombs. Hata ndugu hawaruhusiwi kuishi bila kujali kama hawana makazi bora.
Labda barabara ya Mramba itafungua fursa ngoja tungoje tuone...
 
sio kweli kuwa wachaga ndio wanamaendeleo, nenda kishumundu kwenye maporomoko hawajui hata kiswahili na wako karibu na mjini, je hawa walichelewa wapi, useme walizaana sana kutokana na ndizi hivyo ardhi haiwatoshi ndio maana wakasamba kwa kuwa hawakuwa na chakula cha kutosha, nenda Bukoba, nenda Mbeya na sehemu zote za walima ndizi hawa watu waliweza endelea maana kilimo chao ni cha mazao ya kudumu kama kahawa na migomba sasa kilimo cha kuama au mpaka ualibu mistu ndio ule kama vile kwa wasukuma au wafugaji amabo maji yakikauka wanaama je watasettle saa ngapi kabla ujatadhimini utoe ushuhuda wa sababu za kabila hii kuendelea, hata hivyo kwao ni karibu , kama wangekuwa ni wahaya , ciment , mabati yanapatikana karibu ungazani Ulaya
 
una ugomvi na wakwere?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…