Land cruiser ipi mjapani alitulia kati ya hizi

Land cruiser ipi mjapani alitulia kati ya hizi

Tatizo ni kwamba unashindwa kunielewa au labda umeamua kutokunielewa au pia nimeshindwa kujieleza na kueleweka kwako kwa maana kujieleza na kueleweka wkt mwingine nayo siyo kazi rahisi!
Hiyo ya catalytic converter kama vile navigation system nimetoa kama mifano tu lkn vipo vingi kwa kifupi nilichotaka kusema ni kwamba Toyota for African market haimaanishi kwamba ina ubora dhaifu ukilinganisha na Toyota for US au Japan ni kwamba ziko tofauti kulingana na mahitaji na mazingira ya maeneo husika, hivyo kama lengo lako ni ubora kwa maana uhimili wa gari kama uko TZ ni bora ununue Toyota for African market na siyo Toyota for European au sijui Australian market kwa sababu utaishia kulipa fedha nyingi zaidi kwa mambo ambayo gari inayo lkn wewe hauyahitaji kwa matumizi ya TZ au Afrika na wakati mwingine tofauti inaweza kufika mpaka dola US 10 000, kuna sababu za msingi kwa nini wanaziita hivyo, ndicho nilichomaanisha!

Siwezi kununua Toyota meant for Africa market kama na uwezo cause kuna mapungufu mengi sana kwenye Quality Control, naona bado unakomalia kitu usichokijua.

Bro dont u have some other things to do cause unatia aibu hapa.
 
Kusema kweli mm huwa sijui matoleo ya magari haya lakini ukinipa landcruiser yako niisukume Dar to Arusha, hautakuja kunipa tena...kuna mzee mmoja alijichanganya siku moja akaniomba nimpeleke Tengeru...Hahahaa nilitumia masaa sita tu kutoka Dar...ila sijui ilikuwa ni toleo 86 au 100 maana naona yanafanana kwenye picha ulizozweka hapo juu
 
Una hela au unahusudu tuu? Maana ni dhambi kuusudu bila kuwa na hela matokeo yake
Utatamani
Then
Utaiba
Then
Utafungwa jela
Usimdharau aliye hai,maana kila mmoja ana bahati yake na hizo Gari zinaendeshwa na watu kama wewe,hakuna aliyezaliwa na Gari au utajiri ni juhudi na malengo katika maisha.
 
Usimdharau aliye hai,maana kila mmoja ana bahati yake na hizo Gari zinaendeshwa na watu kama wewe,hakuna aliyezaliwa na Gari au utajiri ni juhudi na malengo katika maisha.
Mbona unatokwa na mapovu? Mi nimetaadharisha tamaa, maneneno yake yanatamani , hataki anahusudu, nayo huzaa dhambi, au na wewe unatamani mkuu? Au ni hiyo chai na muwa?
 

Attachments

  • 1463723590140.jpg
    1463723590140.jpg
    47.9 KB · Views: 80
Siwezi kununua Toyota meant for Africa market kama na uwezo cause kuna mapungufu mengi sana kwenye Quality Control, naona bado unakomalia kitu usichokijua.

Bro dont u have some other things to do cause unatia aibu hapa.


Unatataka kununua gari ya aina gani huwo ni uamuzi wako kwa maana pesa ni yako pia lkn mimi nimekupa sababu ya kwanini zinaitwa hivyo yaani for African/EU/US/Japanese market!

Tatizo ni kwamba unaandika tu juu juu lkn hauendi ndani, unaposema ina mapungufu kwenye quality control unamaanisha nini?
Inaelekea unalishwa sana maneno ya vijiweni na wewe unakubali, ngoja nikuulize swali dogo sana unafahamu magari ambayo UN TZ wanatumia? Je unafikiri ni Toyota for European market au Toyota for African market?
Nakujibia swali, UN wote walioko Afrika pmj na Tanzania wanatumia magari ya Toyota yaliyotengenezwa for African market (tropical version), unafahamu ni kwa nini? kama kulingana na msemo wako ni kwamba hayana ubora?


Au unataka kuniambia wewe unaufahamu klk organization kubwa kama UN ambayo ina wataalamu wa kila fani?
Hata Serikali yetu yenyewe hainunui Toyota for EU au US market bali wananunua Toyota for African market (tropical version) sasa unajua ni kwa nini?
Hata ofisi za Kibalozi zote hapa TZ zinazotumia Toyota pmj na Ubalozi wa Ujapani wenyewe hawanunui Toyota zilizotengenezwa for EU au Austarlia market bali wananunua Toyota for African market sasa unajua ni kwa nini?
Ni kwa sababu zimetengenezwa ili ziendane na mazingira ya TZ/Afrika ambapo ni kawaida kwa mfano gari kuingia kwenye maji yanayofunika mpaka boneti hivyo kuna vitu maalumu wanavyoongezea/kupunguza ambavyo hauvihitaji ukiwa Ulaya au Ujapani lkn ukichukuwa BMW X5 ukaenda nayo Tunduru au Serengeti unaweza ukairudisha na umeibeba kwenye tela hiyo ndiyo sababu!
 
