LATRA: Serikali imeridhia ongezeko la nauli za Mwendokasi, kufikia Tsh. 1,000

LATRA: Serikali imeridhia ongezeko la nauli za Mwendokasi, kufikia Tsh. 1,000

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa sasa nauli ya mpito kwa mabasi ya mwendokasi kwa baranara ya BRT 1 Kimara, Morocco pamoja na ile ya BRT 2 inayohusisha Mbagala hadi Kivukoni itakuwa ni shilingi elfu moja baada ya mapendekezo yaliyoletwa na DART.

Akizungumza baada ya kutembelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya mabasi yaendayo haraka(DART), Mkurugenzi wa LATRA, Dkt Habibu Suluo kwenye maonesho ya wiki ya tathimini ya uchukuzi yanayofanyika Jijini Arusha, amesema walipokea maombi ya nauli mpya za mabasi yaendayo haraka tangu Agosti 29 hivyo kwa sasa wameridhia matumizi ya nauli ya shilingi 1,000.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DART, Said Tunda amesema hatua ya DART kupendekeza nauli ya shilingi elfu moja inatokana na maombi ya wawekezaji wanaotoa huduma katika miundombinu ya Dart ambao waliomba nauli hiyo ili iendane na uwekezaji na huduma wanazozitoa.

Pia soma ~ LATRA: Nauli Mwendokasi (DART) kwanini imepandishwa bila taarifa?

==============================​

CPA DKT. SULUO: NAULI ZA DART NI ZA MPITO
CPA Dkt. Habibu Suluo, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) amesema Shilingi 1000 wanazotozwa abiria wanaotumia usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ni nauli ya mpito na nauli halisi zitatumika baada ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuwasilisha maombi ya nauli mpya.

CPA Dkt. Suluo amebainisha hayo Desemba 17, kwenye Maonesho ya Mkutano wa 18 wa Tathmini ya Utendaji kazi wa Sekta ya Uchukuzi uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kuanzia Desemba 15 hadi 17, 2025.

“Nauli ya mpito ya BRT iliridhiwa kuwa shilingi 1,000 kwa Tangazo la Serikali la Agosti 29, 2025 na hii ilikuwa inawapa uhakika wale wanaoleta mabasi kuwa nauli hii wanaweza wakaanza nayo hadi pale DART itakapoleta maombi rasmi ya mapendekezo ya nauli baada ya kukaa na watoa huduma wa usafiri huo. Kwa sasa nauli hizi zinamtosheleza mtoa huduma kutopata hasara lakini kutopata faida ili aingie sokoni na anaweza akaona faida kwa sababu abiria ni wengi, lengo la kuweka nauli hii ni kuwavutia wawekezaji wengine kutoa huduma,” amesema CPA Dkt. Suluo.

Pia CPA Dkt. Suluo ameipongeza DART kwa kutatua changamoto ambazo zilibainika hapo awali na kufanikisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, “Mamlaka ilifanya ziara ya mradi wa BRT awamu ya pili na kabla ya kutangazwa kwa nauli ya shilingi 1,000 kulikuwa na changamoto kwenye uendeshaji ambapo changamoto hiyo ilitatuliwa na huduma za usafiri zikaanza kutolewa. Tunawapongeza na kuwashukuru kwa uboreshaji wa BRT awamu ya pili kwenye mfumo wa kukusanya nauli pamoja na mabasi kuwa mengi hali iliyopelekea mabasi 60 kuazimwa kwenda BTR awamu ya kwanza,” amesema CPA Dkt. Suluo.

Kwa upande wake Bw. Said Tunda, Mtendaji Mkuu DART amesema kuwa, “Serikali inawajali sana wananchi wake ndio maana hata baada ya kuharibika miundombinu iliyosababisha changamoto ya usafiri kwa wananchi, huduma zinaendelea katika vituo vingi vya mwendokasi kwa kulipia gharama ya shilingi 1,000 tu ambapo ni ongezeko la shilingi 250 kutoka nauli ya awali,” amesema Bw. Tunda.

Aliongeza kuwa, nauli ya shilingi 1,000 inafaa kwa kuanzia kwani lengo sio kuwaumiza watumia huduma bali ni kuhakikisha abiria wanapata huduma bora na endelevu kwani wakati huduma za BRT hazipo, abiria walikuwa wanatozwa hadi shilingi 6,000 kwa safari moja walipotumia vyombo vidogo vya usafiri.

Kwa mujibu wa Kanuni za LATRA za Tozo za mwaka 2020, watoa huduma wanatakiwa kutoa matangazo ya nauli mpya kwa siku kumi na nne (14) kabla ya kuanza kutumia nauli mpya kupitia vyombo vya habari vinavyowafikia watu wengi.
 
