Lakini Je, wangapi waliwahi kushitakiwa Mahakamani au hata kufungwa Jela kutokana na Ripoti ya CAG?

Lakini Je, wangapi waliwahi kushitakiwa Mahakamani au hata kufungwa Jela kutokana na Ripoti ya CAG?

Hakuna consequences zozote.

Rais kasema mkimkamata mwizi na mkakuta taratibu zenu za utumishi haziruhusu kumchukulia hatua basi mhamishieni kwenye kitengo ambacho hakina hela. Sasa kwa nini mkuu wa nchi asihoji, asizipinge na kuzibadilisha kanuni za utumishi zinazomlinda mwizi ?

Yeye huyo huyo jana hiyo hiyo katukana watu walioshindwa kuhoji vitu vya dhahiri visivyoingia akilini vinavyoliumiza Taifa kwamba ni watu stupid! Akarudia tena kwa Kiswahili "puumbav." Yeye huyo huyo!
Kwakweli nilimshangaa alivoshauri kwamba kama vipi wahamishwe. Naona mauzauza
 
Eee,Bhwanah!

Hebu tueleze wewe mtaalam kuhusu ile hela ya ndege, au hizi tenda za gharama ya chini kukataliwa na kuchuliwa ile ya aghali zaidi.
Hebu tueleze hilo nalo linakuwaje. Tupo tayari kujifunza toka kwako mkuu!
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
This is the annual drama - hapa wanakuja kulinganisha mijizi iliyovunja rekodi na kuweka mikakati mipya ya wizi na ubadilifu kwa mwaka ujao.

Haiwezekani watu wasababishe hasara Serikalini, waibe afu wasiwajibishwe.
 
Shida ukaguzi unafanyika kiuhasibu ila report inakuwa presented kisiasa.kumbuka CAG akikukuta huna supporting document ya matumizi yoyote hata kama yamefanyika kihalali utaambiwa umekula hizo pesa.Ndo maana kuchukuliwa hatua sio rahisi.
matumizi gani yanayofanyika kihalali bila supporting documents? Hizo ni fixi tu. Malipo lazima yaidhinishwe na mkuu wa taasisi au muhusika aliyeruhusiwa kisheria (kulingana na kiwango) na halafu kuwe na risiti za kuthibitisha matumizi.

Bila ya hivyo pesa zitakuwa zimepigwa tu.
 
Hili ni Swali ambalo Watanzania tunapaswa kujiuliza , kwamba kwa miaka mingi ofisi ya CAG imejitahidi sana kuanisha mapungufu , Wizi , upotevu na Uchafu wote unaofanywa kwenye mashirika na idara za serikali , wako walioonyeshewa vidole moja kwa moja ( Wengi wao majina yao yanafahamika )

Lakini kwa miaka yote hiyo hakuna hatua zozote za kisheria zimechukuliwa dhidi ya Watuhumiwa hao wanaofahamika ( niko tayari kusahihishwa ) .

Sisi Wananchi tumeanza kuitilia mashaka Serikali yetu kwamba ripoti ya CAG yaweza kuwa mbinu ya kizamani ya serikali ya ccm ya Kupumbaza wananchi ili waone kwamba serikali yao iko makini , CAG yuko Makini , Takukuru iko Makini , Rais anafokea wezi na mchwa wa Taifa , au Rais Kanuna nk . wakati kwenye ukweli Serikali haina umakini wowote ule , na ndio maana wezi wa Taifa wako kila mwaka na wengi wao baada ya kuharibu mahali pale wanahamishiwa pengine , ama wanapandishwa vyeo .

Sasa kwa kufupisha , Swali langu ni dogo tu , Ni akina nani waliotajwa kwenye ripoti ya CAG ambao waliwahi kushitakiwa Mahakamani au kuhukumiwa kwa Haki ?

Ni vzr hoja hii ijibiwe kikamilifu na wafia CCM wakiongozwa na Johnthebaptist!
 
.
 
Back
Top Bottom