LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

[emoji625]SOMENI

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Mhandisi Kamwelwe alisema mfumo wa tiketi mtandao utaondoa upotevu wa mapato kwa wasafirishaji ambayo mara nyingi hupotelea katika mikono ya wapiga debe.

“Utawawezesha wasafirishaji kukopesheka kwa urahisi kwani taarifa za miamala yao zitaakisi moja kwa moja katika mabenki,pia utasaidia kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta kutokana na kuongezeka kwa mapato”alisema.

Mhandisi Kamwelwe alisema kwa upande wa abiria matumizi ya mtandao katika kununua tiketi utawaondolea abiria mlolongo wa kufunga safari kwenda vituo vya mabasi siku moja kabla ya safari waajili ya kukata tiketi.

“Pia utaondoa kero za abiria kubughudhiwa kwenye vituo vya mabasi na kufanya usafiri huu kuwa na heshima zaidi,utakomesha vitendo vya upandaji holela wa nauli hususan kipindi cha mwisho wa mwaka “alisema.

Alisema kwa upande wa Serikali mfumo huo utawezesha kupatikani kwa taarifa muhimu zenye kusaidia Serikali kufikia maamuzi sahihi kwakuwa ndio kitovu cha usafirishaji nchini.
 
View attachment 1667700

Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini ( LATRA ) imetangaza kwamba hadi kufikia January 6 mwaka 2021 mabasi yote yawe yameanza kutumia tiketi za mtandao , vinginevyo watafungiwa kutoa huduma hiyo .

Bado haijajulikana sababu hasa za wenye mabasi ya abiria kulazimishwa kufuata utaratibu huu mpya huku wakitozwa kodi lukuki ambayo wanailipa bila mizengwe yoyote.

Tahadhari : kama una safari ya muhimu ni bora ukafanya hivyo kabla ya tarehe hiyo , maana lolote la kukukwamisha laweza kutokea .

Nakulilia Tanzania .
TAno tena.
Hii nchi ni ya kipumbavu.

Inawezekana elimu waliyopata hawa wakubwa wetu ni useless
 
Wakati Uber inakuja bongo ni Elimu gani ya Kutosha tulipewa hasa sisi abiria?or wakati Mpesa inaingia kwenye market ni Elimu gani ilitolewa?issue inapokuaga ni ya serikali ndo hua tunalilia Elimu ya kutosha..Elimu ipi sasa tunataka itolewe?Mbona ukienda supermarket ukalipa ukapewa risiti hua hatuombi Elimu ya ile system ya kutoa risiti?Heb tuwe sereous aisee

Kwahiyo unataka kusemaje ndugu mfalme juha , maana ni kama umefanya kila kitu kuwa kawaida imekua kanuni sasa, hebu nikuulize wanaotumia UBER na wasafiri wa ma BUS ya mkoani unataka kuniambia haya makundi ya watu wanafanana kiuelewa maana kuna watu wanakaa vijijini huko ndani ufahamu huo unaotaka kuulinganisha ni upi mzee
 
[emoji625]SOMENI

“Mfumo huu utaisaidia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kutambua idadi ya watu wanaosafiri kwenda maeneo mbali mbali hivyo itapanga huduma za usafiri kulingana na mahitaji ya eneo ya njia husika, mamlaka zinazohusika zitakuwa na uwezo wa kupanga sera za usafirishaji na ujenzi wa miundombinu kutambua maeneo ya kipaumbele ya usafirishaji”alisema .Waziri Kamwelwe alisema mfumo huo utatumika kwa majaribio hadi kufikia Juni 2020 na baada ya hapo leseni haitotolewa kwa mmiliki ambaye hajajiunga na mfumo huu ili kuhakikisha kila mmiliki anatumia mfumo huu.

“Kufikia Septemba 2020 utekelezaji uanze kwa upande wa daladala nawaagiza kusimamia kanuni kikamilifu hususan mfumo huu kila atakaye kuja kuchukua leseni lazima aunganishwe na mfumo huu”alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu LATRA Gilliard Ngewe alisema kupitia mfumo huo watoa huduma hawatodanganywa tena kuhusu mapato yao kwani kila abiria anaponunua tiketi moja kwa moja hela ya mmiliki itakwenda benki na mwenyewe kupatiwa ujumbe kiasi cha pesa na idadi ya wateja watakao hudumiwa kwa siku .

“Tajiri atafunga mahesabu mwenyewe na si wakala tena ,tumejipanga kikamilifu kusimamia utoaji huduma kwa mfumo huu na maafisa wetu watashirikiana na Jeshi la Polisi kutoa elimu kuhakikisha wananchi wote wananufaika na mfumo huu na tutakuwa na kituo cha huduma kwa wateja ambacho kitazinduliwa hivi karibuni watu kupitia namba 0800110150 watapiga na kupata elimu juu ya mfumo huu”alisema.

