Shaycas
JF-Expert Member
- Feb 13, 2009
- 906
- 112
Mmakonde:
You are very cheap. Mambo anayofanya mchagga yalifanywa na wazungu zaidi ya miaka 1000 iliyopita. Sasa kwanini usitake wazungu tu wakutawale?
Mungu wangu.....!!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mmakonde:
You are very cheap. Mambo anayofanya mchagga yalifanywa na wazungu zaidi ya miaka 1000 iliyopita. Sasa kwanini usitake wazungu tu wakutawale?
Mmakonde,
..nadhani maendeleo yaliyopatikana UCHAGANI yanatokana na kilimo cha KAHAWA.
..bahati nzuri kwa hawa wenzetu zao la kahawa limekuwa stable[bei,uzalishaji] kwa muda mrefu sana, na halijawahi kuporomoka kama vile korosho au mkonge.
..suala lingine ni kwamba mkoloni hakuwakamata na kuwatumikisha Wachaga kama ilivyo kwa makabila mengine. It was more efficient/profitable kuwaachia Wachaga walime kahawa na mkoloni abakie na jukumu la ununuzi tu.
..kuna maeneo ya nchi hii ambayo yalirudishwa nyuma kimaendeleo kwasababu Mkoloni aliyatawala kikatili. yako maeneo ambayo walitaka kulima kahawa kama Wachaga, lakini kwasababu mkoloni alikuwa na idea nyingine na maeneo hayo basi alizuia jitihada hizo tena kwa mabavu.
..yako maeneo ambayo yalikuwa mahsusi kwa mashamba makubwa plantations. yako maeneo ambayo yalikuwa mahsusi kwa kukamata manamba. ilikuwa ni vigumu kwa wananchi wa maeneo hayo kuweza kujihusisha na shughuli binafsi.
..sasa unaweza kusema kwamba Mkoloni ameondoka miaka mingi mbona wananchi bado wako vilevile? jibu langu ni kwamba tumekuwa tukitawaliwa na serikali za hovyo-hovyo tangu tupate uhuru. hakuna hata moja iliyoweza kubadili maisha ya Mtanzania.
NB:
..maeneo yote ambako Kahawa inalimwa nchi hii wananchi wake wana ahueni ya kimaisha.
Wewe kumbe huwajui wachaga.Jamaa hawa wako interested na maendeleo yao binafsi na ndugu zao. Usishangae Mchaga akiwa Rais waka accumute all the countries wealth unto themselves.Wako selfish sana.Afadhali Mpare bahili kuliko Mchaga mwizi.
Mmakonde na kuunga mkono ila kwa kuwa utofauti na uonavyo wewe, mimi sikuzote naamini watanzania (hawana akili) za maendeleo! au mapinduzi au za kielimu, nasema hivyo nikimaanisha hata yale makabila yaliyoendelea sio watanzania!, nikianza na wahaya hawa ni waganda walisambaa wakati ule wa Buganda kingdom, Wachaga ni Wakenya, Wanyakyusa ni watu wa Zambia na Malawi, Wakurya na Wasukuma hawa wote ni Wakenya na hata waha huko kigoma ni Warundi na Wakongo kwani licha ya kunyimwa fursa wana akili za kimapinduzi ili wawe na uongozi utakaowaletea maendeleo. Tangu baada ya Nyerere tumekua tukipata viongozi waAswahili hawa sasa ndio watanzania wazawa kihistoria. Angalia maeneo yote ya waAswahili hawa utaona ni jinsi gani walivyo na uduni wa maisha ukitoa Dar es salaam ambayo imeendelezwa na wazungu, Wahindi, waarabu, wachaga, wahaya nk, leo hii ukiwatafuta Wazaramo katikati ya jiji utawakuta wachache na ndiyo wanaishi kwenye vijibanda huku wakiwa wamezungukwa na mahekalu baada ya kuuza viwanja, pia rejea DOKTA SLAA katika kampeni zake pale Bagamoyo alivyoshangaa maisha wanayoishi katika mbavu za mbwa.
Mimi nimefanikiwa kuishi dar es salaam, pwani, tanga, morogoro, iringa, mbeya arusha, kilimanjaro manyara na singida kwa kweli utofauti wa hawa ninaowaita waAswahili ambao ni wazawa na hawa wahamiaji ni mkubwa sana japo wengi wetu hatuoni, nilipoishi mbeya wanyakyusa wanavyowajibika kimaendeleo usipowasifu wewe utakuwa mkabila wa dhahiri, nguvu wanaoitumia katika kilimo mchele, mahindi, matunda nk halafu nilinganishe na wale niliowakuta Pwani, Morogoro, Tanga, Manyara na Singida ni tofauti sana.