Attachments

hayo ni matayarisho ya kuuza (kugawa) mwendokasi, kwani atakayegawiwa ni lazima ataongeza nauli, serikali imenunua mabasi mapya kwa kodi zetu halafu inayagawa bure kwa watu binafsi kuyaendesha, kama wanataka watu binafsi waendesha wanunue mabasi kwa fedha zao na kulipia matumizi ya miundo mbinu pia kama kodi ...
 
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa sasa nauli ya mpito kwa mabasi ya mwendokasi kwa baranara ya BRT 1 Kimara, Morocco pamoja na ile ya BRT 2 inayohusisha Mbagala hadi Kivukoni itakuwa ni shilingi elfu moja baada ya mapendekezo yaliyoletwa na DART.

Akizungumza baada ya kutembelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya mabasi yaendayo haraka(DART), Mkurugenzi wa LATRA Dkt Habibu Suluo kwenye maonesho ya wiki ya tathimini ya uchukuzi yanayofanyika Jijini Arusha, amesema walipokea maombi ya nauli mpya za mabasi yaendayo haraka tangu Agosti 29 hivyo kwa sasa wameridhia matumizi ya nauli ya shilingi elfu moja.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DART, Said Tunda amesema hatua ya DART kupendekeza nauli ya shilingi elfu moja inatokana na maombi ya wawekezaji wanaotoa huduma katika miundombinu ya Dart ambao waliomba nauli hiyo ili iendane na uwekezaji na huduma wanazozitoa.
People are eating people aka dogs eat dogs world. Ila mishahara kwa watumishi haiongezeki na huku mambo mengine wakipandisha. Yaani bana huu mfumo wa serikali sijui nchi Kuna watu wachache mno naamanisha wachache mno wanatafuna wengi. Juzi mtt akapewa uwaziri anawahamasisha wengine wakaajiri ilhali na yeye hakujiairi, amekaa anapiga meza tu 18M inaingia
 
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa sasa nauli ya mpito kwa mabasi ya mwendokasi kwa baranara ya BRT 1 Kimara, Morocco pamoja na ile ya BRT 2 inayohusisha Mbagala hadi Kivukoni itakuwa ni shilingi elfu moja baada ya mapendekezo yaliyoletwa na DART.

Akizungumza baada ya kutembelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya mabasi yaendayo haraka(DART), Mkurugenzi wa LATRA Dkt Habibu Suluo kwenye maonesho ya wiki ya tathimini ya uchukuzi yanayofanyika Jijini Arusha, amesema walipokea maombi ya nauli mpya za mabasi yaendayo haraka tangu Agosti 29 hivyo kwa sasa wameridhia matumizi ya nauli ya shilingi elfu moja.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DART, Said Tunda amesema hatua ya DART kupendekeza nauli ya shilingi elfu moja inatokana na maombi ya wawekezaji wanaotoa huduma katika miundombinu ya Dart ambao waliomba nauli hiyo ili iendane na uwekezaji na huduma wanazozitoa.
Bado haitishi kuweza kutoa huduma kwa ufanisi. Inapswa kuwa Tsh 1,500 ili waweze kugharamia uendeshaji wa kampuni (operations cost) na replacement ya magari chakavu
 
Wapande wenyewe eboo!
Utapanda tu utake usitake maana zile zingekuwa plan B yako (daladala) wameziondoa wamekuachia bodaboda na Bajaj.

So uamuzi wako ukampe sa100 elfu moja yake uwahi uendako (japo hizo gari zenyewe hazipo za kutosha) au ukapande bodaboda akuingize uvunguni mwa mwendokasi ubaki mlemavu,Bajaj kuingia town Tsh 4,000/= in short hakuna jinsi ya kukwepa.
 
Umetumwa kuja kuniharibia siku na samuya siyo, sitaki kusikia huu upuuzi wa serikali ya mbogamboga mbele yangu.
 
Wanaopanda mwendokasi siyo walala hoi na watu wenye ajira zao serikalini....mimi mlala hoi nina almost miaka miwili silijui mwendo kasi
 
Maisha ya DSM sio lelemama.

Mwendokas kwenda elfu 1 na kurud elfu 1 (jumla 2k).
Wengne ukishuka utapanda either bajaji au pikipik kwenda kituon na kurud home (jumla 2k).
Hujala mchana na asubuh kwa kujibana (jumla 5k).

Hapo almost 10k kila siku.
Na hapo haujalipia huduma nyingne za kujikimu. Kama Chakula cha familia . Kodi. Vocha. Bill za maji na umeme nk.

Hapo bado una mipango yako mingine ya maendeleo.

Kwa mwendo huu hauwez kuacha kutapel, Kula rushwa au kudanga.

Fursa zipo ila Mjini pagumu.
 
sawa,je mtatoa service nzuri au ndiyo ya kuswaga ngombe

ova
 
Back
Top Bottom