Mapovu unatoka we we,yawezekana hata Baiskel hauna,kama umekata tamaa ya kuvipata wengine bado hatujakata tamaa ya kuvipata,unatadharisha kama nani,au umemuendea kwa Wanganga kupiga ramli,sasa umepewa majibu?
 
Mbona unatokwa na mapovu? Mi nimetaadharisha tamaa, maneneno yake yanatamani , hataki anahusudu, nayo huzaa dhambi, au na wewe unatamani mkuu? Au ni hiyo chai na muwa?
Mtu mmejikatia tamaa,kila kitu unaona hauwezi wala kumiliki,sasa unadhani ni wote,hii ni hatari sana.
 
Huyu jamaa nimeoa nisibishane nae kwa sababu mie na yeye tuna utofauti mkubwa sana.

1. Yeye ana google ndo anarudi kuelezea kitu halafu bado anaigia chaka wakati mie natoa vitu kichwani sababu ya kuelewa hivi vitu kitambo.

2. Previous nimemtajia features kama Full option yeye kaja na nyigine ya catalytic converter kuongezea na kufanya andiko langu kuwa vivid halafu alivyo very mad akawa anajibishia mwenyewe bila kujua.

3. Hajawai endesha European Cars which means he doesn't qualify kubishana na mie so nikimwambia features kama Cruise Control hawezi nielewa wakati wenzetu wameanza kuitumia 80s,90s to date.

4. Atakua anasuffer matatizo ya akili sababu huwezi ongea kitu halafu unaji contradict mwenyewe kwa kupinga unachoongea within the same post.

5. Quallity ya magari inayoenda kwa wenzetu huko ni kubwa sana na hakuna chombo huku Africa kinachoweza mkosoa Japana kwenye Quality Control.

Najua huyu jamaa hafahamu ile case ya Toyota kwenye US market 2010 walivyotengeneza magari yana defect kwenye acceleration system ambayo ilisababisha sana ajali huko kwa wenzetu. Na magari hayo sie tunayanunua with same problems lakini tunajiona kama tupo peponi kwa kutojua.

Rais wa Toyota alitoa machozi na kuomba msamaha wamarekani kwa defect hiyo.




Angalia recall hiyo mwaka 2010 sio Barbarosa unaongea tu vitu usivyovijua.





Mimi nafikiri tunaongelea ktk ngazi tofauti kabisa, nimekwambia kwamba Kampuni zote za magari hutengeneza magari kulingana na mahitaji ya mahali husika ndiyo maana nikakupa mfano wa navigation system ambapo gari linalotengenezwa kwa matumizi ya Ngara, TZ halihitaji lkn kwa matumizi ya Ulaya ni standard, ukiangalia hata Audi inayotengenezwa kwa matumizi ya Ulaya ni tofauti na matumizi ya Uchina kulingana na mazingira ya Uchina lkn haimaanishi kwamba moja ni bora klk nyingine kila moja ni bora kulingana na mazingira yake!
 
Siwezi kununua Toyota meant for Africa market kama na uwezo cause kuna mapungufu mengi sana kwenye Quality Control, naona bado unakomalia kitu usichokijua.

Bro dont u have some other things to do cause unatia aibu hapa.
gari kwa soko la ulaya ni tofauti na gari kwa soko la afrika. kuna tofauti kubwa tu. ndio maana kuna gari za japan haziingii ulaya kabisa ila zimejaa afrika saaana. toa somo mkuu kwa wabishi
 
Had top 78 series zinayumba sana kwenye kona

Kutokana na kimo chake na pia stock tyres zinazotumika huwa zina impact katika balance ya gari, sema uzuri wake ni kwamba mwendo upo, inachanganya fasta
 
Ndio mkuu ndio same enginesm Engie za Ladcruiser most of them zinatumika na Coaster.

Engine za prado most of them zinatumika na Toyota Hiace
sema land cruiser 200 zinaboa hazina ile feel ya off road 4x4 halafu engine hata haina muito mzuri kama za 100 ama 80 series, pia mkunjo wa body umekaa kinyanya sana, at least hii facelift ya 2016 ipo na mvuto zaidi
 
En


Engine ni za Toyota kabisa na unatakiwa kufahamu kiwanda kilinunuliwa since 1998 platfoams zote za engine za Toyota.

Mfano

Lexus na Landcruiser za 100 series petrol engine zinatumia UZ series, Hii ni mfano kuna engines nyingi tu ila most ni UZ series



Duh! wewe mshikaji halafu unavyoandika kwa harufi kubwa kumbe haujui unapotosha hapa!
Toyota haijawahi kununua Lexus kama unavyotaka kuaminisha watu hapa bali Lexus ni brand iliyoanzishwa na Toyota ili kutengeneza luxurious version ya Toyota ambayo itashindana na likes za BMW's Audis &Co. na hazijawahi kuwa Kampuni (Toyota na Lexus) mbili tofauti bali Lexus imeanzishwa na Toyota!
 
Back
Top Bottom