Huko Kilimanjaro nilishangaa sana mwaka 2000 kwa mara ya kwanza nilipita kuanzia Moshi mjini kwenda SANYA JUU niliona nyumba tatu tu ambazo ni za udongo tena nyumba hizo zilionyesha si za kuishi kwani pembeni kulikuwa na nyumba nzuri ya block. Mnaoishi huko mtalithibitisha hilo kwangu ilikuwa maajabu kwani nililazimika kuangalia nyumba hizo ili nione nyumba za nyasi lakini sikufanikiwa mpaka nilipofika tena kule vijijini kumejengwa vizuri karibia kulingana na mjini cha kushangaza Kilimanjaro hiyohiyo nenda kwa Wapare utashangaa na utaweza kumuunga mkono MMAKONDE kimaendeleo hawa WACHAGA hawana utani.
Kilichonishangaza zaidi kule suala la afya wanakimbizana na hapa DAR ES SALAAM kuna hospitali kubwa za rufaa mbili KCMC na KIBONGOTO-TB, MAWENZI HOSP, MARANGU HOSP, KIBOSHO HOSP, MACHAME HOSP, KILEMA HOSP, MOSHI ARUSHA HOSP, ROMBO MISSON HOSP hizi zote ni hospital kubwa katika kamkoa kadogo unachokiona kwenye ramani ya TZ na bado sijataja hospitali yoyote ya wilaya katika wilaya za mkoa huo.
Nilipoishi arusha kwa kweli hata wanaoishi pale wanisaidie kwasababu nilichora picha ya Dar na Pwani watu wazaliwa wa mkoa wa Pwani mpaka leo hawajaweza kuchangamkia fursa ya kuwepa kwa jiji la Dar es salaam karibu yao kwani ni maskini wa kutupa rejelea maisha ya kisarawe, bagamoyo, kibaha, chalinze na hata morogoro ni tofauti na wachaga walivyotumia fursa ya kuwepo kwa TANZANITE, NGORONGORO,TARANGIRE, KENYAN BOARDER, na utalii kwa ujumla. Leo hii pale Arusha 5*s hotel asilimia kubwa ni za wachaga na nyingine za kiwango cha kati the same COIN here in Dar nenda kwenye maduka pale kariakoo baada ya mhindi na mpemba utamkuta nani?
Hivi kweli kwanini mabasi yanayotoka DAR kwenda MOSHI/ARUSHA asubuhi ni mengi kuliko yanayokwenda mikoa mingine? au kuliko daladala zinazokwenda Kisarawe? au costa Morogoro? na kwanini basi linapofika MOSHI abiria karibia wote wanashuka linapakia wengine kwenda ARUSHA? je si hawa wachaga wanatumia fursa ya jiji la dar na arusha kimaendeleo kuliko WAARUSHA, WAIRAKI,WAKWERE, WASAMBAA na WAZARAMO walioko karibu zaidi na mikoa hiyo?
HIVI kwanini licha ya kuwa na shule nyingi (500) za sekondari kihistoria kabla la shule za kata hawakutosheka na hizo sasa hivi ziko (900 na)? na kiutafiti wangu wakati huo kwao maji, umeme, nyumba, kwao si tatizo hivyo walimu wakipangiwa huko wanakwenda bila kusita. je ukitoa dar nimkoa gani una vyuo vikuu vitano; MUCCOBS,KCMC, SMMUCO,MWUCE na MWIKA?.
Kwa kweli mimi nimeshalitafakari kwa muda mrefu kabila hili na ninaona hawa watu si wa kubeza na kupitia hilo limeshanipa changamoto nyingi kiasi kwamba na mimi kwa kiasi fulani nimefanikiwa kibiashara. Na siku nikiamua kuona nitaoa MCHAGA atakayenipenda ili wanangu wasiwe na elementi za uswaAhili jumla kama baba yao.
ILA SI LAZIMA KUWA RAIS KAMA ANAVYODHANI MMAKONDE.
NAWASILISHA.
