LAPTOP inaharibika muda gani usipoizima bali inapiga mzigo

umejikausha hujaliona hilo jibu ama hujaliona kweli? screenshot hii

huyo jamaa umeona status yake? Admin wa dell hivyo ni mtu wao kwa ajili ya kujibu maswali kwenye official website ya dell. sasa mkuu wanaotengeneza laptop wenyewe wanasema ni safe, wewe nani huku unaetaka kutuaminisha vyengine na hata source ya uongo na kweli huna?
tofautisha battery kuachwa yenyewe kifaa kikiwa kimezimwa na hakitumiki na batttery kuachwa yenyewe hali ya kuwa kifaa kinatumika. ni vitu viwili tofauti na wala huwezi tumia huo mfano kwenye hii case.
 
Chief. Mbona unapoteza muda. Potezea
 
mimi naona njia nzuri ni kuweka ifanye hybernate kulko kusleep
Mimi kuizima ni ikitokea inainstall updates ila tofauti na hapo inasleep tu
mimi niligundua ni bora kufanya pc iwe ina hybernate kuliko kusleep jarbu hybernate utaona tofauti
 
Ushahidi Pls.

Simu zina miundo yake, kitochi hakipokei 1a ama 2a hata utumie hio chaja umeme unaingia kidogo kidogo kama kawaida, na hizo Habari za kwamba inaisha upesi ni za kijiweni otherwise leta ushahidi.
Nimelithibitisha mwenyewe sasa kama unataka ushahidi sijui waaje lakini hata wewe waweza jaribu simu unayo tumia charger ya 2A kucharge simu yenye batt ya 750 mah , ninacho ongea nimethibitisha mwenyewe na si kwa simu moja ni zaid ya moja na nimelifanyia utafiti kabisa

Mkuu chief mkwawa usicho kijua wewe haimaanishi hakipo na wala siwezi kuleta habari za vijiweni hapa kwa sababu mimi pia simtu wa viniweni
 
CHIEF MKWAWA ..kwamba hio screenshot hujasoma au? Me sielewi hata unachobisha ni kipi... nimekwambia huwa inajitafuna haraka ikikaa na volt nyingi that means ikiwa fully charged hio ndo elimu ya bure ya battery za li polymer au li ion ndo tabia zake ... .. bado unabisha ...huyo wa dell anaongelea swala la kuwa overcharged hilo haliwezi tokea ...


Basi kasome namna ya kuitunza any lithium battery utaona precaution zake ,,, dell enyewe wananunua hattery kwa panasonic ..legeza ubongo au nkuache ulivyo
 
Sababu unadanganya simu ndogo kama za tochi hazipokei hio 2A hata siku moja, sina mita ya kupimia hapa ila nikipata access nitaleta ushahidi.
 
So unacho Taka kutuambia hayo makampuni hayajui kuitunza battery kama hao dell? Lete basi huo ushahidi toka Panasonic? Ni ngumu sana kuleta ushahidi?

Na usidanganye watu kuhusu volt Sababu tayari laptop zina adapter, ile adapter kazi yake ni kutoa volt maalum, haiwezekani hata siku moja laptop ikapokea volt nyingi na ikitokea adapter is ifanye kazi yake na volt nyingi zikaingia basi jua BOOOM laptop inaungua.
 
Sawa Chief na laptop zipo tofauti masaa marefu laptop kukaa on battery charger disconnected ni masaa ngapi na laptop zipi hizo kama unaweza kuzifahamu ?
 
Sababu unadanganya simu ndogo kama za tochi hazipokei hio 2A hata siku moja, sina mita ya kupimia hapa ila nikipata access nitaleta ushahidi.
Unaposema hazipokei unamaanisha nini labda Chief-Mkwawa

sababu yawezekana wewe unaongea mambo ya kwenye madaftari na vitabu wakati mwenzio nimefanya utafiti tena zaid ya simu 10 ndio maana na hakika na ninacho ongea na simu ina charge bt within a short time inakwambia battery is fully charged lakini unavyo tumia charge ina isha haraka nina hakika na ninacho sema chief

Ila kwa baadhi ya simu hasa hizi genuine brand ndio zinaweza kutoa alerts kwamba ni over wattage over voltage sasa sijui unabishaje chief
 
Unasemaje volt hazina maana wat does it mean kujaa kwabattery ,,, lithium zinajaa kwa 4.3v or 4.2v ..hizo volt zinakula ile chemical kule ndani zikikaa hapo muda mrefu ..hata kama situmii nitapunguza kidogo siwezi acha ikae mia hata kwa nusu saa natoa chaji
 
Kichwa chako kigumu sana kuelewa ...nimekwambia legeza ubongo ..kama hujanywa chai kunywa uje usome tena
 
Mkuu circuit ya simu inajua ipokee amps ngapi, unapozidisha amps inachuja yenyewe amps inazotaka. Ukitumia chaja ya 2A kwenye kitochi inachujwa mpaka amps husika ambazo manufacture mwenyewe ameamua.

