BALENSIAGA
JF-Expert Member
- Aug 27, 2019
- 3,353
- 5,800
Itatagemea karudia kosa mara ngapiMmoja afungiwe kwa kosa hilohilo wengine wapewe onyo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Itatagemea karudia kosa mara ngapiMmoja afungiwe kwa kosa hilohilo wengine wapewe onyo
Niko kuwaza juu ya hili kwanini wengine wapewe onyo tu na Mwingine afungiwe ikiwa kesi ni moja.?Hapa kuna visa hapa inawezekanaje wengine wapewe onyo halafu katarama afungiwe ? Wakati wote makosa yao yanafanana?
Kwa hiyo unataka ajali itokee kwanza ndio wachukue hatua?Hapana hapa kuna wivu na visa na sio bure , hii nchi ndiyo maana hatupati wawekezaji wapya na waliopo wanahama ,viongozi wanamambo ya kipuuzi sana sana,
Kuna kampuni kila siku zinasababisha ajali kizembe na hazifungiwi wana msakama tu muwekezaji , nantangu kaanza usafirishaji hajawahi kupata ajali hata mara moja ila kuna kampuni zina sababisha ajali kila mara, viongozi wa latra kuweni waadilifu
Kuchezea VTD ndio kaonewa?Hapana hapa kuna wivu na visa na sio bure , hii nchi ndiyo maana hatupati wawekezaji wapya na waliopo wanahama ,viongozi wanamambo ya kipuuzi sana sana,
Kuna kampuni kila siku zinasababisha ajali kizembe na hazifungiwi wana msakama tu muwekezaji , nantangu kaanza usafirishaji hajawahi kupata ajali hata mara moja ila kuna kampuni zina sababisha ajali kila mara, viongozi wa latra kuweni waadilifu
Ni Tanzania pekee watu wakisimamia sheria za nchi, raia wanaona wanaonewa ila wasimamia sheria wasipozisimamia wanaoneaka hawajali.Ila hata hivyo hii hoja bado haitoshi kutuhamisha kwenye mjadala wa utekaji na mauaji
Katarama ni onyo la 3Hapa kuna visa hapa inawezekanaje wengine wapewe onyo halafu katarama afungiwe ? Wakati wote makosa yao yanafanana?
Shida sio mwendo.Kuna vitu vinavifikirisha sana wakuu inawezekanaje katarama inaingia mwanza alafu iinafata ally badae isamilo nayo inafika muda si mrefu! Vp kuhusu vithibiti mwendo awe amechezea katarama peke yake wakati kampuni kama ally's na nyinginezo zinamwaga moto vibaya mno barabarani inamana latra wanashindwa kuona yote hayo au kuna conflict of interest hapo kiukweli nina maswali mengi sana lakini yanakosa majibu
Zaidi ya mara 3. Huwa analipa faini.Uenda alishapewa sana onyo mara nyingi kwa kukiuka sheria .
Katarama ni kosa la 3.Niko kuwaza juu ya hili kwanini wengine wapewe onyo tu na Mwingine afungiwe ikiwa kesi ni moja.?
kweli mkuu ila ndugu zetu wakipotea na kuokotwa wamekufa hadithi inakua tofautiUenda alishapewa sana onyo mara nyingi kwa kukiuka sheria .
Naona watu wengi mmekua upande wake kwamba kaonewa lakini tambueni madreva wake wanakiuka sana sheria za barabarani tuiachie serikali ifanye kazi yake tusiwe upande wa ushabilki ndugu zetu wengi wamepoteza maisha au kupata ulemavu wa maisha kutokana na na uzembe wa mwenye makampuni ya mabasi kuruhusu madreva wao wavunje sheria.
Hii imekaa vibaya sana ni uonevu wa hali ya juu sana kiukweli viongozi wetu wanatugawa sana mtu anapambana kukuza mtaji wake alafu anatokea mtu mmoja kuja kuharibu ugali wa familia yakeHapo ni visa tuu na roho mbaya za rushwa kwa hawa viongozi wenye madaraka si bure maana makosa hayo mbona ni ya mabasi yote, hapo wanataka kumkomoa kupitia viongozi wa hovyo wa serikali
Naona Abood na wengine wamepewa onyo hata mimi nina mashaka na hiyo hukumu yao ni Vita ya biashara na jamaa ana DNA za marehemu Sauli ana uthubutu wa kuleta vyuma kweli hao Tanzania hawatakiwi..Kuchezea VTD ndio kaonewa?
Kwa nini wengine hawachezei?
Umeandika kishabiki sana, hawajamfungia kwa vile hajawahi pata ajali, bali kavunja sheria za leseni ya usafirishaji abiria. Na sio wa kwanza kupewa adhabu hiyo.
Abood ni onyo la kwanza.Naona Abood na wengine wamepewa onyo hata mimi nina mashaka na hiyo hukumu yao ni Vita ya biashara na jamaa ana DNA za marehemu Sauli ana uthubutu wa kuleta vyuma kweli hao Tanzania hawatakiwi..
Hizo bus zote zinatembea na king'amuzi kinapiga kelele toka mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari hasa kwa safari za usiku ujanja ujanja tu.Abood ni onyo la kwanza.
Huyo kosa hilo hilo amerudia mara 3 na mara zote amekuwa akilipa faini.
Onyo mwisho ni mara mbili, ya tatu unachukuliwa hatua
Mnyama SCANIA hakupewa onyo, kaadhibiwa direct.. Michina yote imepewa onyo na muda🥺😂Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani imefanya kikao na wasafirishaji wa mabasi ya Mkoani ili kuwakumbusha kuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani.
Aidha, LATRA imesitisha Leseni ya kusafirisha abiria kwa kampuni ya mabasi ya KATARAMA Luxury kutokana na kuchezea kifaa cha kufuatilia mwenendo wa magari (VTD)
Kufuatia kikao hicho, Mamlaka imetoa onyo kali ya wiki moja kwa ABOOD Bus Service, BM Coach na SUPER FEO kwa kosa la kuchezea mfumo wa mwenendo wa magari (VTS) na kukiuka masharti ya leseni walizopewa na kuwataka wasafirishaji wote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.
Kikao hicho kimefanyika Ofisi ya LATRA Dar es Salaam, Septemba 12, 2024 na kuhudhuriwa wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania (TABOA), Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, pamoja na Wamiliki na Wawakilishi wa Makampuni hayo.
170 kph kwa barabara ipi kwa mfano? Au umeandika tu kwa kuwa unajua kusoma?kifaa haki cap mwendo, bali huwapa taarifa latra bus ipo speed ngapi
wanang'oa ICs wanaweka zingine, inatuma taarifa ya uongo, like 60kph mda wote wakati chuma iko 170kph
Sijui hata unachotaka.Maustaadhi bhana
Hizo bus zote zinatembea na king'amuzi kinapiga kelele toka mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari hasa kwa safari za usiku ujanja ujanja tu.
Ni kosa la 3Mnyama SCANIA hakupewa onyo, kaadhibiwa direct.. Michina yote imepewa onyo na muda🥺😂