Usiandike kwa kujifurahisha nafsi yako andika ili wenzako wapate chochote cha kujenga kutoka kwako.Chagga=jews
Naomba nikusahihishe kidogo kuhusu kujipendelea na umimi. Mimi ni mchagga na ninalifahamu kabila langu vizuri sana.Wachagga hatupendani hata kidogo.!Kinachotuletea maendeleo ni challenge! Wachagga tuna tabia ya kushushuana na ku-despise each other. Hata ndugu akitaka kufanya ki2 utasikia " mwache tuone kama ataweza". Hiyo ndiyo inayotupa changamoto na hasira ya maendeleo. Tofauti yetu na makabila mengine kama Wahaya ni kwamba huwa hatubebani kama wanavyobebana. Kwa wachagga kama huonyeshi uwezo wa kuweza kujisaidia hakuna atakayekupush.Nakubali wachaga ni watu wa maendeleo, lakini tatizo lao ni umimi wa kikabila, wao wanataka maendeleo kwa wao na kwa wachaga wenzao tu. Ila mchaga akiwa rais nadhani maendeleo yataonekana angalau kidogo kuliko watu wa pwani, yaani watajipendelea lakini watakumbuka na wengine, hawa watu wanajua kucheza na fulsa, pale mahali kabila lingine limeshindwa wao hufanikiwa, ni kama Jews wa Tanzania.
kwahiyo wewe kwako mzungu ni bora kuliko mwafrica?
you are the one who is cheap,tena nahisi you are "cost-less"
Usiandike kwa kujifurahisha nafsi yako andika ili wenzako wapate chochote cha kujenga kutoka kwako.
Mh. Mbowe anajinasibu sana kuwa ana mabiashara yake makubwa Nje na Ndani ya nchi, sijui ni biashara Gani zaidi ya hotel ambayo hata Sugu anayo.That's true kabisa...., sema sio watu wote wa pwani ni wazembe me ninawajua wengi and they are very intelligent..hata me mwenyewe nashangaa........... Sema wachache kama Dr,Dr,Dr baba ridhimoja..... Ni mahopless.
Kama Mbowe CHADEMATukubali kuwa Wenzetu wanapenda maendeleo.Nenda popote mijini Tanzania utawakuta,wawe wamesoma au kutosoma.
Nenda Mpwapwa,Singida ,Babati utawakuta.Mnaweza kupata mshahara mmoja,lakini Mchaga anafikiria kujenga kidogo kidogo.Atakunywa bia moja muda mrefu anafikiria miradi.
Nilipofika Moshi ,O-level miaka ya 80s ,nilishangaa.Niliona nyumba nzuri tu,wakati kula nikatoka ,ni nyumba za nyasi na watu wanalalia ngozi.Kabla ya utitiri wa secondari sasa,Nafikiri kipindi kile K'manjaro ilikuwa inaongoza kwa shule za sekondari.Tukubali wengi walikwenda shule mapema.Kwa hiyo kikabila wako overrepresented katika fani mbali mbali ,udaktari,uhandisi,accountants etc.
Nafikiri tungekuwa na Mchaga,baada ya Nyerere may be nchi yetu ingekwenda mbele zaidi maana wenzetu tutake tusitake wanajua nini maana ya maendeleo.Nawafahamu watu fulani(makabila mengine) wananyumba nzuri Dar,lakini ukifika kijijini walipozaliwa utashangaa!
Nimefanya kazi na wachaga nawaelewa sana.
Mh. Mbowe anajinasibu sana kuwa ana mabiashara yake makubwa Nje na Ndani ya nchi, sijui ni biashara Gani zaidi ya hotel ambayo hata Sugu anayo.Rudia yako ya kwanza. Unamtaka mchagga kwa sababu ya maendeleo yao. Kwanini usimtake mzungu au mjapani kwa maendeleo yake. Na kama unataka mtanzania mwenzako, ukienda Kagera wahaya nao hawakuchelewa kwani usitake muhaya?
Wakinga je?Tukubali kuwa Wenzetu wanapenda maendeleo.Nenda popote mijini Tanzania utawakuta,wawe wamesoma au kutosoma.
Nenda Mpwapwa,Singida ,Babati utawakuta.Mnaweza kupata mshahara mmoja,lakini Mchaga anafikiria kujenga kidogo kidogo.Atakunywa bia moja muda mrefu anafikiria miradi.
Nilipofika Moshi ,O-level miaka ya 80s ,nilishangaa.Niliona nyumba nzuri tu,wakati kula nikatoka ,ni nyumba za nyasi na watu wanalalia ngozi.Kabla ya utitiri wa secondari sasa,Nafikiri kipindi kile K'manjaro ilikuwa inaongoza kwa shule za sekondari.Tukubali wengi walikwenda shule mapema.Kwa hiyo kikabila wako overrepresented katika fani mbali mbali ,udaktari,uhandisi,accountants etc.
Nafikiri tungekuwa na Mchaga,baada ya Nyerere may be nchi yetu ingekwenda mbele zaidi maana wenzetu tutake tusitake wanajua nini maana ya maendeleo.Nawafahamu watu fulani(makabila mengine) wananyumba nzuri Dar,lakini ukifika kijijini walipozaliwa utashangaa!
Nimefanya kazi na wachaga nawaelewa sana.