LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

Kwahiyo unataka kusemaje ndugu mfalme juha , maana ni kama umefanya kila kitu kuwa kawaida imekua kanuni sasa, hebu nikuulize wanaotumia UBER na wasafiri wa ma BUS ya mkoani unataka kuniambia haya makundi ya watu wanafanana kiuelewa maana kuna watu wanakaa vijijini huko ndani ufahamu huo unaotaka kuulinganisha ni upi mzee
Huko vijijini nani aliwafundisha Mpesa?tuanzie hapo. ni kwakua tu Uber haipo vijijini ila ingekuepo wangeitumia na ungeshangaa wanaitumiaje...mambo ya select destination then..next next confirm yanahitaji Elimu gani?tena App yenyewe imeandikwa kwa kiswahili km Mpesa...ukiniambia mtandao ntakuelewa ila sio Elimu.
 
[emoji625]SOMENI

“Mfumo huu utaisaidia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kutambua idadi ya watu wanaosafiri kwenda maeneo mbali mbali hivyo itapanga huduma za usafiri kulingana na mahitaji ya eneo ya njia husika, mamlaka zinazohusika zitakuwa na uwezo wa kupanga sera za usafirishaji na ujenzi wa miundombinu kutambua maeneo ya kipaumbele ya usafirishaji”alisema .Waziri Kamwelwe alisema mfumo huo utatumika kwa majaribio hadi kufikia Juni 2020 na baada ya hapo leseni haitotolewa kwa mmiliki ambaye hajajiunga na mfumo huu ili kuhakikisha kila mmiliki anatumia mfumo huu.

“Kufikia Septemba 2020 utekelezaji uanze kwa upande wa daladala nawaagiza kusimamia kanuni kikamilifu hususan mfumo huu kila atakaye kuja kuchukua leseni lazima aunganishwe na mfumo huu”alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu LATRA Gilliard Ngewe alisema kupitia mfumo huo watoa huduma hawatodanganywa tena kuhusu mapato yao kwani kila abiria anaponunua tiketi moja kwa moja hela ya mmiliki itakwenda benki na mwenyewe kupatiwa ujumbe kiasi cha pesa na idadi ya wateja watakao hudumiwa kwa siku .

“Tajiri atafunga mahesabu mwenyewe na si wakala tena ,tumejipanga kikamilifu kusimamia utoaji huduma kwa mfumo huu na maafisa wetu watashirikiana na Jeshi la Polisi kutoa elimu kuhakikisha wananchi wote wananufaika na mfumo huu na tutakuwa na kituo cha huduma kwa wateja ambacho kitazinduliwa hivi karibuni watu kupitia namba 0800110150 watapiga na kupata elimu juu ya mfumo huu”alisema.

Alisema mwananchi kwa kutumia simu ya mkononi ataweza kununua tiketi ya basi analotaka aina ya kiti na kupangiwa muda wa safari.

Alisema katika ulipaji wa tiketi abiria ataletewa ujumbe kwenye simu ujumbe ambao utampa maelekezo ya kufanya malipo na mara baada ya kukamilisha atapatiwa ujumbe mwingine ambao utakuwa tiketi yake atakayolazimika kuitunza ili kuingia nayo katika basi.
[emoji625]SOMENI

Pia kwa abiria ambao hawatakuwa na simu janja hawatosumbuka Kwani watakapofika vituoni watakatiwa tiketi hizo kwa kifaa maalumu kiitwacho POS .

Mbali na hilo alisema abiria watanufaika zaidi kwani kwa kutumia mfumo huo watakuwa na uwezo wa kuchagua kituo cha kupanda basi pamoja na kushuka.

Mkurugenzi wa Imani Class Amani Kaganda ambaye tayari ameanza kutumia mfumo huo kwa majaribio alisema faida za mfumo huo ni nyingi kwani mmiliki wa basi anajua fedha alizoingiza kwa siku na kuanza kupanga matumizi yake .

“Fedha naipata kwa wakati sisumbuki na watu kunipa hesabu pia nina uhakika na abiria wanaoingia kwenye gari”alisema.

Njoo utoe Tahadhari Tena
Erythrocyte
Asante sana kwa bandiko hili Nextman
 
Hizo ticket tutazipata kupitia website ya LATRA au kwa namna ipi?
 