Alisema mwananchi kwa kutumia simu ya mkononi ataweza kununua tiketi ya basi analotaka aina ya kiti na kupangiwa muda wa safari.

Alisema katika ulipaji wa tiketi abiria ataletewa ujumbe kwenye simu ujumbe ambao utampa maelekezo ya kufanya malipo na mara baada ya kukamilisha atapatiwa ujumbe mwingine ambao utakuwa tiketi yake atakayolazimika kuitunza ili kuingia nayo katika basi.
 
[emoji625]SOMENI

Pia kwa abiria ambao hawatakuwa na simu janja hawatosumbuka Kwani watakapofika vituoni watakatiwa tiketi hizo kwa kifaa maalumu kiitwacho POS .

Mbali na hilo alisema abiria watanufaika zaidi kwani kwa kutumia mfumo huo watakuwa na uwezo wa kuchagua kituo cha kupanda basi pamoja na kushuka.

Mkurugenzi wa Imani Class Amani Kaganda ambaye tayari ameanza kutumia mfumo huo kwa majaribio alisema faida za mfumo huo ni nyingi kwani mmiliki wa basi anajua fedha alizoingiza kwa siku na kuanza kupanga matumizi yake .

“Fedha naipata kwa wakati sisumbuki na watu kunipa hesabu pia nina uhakika na abiria wanaoingia kwenye gari”alisema.

Njoo utoe Tahadhari Tena
Erythrocyte
 
[emoji625]SOMENI

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo Mhandisi Kamwelwe alisema mfumo wa tiketi mtandao utaondoa upotevu wa mapato kwa wasafirishaji ambayo mara nyingi hupotelea katika mikono ya wapiga debe.

“Utawawezesha wasafirishaji kukopesheka kwa urahisi kwani taarifa za miamala yao zitaakisi moja kwa moja katika mabenki,pia utasaidia kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta kutokana na kuongezeka kwa mapato”alisema.

Mhandisi Kamwelwe alisema kwa upande wa abiria matumizi ya mtandao katika kununua tiketi utawaondolea abiria mlolongo wa kufunga safari kwenda vituo vya mabasi siku moja kabla ya safari waajili ya kukata tiketi.

“Pia utaondoa kero za abiria kubughudhiwa kwenye vituo vya mabasi na kufanya usafiri huu kuwa na heshima zaidi,utakomesha vitendo vya upandaji holela wa nauli hususan kipindi cha mwisho wa mwaka “alisema.

Alisema kwa upande wa Serikali mfumo huo utawezesha kupatikani kwa taarifa muhimu zenye kusaidia Serikali kufikia maamuzi sahihi kwakuwa ndio kitovu cha usafirishaji nchini.
Umefafanua vyema
 
View attachment 1667700

Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini ( LATRA ) imetangaza kwamba hadi kufikia January 6 mwaka 2021 mabasi yote yawe yameanza kutumia tiketi za mtandao , vinginevyo watafungiwa kutoa huduma hiyo .

Bado haijajulikana sababu hasa za wenye mabasi ya abiria kulazimishwa kufuata utaratibu huu mpya huku wakitozwa kodi lukuki ambayo wanailipa bila mizengwe yoyote.

Tahadhari : kama una safari ya muhimu ni bora ukafanya hivyo kabla ya tarehe hiyo , maana lolote la kukukwamisha laweza kutokea .

Nakulilia Tanzania .
Nimekata ila namba ya kukatia ni siri yangu na LATRA.
 
Tuki rely kwenye huu mfumo, tukiingia kwenye vipindi vya uchaguzi wasije wakatuzimia tena mitandao sijui tutalipaje hizo tiketi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],
Mkuu umeona mbali sana!!
 
Asilimia kubwa ya wachangiaji wa mada hii wamekurupuka kujibu bila hata kujua huo mfumo unafanyaje kazi

Lengo la technologia yoyote ni kufanya mambo yafanyike kwa speed, ufanisi na urahisi zaidi

Kwanza hapa nipende kuipongeza serekali maana abiria hua wanapigwa sana kwenye bei za tickets za vitabu ila kwa hizi za mashine itakua ngumu Kuweka udalali hivyo unalipia nauli halali iliyoandikwa kwenye ticket
 
Mleta mada kaingiza watu mkenge ndio maana mkanganyiko umekuwa mkubwa.

huu mfumo ni mfumo wa kawaida wa ukataji ticket kwa njia ya kielektroniki kwa kutumia Efd machine ahusiani na matumizi ya simu janja au computer kama wengi mlivyoelewa.
 
Daah jambo zuri sanaa..

Hivi naombeni kujua nauli kutoa dar adi nzega Bei gani?
Na bus gani zuri?
 
Back
Top Bottom