Changamoto hapa zipo nyingi, usitazame suala la kwenda na tecnolojia.
Unapoliendea Jambo Fulani ni lazima upime na madhara yake au uangalie pande zitakazoathiri.
Vinginevyo ndiyo hiyo watu wanasema utawala huu ni was kidictator. NI AMRI TU.
1. WADAU
Serikali ilitakiwa ikae na wadau husika( wamiliki vya mabasi) wajadiri na kuona athari zitakazopatikana.
2. WAPIGA DEBE NA MAWAKALA
Ajira haikubuniwa na serikali, ni kama kondoa au mbuzi amekosa mchungaji akatafuta namna ya kujilisha, japokuwa wapiga debe wanakera lakini madhara yao siyo makubwa.
Ni wajibu wa serikali kubuni mbinu mbalimbali za kuwatafutia ajira wananchi wake, Sasa Hawa vijana wamejitafutia ajira je serikali imefikiria hatima ya maisha yao?
Waturudi mitaani na wengine walitoka kwenye wizi,ujambazi.
Wengine ni mateja, watarudi mitaani,je usalama utakuwepo?
Suala hili hata wizara ya Mambo ya ndani hususa idara ya polisi ingehusishwa ili itoe maoni juu ya madhara yatakayotokea mitaani.
Japokuwa suala hili lilisikika kipindi Cha nyuma lakini zipohatua hazijapitiwa.
Watawala wasifikirie maziwa tu bali wafikirie ng'ombe wanaowakamua na wachungaji pia
Watanzania ni wajinga Sana,lakini ipo siku Mungu atawaondolea ujinga wao na ndipo hatari itakuwa kubwa.
Tunasoma maandiko kuwa uasi ulianzia mbinguni,huyu tunayemwita shetani na mapepo,majini malikuwa malaika lakini waliasi na Vita vikapiganwa Mbinguni. WENYE MAMLAKA MSIRAHISISHE KILA JAMBO.
HERI YA MBOGA ZA KONDENI NA AMANI
KULIKO UTAJIRI NA MACHAFUKO.
Cc, Pascal Mayalla,bia yetu, magonjwa mtambuka.
Niwaone kwenye Uzi huu muoneshe uzalendo wenu,isiwe mnaonekana kwenye nyuzi za kusifia tu.