LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

LATRA yawataka wenye mabasi ya abiria kuanza kutumia tiketi za mtandao, watakaoshindwa kufanya hivyo kufutiwa leseni

Sasa mtu wa buchosa ndani ndani akitaka ticket na kwenye mambo ya kutumia mtandao yuko chini inakuwaje hapo

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Kuna wakala wa kukatisha ticket kwa mtandao mabasi yote ... kama unavotaka kununua umeme wa luku huko ndanindani ananunuaje ?
 
Sio kwamba sisi ambao ni wahusika wa kusafiri tutakuwa tumepata unafuu maana tutakata tiketi elekezi?? Kama ni elfu kumi basi ni elfu kumi hakuna kudalaliwa??
𝑵𝒂𝒅𝒉𝒂𝒏𝒊 𝒊𝒕𝒂𝒌𝒖𝒘𝒂 𝒏𝒂𝒇𝒖𝒖
 
Hivi mnaposema wadau hawakushirikishwa, ina maana huko serikali kumejaa wajinga kiasi kwamba wafikirie kuanzisha kitu bila kushikisha wadau.?

Mawakala na Wapiga debe watapotezaje ajira.?
Hebu jiulize, kwanini itoke kauli kuwa atakaepinga kufutiwa leseni.
Happy panaushirikishwaji wadau, huoni huu ni ubabe?

Ukisoma mada tulia Kwanza ili ubongo ufanye kazi take Sasa na ikupe uelewa, maana wengine akili ni nzito
 
Hebu jiulize, kwanini itoke kauli kuwa atakaepinga kufutiwa leseni.
Happy panaushirikishwaji wadau, huoni huu ni ubabe?

Ukisoma mada tulia Kwanza ili ubongo ufanye kazi take Sasa na ikupe uelewa, maana wengine akili ni nzito
Hivi kwanini serikali isilete mabasi yake ili kuwakomoa wamiliki wabishi ?
 
Hebu jiulize, kwanini itoke kauli kuwa atakaepinga kufutiwa leseni.
Happy panaushirikishwaji wadau, huoni huu ni ubabe?

Ukisoma mada tulia Kwanza ili ubongo ufanye kazi take Sasa na ikupe uelewa, maana wengine akili ni nzito
Wadau gani unawasemea wewe ?

Mbona tunakua wazito hivi
Sio Swala la Jana wala Juzi hili
Soma hapo chini


Miaka 2 iliyopita wamiliki wa mabasi walikutana kujadili suala hili. Kwenye kile kikao bwana Joseph Kasheku "King Msukuma" naye alikuwapo kama mmliki wa mabasi.

Siku hiyo aliongea hoja yake ni Kwa mabasi yanayofanya safari za vijijini ambapo mtandao ni shida itakuwaje, kama tiketi zikigoma kutoka Kwa hiyo na Basi lisiondoke kufanya safari. Akajibiwa mtandao utaboreshwa sehemu zote.
 
Si ajabu hata hawa madalali nao wakaihuka na janja yao kwenye hizi tiket
 
Haya mambo ni mazuri kwa sababu yanaongeza wigo wa ukusanyaji kodi lakini Kasoro zake ni kama hivi:
1.Ushirikishwaji wa stakeholders na kutoa Elimu ya kutosha kwa wote-Mlaji na agent wa kodi.
2.Target au kiasi kinachotegemewa kukusanywa kutoka kwenye mfumo huo na Tija ya huo mfumo iwekwe wazi.Mfano kwenye mafuta tunajua kuna pesa Ya REA so watu wako Happy kulipa kwa sababu wanajua tija zilizoko.
3.Pilot,TRIALS.
Mfumo mpya upate muda wa majaribio nk nk
Mtaelewa tu, nyie wenzetu kila kitu mnaanza na vikwazo.
Tanesco wakati wanaleta mfumo wa kununua umeme kwa simu mlianza hivihivi.
Kipindi kikwete analeta BVR napo mlianza hivihivi.
 
Changamoto hapa zipo nyingi, usitazame suala la kwenda na tecnolojia.
Unapoliendea Jambo Fulani ni lazima upime na madhara yake au uangalie pande zitakazoathiri.

Vinginevyo ndiyo hiyo watu wanasema utawala huu ni was kidictator. NI AMRI TU.

1. WADAU
Serikali ilitakiwa ikae na wadau husika( wamiliki vya mabasi) wajadiri na kuona athari zitakazopatikana.

2. WAPIGA DEBE NA MAWAKALA
Ajira haikubuniwa na serikali, ni kama kondoa au mbuzi amekosa mchungaji akatafuta namna ya kujilisha, japokuwa wapiga debe wanakera lakini madhara yao siyo makubwa.

Ni wajibu wa serikali kubuni mbinu mbalimbali za kuwatafutia ajira wananchi wake, Sasa Hawa vijana wamejitafutia ajira je serikali imefikiria hatima ya maisha yao?
Waturudi mitaani na wengine walitoka kwenye wizi,ujambazi.
Wengine ni mateja, watarudi mitaani,je usalama utakuwepo?
Suala hili hata wizara ya Mambo ya ndani hususa idara ya polisi ingehusishwa ili itoe maoni juu ya madhara yatakayotokea mitaani.

