LATRA: Serikali imeridhia ongezeko la nauli za Mwendokasi, kufikia Tsh. 1,000

hayo ni matayarisho ya kuuza (kugawa) mwendokasi, kwani atakayegawiwa ni lazima ataongeza nauli, serikali imenunua mabasi mapya kwa kodi zetu halafu inayagawa bure kwa watu binafsi kuyaendesha, kama wanataka watu binafsi waendesha wanunue mabasi kwa fedha zao na kulipia matumizi ya miundo mbinu pia kama kodi ...
Mkuu Mofat kanunua mabasi yake. Halafu hata phase 1 nauli iliopendelezwa ilikuwa 1,200/- ipa Magu na siasa zake mara uzalendo akakaza nauli ikawa 750/- na ndio maana ilibidi yaemdeshwe kama daladala ili kuwalipa na matokeo yake wote tumeyaona. Pia uendeshaji mbovu nao.
Ila kwa nauli hii ya 1000/- na muendeshaji binafsi natumaini hiduma itakuwa nzuri. So far so good Mbagala-Gerezani/Kivukoni wanainjoi maisha. Na hawapiti madirishani kama ilivyotarajiwa.
 
Maisha ya DSM sio lelemama.

Mwendokas kwenda elfu 1 na kurud elfu 1 (jumla 2k).
Wengne ukishuka utapanda either bajaji au pikipik kwenda kituon na kurud home (jumla 2k).
Hujala mchana na asubuh kwa kujibana (jumla 5k).

Hapo almost 10k kila siku.
Na hapo haujalipia huduma nyingne za kujikimu. Kama Chakula cha familia . Kodi. Vocha. Bill za maji na umeme nk.

Hapo bado una mipango yako mingine ya maendeleo.

Kwa mwendo huu hauwez kuacha kutapel, Kula rushwa au kudanga.

Fursa zipo ila Mjini pagumu.
Zipo njia za kukwepa hizo gharama.
1. Kutembea
2.Kutumia baiskeli
3. Kununua bodaboda
Otherwise nauli ni mji wowote mkubwa labda vijijini ndio hamna commuter buses.
 
HUU MRADI HUWA SIYO KUMUSAIDIA MWANANCHI BALI KUMKAMUA KODI.NI BORA TUNGEACHANA NA HUU MRADI TUKAJIKITA KUPANUA BARABARA ILI KILA MMOJA APITE KWENYE HIZO BARABARA KAMA ILIVYO KIMARA HADI MBEZI.MWENDOKASI ILISTAHILI NAULI IWE TS500 KWA SABABU BARABARA ZIMEJENGWA KWA KODI YA WANANCHI NA WANAPITA PEKE YAO(hawana mshindani)
 
Mkuu Mofat kanunua mabasi yake. Halafu hata phase 1 nauli iliopendelezwa ilikuwa 1,200/- ipa Magu na siasa zake mara uzalendo akakaza nauli ikawa 750/- na ndio maana ilibidi yaemdeshwe kama daladala ili kuwalipa na matokeo yake wote tumeyaona. Pia uendeshaji mbovu nao.
Ila kwa nauli hii ya 1000/- na muendeshaji binafsi natumaini hiduma itakuwa nzuri. So far so good Mbagala-Gerezani/Kivukoni wanainjoi maisha. Na hawapiti madirishani kama ilivyotarajiwa.

swali ni kwamba hayo mabasi kanunua nani? mwekezaji au serikali? ...
 
Mwekezaji

kwa mujibu wa ai ni serikali imenunua

''the Tanzanian government, through the Dar es Salaam Rapid Transit Agency (DART) and local operator Mofat Company Limited, has acquired a large fleet of new, gas-powered (CNG) Bus Rapid Transit (BRT) buses from China (Golden Dragon) for the Dar es Salaam BRT Phase Two, with deliveries and operations ramping up in 2025 to improve public transport.''

hivyo ni wizi kama wizi mwingine tu, na hakuna mwekezaji hapo, hayo ni madili ya wizi na hakuna kitu serikali itapata, ni kama mradi wa parking kwenye stendi ya ubungo ya kina kingunge ngombale mwilu hakuna tofauti, watachukuwa fedha na kulipa peanut serikalini baada ya muda mfupi miundo mbinu itakuwa imeharibika na serilaki itapaswa kurepair kwa kutumia kodi za wananchi lkn faida inakwenda kwa watu binafsi ambao hata kodi hawalipi na mradi utakufa, ndiyo maana wanangangania madaraka na wako tayari kuuwa hata nchi nzima sababu ni hiyo, wizi na dhuluma.

mwekezaji wa kweli angekwenda benki akakopa fedha na kununua mabasi kwa fedha yake kuyaweka barabarani na yeye ndiyo anakuwa responsible kama yakiharibika au akishindwa kurudisha deni atajuana na benki alikokopa na siyo serikali itumie kodi za wananchi kununua mabasi halafu faida inakwenda kwa watu binafsi, huo ni wizi, wake up man ...
 
Mtendaji Mkuu wa DART, Said Tunda amesema hatua ya DART kupendekeza nauli ya shilingi elfu moja inatokana na maombi ya wawekezaji wanaotoa huduma katika miundombinu ya Dart ambao waliomba nauli hiyo ili iendane na uwekezaji na huduma wanazozitoa.
Si walisema sasa mwekezaji Rostam Aziz anatumia gesi kwa hiyo nauli itashuka?
 