Unless unaongelea visimu vya kichina copy za mtaani, nina Samsung ya kitochi hapa, nitatafuta mita ya amps nikipata baadae nitatumia fast charge na 2A charger kukuthibitishia ninacho sema.
 
Mkuu ushaambiwa battery haiwez kuwa overcharged, ikijaa umeme unaenda moja kwa moja kwenye power supply ya laptop hauendi tena kwenye battery hizo cell zitaliwa vipi?

Na usikariri 4v, cell moja ina chajiwa na around 3.7v kwa laptop zinakuwa na cell zaidi ya moja, battery nyingi za laptop ni zaidi ya hizo volt, mfano hii hapa ya muda kweli ni volts zaidi ya 10.

Yani assumption zako wewe ni kama wanao tengeneza hivi vifaa ni mambumbu vyote unavyotaja hawavioni.
 
Sawa Chief na laptop zipo tofauti masaa marefu laptop kukaa on battery charger disconnected ni masaa ngapi na laptop zipi hizo kama unaweza kuzifahamu ?
Unamaanisha laptop zinazokaa na chaji mda mrefu?
 
Kama simu yangu tu inakaaga hata weeks 3 siizimi naichaji ikifikia 5% tu na haijawahi kuniletea shida yoyote iwe ya bettery, oS, wala joto na ina miaka 3 sasa, Naipigia kazi sana kuliko hata laptop, leo hii ww computer unataka kuizima zima kisa nini mkuu?

Pigia kazi tu mradi kama haina tatizo lolote na haichemki..
 

Kichwa chako kigumu sana ....lithium zote nominal ni 3.7 or 3.8 zikijaa zinakuwa na 4.2 au 4.3

Ndo mana niliandika per bank hukuelewa unajibu kulingana na akili yako inavokutuma...

Hiyo picha uliotuma ina battery 6 ndani zenye 2200mah kila moja na nominal volt ya 3.6 volt

Ukikuta lithium inasoma volt nyingi zaidi basi jua wameweka kadhaa in series and parrallel connection ku achieve volt wanataka...

Na hakuna sehemu nimesema itakuwa overcharge haiwezi labda hio system utengeneze wewe

Nimekwambia higher volt per battery inakula hizo chemical haraka sana ...nimekwambia soma post zangu zote kama ninmwelewa utaelewa ulichofanya ww ni kuja ku comment kabla hujarudia soma......hayo mavitu sijui battery uliotuma nayajua than you think na ndo mana nimeweza kwambia ina battery ngap ndani bila kufungua kama huamin kaangalie mwenyewe ...najua test zote battery zinapitia pia nina imax ya kupimia battery niliagiza
 
Kuna mwngne atabisha tena....according to test battery zinapitia...life cycle unaweza double kama utatumia kati ya 34% to 80 yani muda wote ipo hapo ...usifikishe 100 kama haina ulazima ndicho nabishana na jamaa ...naweza fika 100% kama naondoka karbu na socket ...simu ina karbu 2yrs haijawah zima charge ..sina amani kuitumia ikiwa na below 30% ...mpaka sasa kama imepungua mah basi ni kwa kiwango kidogo sana ....itakuwa bado inanipa over 90% but not 100%

Huwa natumia over 8hrs bila kioo kuzima hata kidogo
 
Jamaa muongo wewee, battery ninayo mwenyewe nimepiga picha mwenyewe picha inaonesha kabisa ina 4200mah, ila wewe unasema ina cell 6 za 2200mah?

Kwa hio hao kina Lenovo na dell hawajui kiasi cha volt Kinachotakiwa kiingie kwenye battery?
 
Acha ubishi basi jamaa yangu na nimekuchunguza wewe ni wale ma electrician wa kwenye vitabu na madesa wenzio tupo field ninacho kwambia ninahakika nacho 100% naona hutaki kushindwa haya.

Nina samsung kitochi hapa SM -B310E Nimesha jaribu zaid ya mara 10 nina hakika na ninacho sema chief

Hayo yote unayo yasema sijui circuit sijui nini si kwamba siyajui ni theories hizo nimejiridhisha pasipo shaka na nisemacho

Hii simu ina 800Mah nikicharge na charger ya smartphone yenye 2. A haikai na charge kwa siku inazo kaa kama nikicharge na charger yake yenye 300Mah pamoja na kwamba nikitumia charger ya smart inajaa mapema sana tofauti na nikicharge na charger yake ya 300Mah.
 
Mimi pia ninayo na inakaa na chaja what's your point? Na kwanini hutaki ushahidi?

Wabongo mnapenda kuongea vitu bila facts mtu akitaka kuleta facts inakua tabu pia?

Na mimi sijahudhuria course yoyote ya umeme wala madaftari unayo sema sina ni natumia pia uzoefu,

Hio ni logic ya kawaida tu ukitumia chaja yenye amps kubwa simu inachuja ina chukua amps inazotaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…