LATRA yasitisha leseni ya kampuni ya mabasi ya Katarama

Kwa hiyo unataka ajali itokee kwanza ndio wachukue hatua?
 
Kuchezea VTD ndio kaonewa?
Kwa nini wengine hawachezei?
Umeandika kishabiki sana, hawajamfungia kwa vile hajawahi pata ajali, bali kavunja sheria za leseni ya usafirishaji abiria. Na sio wa kwanza kupewa adhabu hiyo.
 
Ila hata hivyo hii hoja bado haitoshi kutuhamisha kwenye mjadala wa utekaji na mauaji
Ni Tanzania pekee watu wakisimamia sheria za nchi, raia wanaona wanaonewa ila wasimamia sheria wasipozisimamia wanaoneaka hawajali.
 
Hapa kuna visa hapa inawezekanaje wengine wapewe onyo halafu katarama afungiwe ? Wakati wote makosa yao yanafanana?
Katarama ni onyo la 3
Hao wengine ni la 1.

Unaweza kuona alieonywa mara 3 na haachi maana yake anafanya makusudi.
 
Shida sio mwendo.
Hivyo vifaa vinatakiwa kutuma taarifa za kweli Latra, yaani kama yuko 80km/h ionekane hivyo kule Latra. Walichofanya katarama ni ku temper na hiyo system akiwa 80km/h kule latra inatuma taarifa za uongo 50km/h.
 
kweli mkuu ila ndugu zetu wakipotea na kuokotwa wamekufa hadithi inakua tofauti
 
Au kawatikisa mabosi[emoji1783][emoji1783][emoji1783][emoji1783]
 
Hapo ni visa tuu na roho mbaya za rushwa kwa hawa viongozi wenye madaraka si bure maana makosa hayo mbona ni ya mabasi yote, hapo wanataka kumkomoa kupitia viongozi wa hovyo wa serikali
Hii imekaa vibaya sana ni uonevu wa hali ya juu sana kiukweli viongozi wetu wanatugawa sana mtu anapambana kukuza mtaji wake alafu anatokea mtu mmoja kuja kuharibu ugali wa familia yake
 
Kuchezea VTD ndio kaonewa?
Kwa nini wengine hawachezei?
Umeandika kishabiki sana, hawajamfungia kwa vile hajawahi pata ajali, bali kavunja sheria za leseni ya usafirishaji abiria. Na sio wa kwanza kupewa adhabu hiyo.
Naona Abood na wengine wamepewa onyo hata mimi nina mashaka na hiyo hukumu yao ni Vita ya biashara na jamaa ana DNA za marehemu Sauli ana uthubutu wa kuleta vyuma kweli hao Tanzania hawatakiwi..
 
Naona Abood na wengine wamepewa onyo hata mimi nina mashaka na hiyo hukumu yao ni Vita ya biashara na jamaa ana DNA za marehemu Sauli ana uthubutu wa kuleta vyuma kweli hao Tanzania hawatakiwi..
Abood ni onyo la kwanza.
Huyo kosa hilo hilo amerudia mara 3 na mara zote amekuwa akilipa faini.
Onyo mwisho ni mara mbili, ya tatu unachukuliwa hatua
 
Maustaadhi bhana
Abood ni onyo la kwanza.
Huyo kosa hilo hilo amerudia mara 3 na mara zote amekuwa akilipa faini.
Onyo mwisho ni mara mbili, ya tatu unachukuliwa hatua
Hizo bus zote zinatembea na king'amuzi kinapiga kelele toka mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari hasa kwa safari za usiku ujanja ujanja tu.
 
Mnyama SCANIA hakupewa onyo, kaadhibiwa direct.. Michina yote imepewa onyo na muda🥺😂
 
kifaa haki cap mwendo, bali huwapa taarifa latra bus ipo speed ngapi
wanang'oa ICs wanaweka zingine, inatuma taarifa ya uongo, like 60kph mda wote wakati chuma iko 170kph
170 kph kwa barabara ipi kwa mfano? Au umeandika tu kwa kuwa unajua kusoma?
 
Maustaadhi bhana

Hizo bus zote zinatembea na king'amuzi kinapiga kelele toka mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari hasa kwa safari za usiku ujanja ujanja tu.
Sijui hata unachotaka.
Anyway iwe kama upendanvyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…