LATRA tunaomba usafiri wa daladala katika barabara kutoka Goba njia nne kupitia Madale kwenda Tegeta

LATRA tunaomba usafiri wa daladala katika barabara kutoka Goba njia nne kupitia Madale kwenda Tegeta

Kidenga

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
233
Reaction score
676
Wasaalam Mlioko humu ndani. Kichwa cha habari chahusika.

Kutokana na kukamilika kwa ujenzi wa barabara kutoka njia nne kwenda Tegeta Nyuki ambapo tumeona magari mengi ya mikoani yanayoenda mikoa ya kaskazini yakipita katika barabara hii.

Ni wakati mwafaka kwa LATRA kupanga route ya Daladala kutoka Makumbusho-Goba-Njianne-Madale-Tegeta nyuki. Pia route nyingine ya Mbezi mwisho Njia nne Madale Tegeta nyuki.

Hizi route mbili zitasaidia sana kupunguza adha ya usafiri wanayokumbananayo watu wanaoishi katika maeneo niliyoyataja kwani ngarama za kuunganisha unganisha safari kwa bodaboda na bajaji ni kubwa sana.

Wahusika tunaomba mjitahidi kushughulikia hili swala mapema iwezekanavyo.
 
Kama imekamilika siyo suala la LATRA tu bali hata wenye magari wanapaswa kuomba kuanza route mpya ili hao latra waone umuhimu.

Pamoja na yote nitaona tija kama kutakuwepo na long route inayoanzia bunju kwenda mbezi mwisho kupitia hiyo njia hata nauli ikiwa 800 itakuwa route nzuri na italipa sana.
 
Mbezi-nyuki tayari yameanza, ila yapo machache
 
Kama imekamilika siyo suala la LATRA tu bali hata wenye magari wanapaswa kuomba kuanza route mpya ili hao latra waone umuhimu.

Pamoja na yote nitaona tija kama kutakuwepo na long route inayoanzia bunju kwenda mbezi mwisho kupitia hiyo njia hata nauli ikiwa 800 itakuwa route nzuri na italipa sana.
Umeboresha asante
 
Back
Top Bottom