TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 28,186
- 15,549
TOC yote haifaiHello!
Moja kwa moja kwenye mada!
Nikiwa O - level nimesoma na mwamba mmoja jamaa alikuwa anakimbia mita 100 kwa sekunde 13-15 tu. Ikumbukwe Bolt alikuwa anakimbilia kwa sekunde 9-10. Huyu wa sekunde 13-15 ni mtoto wa familia maskini, alikuwa mwanafunzi busy na masomo mbio anakimbia kwenye mashindano tu.
Huyu kijana kama atatumia muda wake wote au muda mwingi kupiga tizi sure atafika mbali. Ajabu ni kwamba jamaa hakubahatika hata kufika popote. Viongozi ndio mwiba.
Kijana mwingine wa mbio ndefu jirani yetu kule Lindi miaka kama 10 nyuma aling'ara na aliweza kuvunja rekodi za manguli wa riadha wa Dunia akiwa hapahapa Bongo. Tulitegemea angefika mbali. Kijana akiwa kwenye Kambi kuelekea Olympic huyo niliyemtaja juu akamla kichwa kwa sababu za hapa na pale.
Hofu ni kwamba angevunja rekodi yake na labda angekosa heshima anayoipata sasa .
Serikali vijana hawana pa kusemea dukuduku zao. Mchunguzeni huyu Mzee. Mtanishukuru.
Simbu sasa anang'ara kwakuwa ametokea jeshini hivyo kapata fursa za nje kupitia mgongo wa jeshi na sasa hawezi kumzuia.
Filbert Bayi achunguzwe na ikibaonika ni kweli alifanya hujuma yoyote ashitakiwe.
Ni wahuni, selfish and talents killers