Huko vijijini nani aliwafundisha Mpesa?tuanzie hapo. ni kwakua tu Uber haipo vijijini ila ingekuepo wangeitumia na ungeshangaa wanaitumiaje...mambo ya select destination then..next next confirm yanahitaji Elimu gani?tena App yenyewe imeandikwa kwa kiswahili km Mpesa...ukiniambia mtandao ntakuelewa ila sio Elimu.

Mkuu utake usitake jambo jipya hasa la kielektroniki litakalotumiwa na umma kwa wingi elimu inahitajika usikatae kufafanuliwa, usijifananishe wewe na watu wengine
 
Asante sana kwa bandiko hili Nextman
[emoji625]Hii ni Taarifa Since May 2020

Alafu mtu anakuja anasema Serikali inaleta Maagizo kwa kushtukiza, alafu blah blah kibao vingereza viiiiingi ilimradi tuu na yeye aonekane amepinga

Moja ya sifa kubwa ya serikali ya Tanzania kufanya maamuzi kwa kushtukiza, bila kushirikisha wadau au kufanya pilot study. Na maamuzi yao siku zote yanakuwa ni amri zinazotolewa on short notice. Hili agizo halitekelezeki kirahisi na litaleta shida kubwa.
 
[emoji625]Hii ni Taarifa Since May 2020

Alafu mtu anakuja anasema Serikali inaleta Maagizo kwa kushtukiza, alafu blah blah kibao vingereza viiiiingi ilimradi tuu na yeye aonekane amepinga
Walifanya pilot study? Wameshirikisha wadau? Kuongoza kwa amri za kushtukiza ndiyo jadi yenu.
 
Walifanya pilot study? Wameshirikisha wadau? Kuongoza kwa amri za kushtukiza ndiyo jadi yenu.
Ni wajibu wao wakutafute wakuambie ?

AU

Ni wajibu wako kutafuta taarifa ?

[emoji625]Soma hiyo
Miaka 2 iliyopita wamiliki wa mabasi walikutana kujadili suala hili. Kwenye kile kikao bwana Joseph Kasheku "King Msukuma" naye alikuwapo kama mmliki wa mabasi.

Siku hiyo aliongea hoja yake ni Kwa mabasi yanayofanya safari za vijijini ambapo mtandao ni shida itakuwaje, kama tiketi zikigoma kutoka Kwa hiyo na Basi lisiondoke kufanya safari. Akajibiwa mtandao utaboreshwa sehemu zote.
 
View attachment 1667700

Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini ( LATRA ) imetangaza kwamba hadi kufikia January 6 mwaka 2021 mabasi yote yawe yameanza kutumia tiketi za mtandao , vinginevyo watafungiwa kutoa huduma hiyo .

Bado haijajulikana sababu hasa za wenye mabasi ya abiria kulazimishwa kufuata utaratibu huu mpya huku wakitozwa kodi lukuki ambayo wanailipa bila mizengwe yoyote.

Tahadhari : kama una safari ya muhimu ni bora ukafanya hivyo kabla ya tarehe hiyo , maana lolote la kukukwamisha laweza kutokea .

Nakulilia Tanzania .
Kama kawa wanatengeneza tatizo mkuu anakuja kutengua ili aonekane kipenzi na mtetezi wa wapiga debe
 
View attachment 1667700

Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini ( LATRA ) imetangaza kwamba hadi kufikia January 6 mwaka 2021 mabasi yote yawe yameanza kutumia tiketi za mtandao , vinginevyo watafungiwa kutoa huduma hiyo .

Bado haijajulikana sababu hasa za wenye mabasi ya abiria kulazimishwa kufuata utaratibu huu mpya huku wakitozwa kodi lukuki ambayo wanailipa bila mizengwe yoyote.

Tahadhari : kama una safari ya muhimu ni bora ukafanya hivyo kabla ya tarehe hiyo , maana lolote la kukukwamisha laweza kutokea .

Nakulilia Tanzania .
Acha ujinga tunaolipa kodi ni sisi abiria, wenye mabasi ni wakala tu wa kukusanya kodi! Kinawashinda nini kutoa ticket za kielectroniki? Tatizo wanataka faida wale na kodi ya serikali waile! tunajenga nchi sisi ni lazima tulipe kodi, waache janjajanja!
 
Back
Top Bottom