Japokuwa suala hili lilisikika kipindi Cha nyuma lakini zipohatua hazijapitiwa.
Watawala wasifikirie maziwa tu bali wafikirie ng'ombe wanaowakamua na wachungaji pia

Watanzania ni wajinga Sana,lakini ipo siku Mungu atawaondolea ujinga wao na ndipo hatari itakuwa kubwa.
Tunasoma maandiko kuwa uasi ulianzia mbinguni,huyu tunayemwita shetani na mapepo,majini malikuwa malaika lakini waliasi na Vita vikapiganwa Mbinguni. WENYE MAMLAKA MSIRAHISISHE KILA JAMBO.

HERI YA MBOGA ZA KONDENI NA AMANI
KULIKO UTAJIRI NA MACHAFUKO.
Cc, Pascal Mayalla,bia yetu, magonjwa mtambuka.
Niwaone kwenye Uzi huu muoneshe uzalendo wenu,isiwe mnaonekana kwenye nyuzi za kusifia tu.
Hao wenye mabasi walishashirikishwa na wakaukubali huo mfumo na baadhi walishaanza kuutumia muda tu mrefu, mfano Darlux, shabiby, nbs
Kuhusu wapiga debe na mawakala kushirikishwa, kumbuka wapiga debe hawatambuliwi , hakuna sehemu ambapo mpiga debe anatambuliwa.
Wakala yeye atamalizana na wamiliki wa mabasi, kwa maana hiyo maelekezo atapewa na wamiliki wa mabasi wanayoyahudumia.
Wengi sijui mkisikia ticket za kielectronic mnaelewa nini? Hizo ticket ni kama zile za mwendokasi, kwa tafsiri rahisi hakutakuwa na ticket za vitabu. Bali ticket zitakatwa kwa mashine na hao mawakala
 
hawa LATRA watatununulia na smart phone ili tamko lao kushtukiza lisogee
Wenzetu mna ubongo kweli? Smartphone ya nini?? Kwani ticket ya mwendokasi inahitaji uwe na smartphone?
Hizo ticket ni kama zile za mwendokasi
 
9

Hapa wale jamaa wanaogombea abiria nje ya stendi wapate kula ndio kiyama chao sasa
kimefika.

Kivipi? Wenzetu sijui hata kama mna vichwa.
Mawakala watakuwepo kama kawaida na wao ndio watakuwa wanakata hizo ticket, wapiga debe wao kazi yao ni kukupeleka kwa wakala
 
Wadau gani unawasemea wewe ?

Mbona tunakua wazito hivi
Sio Swala la Jana wala Juzi hili
Soma hapo chini
Wewe ndiyo mzito, umekomalia jambo jepesi kabisa, kwani watu na wadau wakipewa elimu wewe kinakuuma nini mzee, halafu hiyo elimu unayoisema ilitolewa ilitolewa kwenye platform gani au media gani ambayo inaweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi? Mitandaoni je kila mtu ana smartphone akaona mafundisho hayo? Acha mihemko ujiaji mwingi, acha watu wapate elimu hata kama ilitolewa itolewe zaidi, sijui kwanini ikuume hivi maana atangu jana umeshupalia kweli kweli
 
Jinsi uneployment inavyokuwa kwa kasi tatizo..

Watu lukuki watakosa ajira...
Hapa ndo kusema maajenti na wapiga debe nchi nzima kwisha habari yao!!! Mbona tunaboost unemployment badala ya kuidhibiti?

Kumbe yawezekana hata wale maadui watatu wa tangu uhuru (ujinga, maradhi na umaskini) tuliwabeba hivi hivi mpaka saivi bado tunahangaika nao eeh??
 
Moja ya sifa kubwa ya serikali ya Tanzania kufanya maamuzi kwa kushtukiza, bila kushirikisha wadau au kufanya pilot study. Na maamuzi yao siku zote yanakuwa ni amri zinazotolewa on short notice. Hili agizo halitekelezeki kirahisi na litaleta shida kubwa.
Tusubiri tuone tarehe 6 +
 
Wewe ndiyo mzito, umekomalia jambo jepesi kabisa, kwani watu na wadau wakipewa elimu wewe kinakuuma nini mzee, halafu hiyo elimu unayoisema ilitolewa ilitolewa kwenye platform gani au media gani ambayo inaweza kuwafikia watu wengi kwa urahisi? Mitandaoni je kila mtu ana smartphone akaona hilo tangazo? Acha mihemko ujiaji mwingi, acha watu wapate elimu hata kama ilitolewa itolewe zaidi, sijui kwanini ikuume hivi maana atangu jana umeshupalia kweli kweli
We ni zaidi ya mjinga!
Elimu elimu gani? Kwenda kukata ticket ubungo unataka upewe elimu gani?
Utaenda kama kawaida ubungo kukata ticket, ila badala ya kupewa ticket za kwenye kitabu, utapewa ticket kutoka kwenye mashine. Kama ilivyo kwa mwendokasi
 
Back
Top Bottom