Mtu Asiyejulikana
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 2,254
- 5,161
Toka miaka ya 90 moja ya utani kwa mtu anayependa vitu vya bure aende Mombasa. Kuwa kwa Mombasa unaweza enda kula sehemu ukataka kulipa wakakuambia ushalipiwa wewe.....
Ukaoneshwa mtu ambaye unaambiwa amekulipia unamwona anakuna ndevu zake akitabasamu. Hii hali na huu utani upo miaka nenda rudi. Unaweza pia msikiliza Solo Thang kwenye wimbo wake Mambo ya Pwani.
Kama haitoshi nenda kasikilize wimbo wa Wagosi wa Kaya... TANGA KUNANI
sijajua kwa nini hayo maeneo ya Upwa yamekuwa yakinasibishwa na tabia hizo za kifedhuli kwa miaka mingi. Tabia ya kuonedha kuwa kukirimiwa ni jambo baya. Haya mambo yamekuwa yakinichanganya. Nadhani kuna haja ya Mikoa au maeneo hayo kufanya jitihada za makusudi kujisafisha kuwa ukarimu si jambo baya.
Usikubali ukarimu wa kulipia huduma uendapo maeneo hayo. Hii ni dhana ambayo imekuwa ikipandikizwa kukataa utu wema unaooneshwa na watu wa huko. Kama ninyi Bara hampendi kusaidiana basi msitake watu wote waogope kulipiwa kitu au huduma.
Sawa tupo sisi wachache hatuamini katika ubinadamu na utu wema. Mimi binafsi siamini katika hilo. So sitaki kumlipia mtu wala kulipiwa. Kila mtu afe kivyake. Lakini sikatazi wengine wanapotaka kulipia au kulipiwa.