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema kwa sasa nauli ya mpito kwa mabasi ya mwendokasi kwa baranara ya BRT 1 Kimara, Morocco pamoja na ile ya BRT 2 inayohusisha Mbagala hadi Kivukoni itakuwa ni shilingi elfu moja baada ya mapendekezo yaliyoletwa na DART.

Akizungumza baada ya kutembelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya mabasi yaendayo haraka(DART), Mkurugenzi wa LATRA, Dkt Habibu Suluo kwenye maonesho ya wiki ya tathimini ya uchukuzi yanayofanyika Jijini Arusha, amesema walipokea maombi ya nauli mpya za mabasi yaendayo haraka tangu Agosti 29 hivyo kwa sasa wameridhia matumizi ya nauli ya shilingi 1,000.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DART, Said Tunda amesema hatua ya DART kupendekeza nauli ya shilingi elfu moja inatokana na maombi ya wawekezaji wanaotoa huduma katika miundombinu ya Dart ambao waliomba nauli hiyo ili iendane na uwekezaji na huduma wanazozitoa.

Pia soma ~ LATRA: Nauli Mwendokasi (DART) kwanini imepandishwa bila taarifa?

==============================​

CPA DKT. SULUO: NAULI ZA DART NI ZA MPITO
CPA Dkt. Habibu Suluo, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) amesema Shilingi 1000 wanazotozwa abiria wanaotumia usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) ni nauli ya mpito na nauli halisi zitatumika baada ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuwasilisha maombi ya nauli mpya.

CPA Dkt. Suluo amebainisha hayo Desemba 17, kwenye Maonesho ya Mkutano wa 18 wa Tathmini ya Utendaji kazi wa Sekta ya Uchukuzi uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) kuanzia Desemba 15 hadi 17, 2025.

“Nauli ya mpito ya BRT iliridhiwa kuwa shilingi 1,000 kwa Tangazo la Serikali la Agosti 29, 2025 na hii ilikuwa inawapa uhakika wale wanaoleta mabasi kuwa nauli hii wanaweza wakaanza nayo hadi pale DART itakapoleta maombi rasmi ya mapendekezo ya nauli baada ya kukaa na watoa huduma wa usafiri huo. Kwa sasa nauli hizi zinamtosheleza mtoa huduma kutopata hasara lakini kutopata faida ili aingie sokoni na anaweza akaona faida kwa sababu abiria ni wengi, lengo la kuweka nauli hii ni kuwavutia wawekezaji wengine kutoa huduma,” amesema CPA Dkt. Suluo.

Pia CPA Dkt. Suluo ameipongeza DART kwa kutatua changamoto ambazo zilibainika hapo awali na kufanikisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, “Mamlaka ilifanya ziara ya mradi wa BRT awamu ya pili na kabla ya kutangazwa kwa nauli ya shilingi 1,000 kulikuwa na changamoto kwenye uendeshaji ambapo changamoto hiyo ilitatuliwa na huduma za usafiri zikaanza kutolewa. Tunawapongeza na kuwashukuru kwa uboreshaji wa BRT awamu ya pili kwenye mfumo wa kukusanya nauli pamoja na mabasi kuwa mengi hali iliyopelekea mabasi 60 kuazimwa kwenda BTR awamu ya kwanza,” amesema CPA Dkt. Suluo.

Kwa upande wake Bw. Said Tunda, Mtendaji Mkuu DART amesema kuwa, “Serikali inawajali sana wananchi wake ndio maana hata baada ya kuharibika miundombinu iliyosababisha changamoto ya usafiri kwa wananchi, huduma zinaendelea katika vituo vingi vya mwendokasi kwa kulipia gharama ya shilingi 1,000 tu ambapo ni ongezeko la shilingi 250 kutoka nauli ya awali,” amesema Bw. Tunda.

Aliongeza kuwa, nauli ya shilingi 1,000 inafaa kwa kuanzia kwani lengo sio kuwaumiza watumia huduma bali ni kuhakikisha abiria wanapata huduma bora na endelevu kwani wakati huduma za BRT hazipo, abiria walikuwa wanatozwa hadi shilingi 6,000 kwa safari moja walipotumia vyombo vidogo vya usafiri.

Kwa mujibu wa Kanuni za LATRA za Tozo za mwaka 2020, watoa huduma wanatakiwa kutoa matangazo ya nauli mpya kwa siku kumi na nne (14) kabla ya kuanza kutumia nauli mpya kupitia vyombo vya habari vinavyowafikia watu wengi.
Barabara kodi zetu na hazitupi unafuu.
Mbona mabasi binafsi nauli ni affordable?

Dawa ni kuwaondoa hao wawekezaji warudi kwao. Sisi siyo shamba la bibi.

Watajuta
 
Kama hiyo 1000 ni bei ya mpito, tutegemee bei halisi baada ya wawekezaji kutulia kuwa zaidi ya hapo.

Ni lini walikaa na wadau wakajadili hilo ongezeko, kuna ripoti ya Cag miaka kama mitatu iliyopita alipendekeza mwendo kasi kutumia gesi ili kuokoa mamilioni ya pesa ambayo walikuwa wanatumiaa kwa kununua mafuta.
kwanini baada ya mwendokasi kuanza kutumia gesi bei iongezeke badala ya kupungua.
huyo jamaa haitendei cpa yake haki.
 
Uranium inatusaidia nini sasa?
 
WANAMTANDAO WANAFANYA BIASHARA IKULU,MWENDOKASI YA ROSTAM !!NAULI HAZITAPUNGUA KWA MTANZANIA HATA KIDOGO TUENDELEE KUWA MASKINIIII
 
Back
Top Bottom