Lawama zote za umeme ziwaendee Kitila Mkumbo na Nehemiah Mchechu

Ukiipata business model tu imekula kwako
 
Haaaa! ule ni mfumo mzima wa database ya shirika, si ya wale Mahindra lakini wali fail mapema sana ndiyo tunarudi pale pale hakuna usimamizi mzuri wa shamba la bibi Kwa maana kila mmoja akiona kuna upenyo anachota chake mapema.
TANESCO sehemu iko na wajinga wengi na ndiyo yenye staffs wengi ni distribution note me, Maharage aliwapa hela nyingi zaidi ya 3billion Kwa mikoa class A na 2 b Kwa mikoa mingine wafanye matengenezo yenye tija ahaaaa mtu mweusi akaonesha rangi yake Kwa kurudisha pesa mwisho wa mwaka wa bajeti tena karibu nusu, jamaa hapo ndipo alipoona kumbe humu Tanesco wajinga ni wengi sasa mwaka uliofuatia wa fedha akahamisha magori yote ofisini kwake ili ajipigie vizuri. Ukimpata Engineer wa Tanesco muulize yupo kitengo gani na yapi majukumu yake utakuja nipatia majibu hapa , kile ni kijiwe hakuna mgawanyo wA kazi hapo utategemea kupata matokeo chanya sahau. Ujawagusa hao mameneja wengi wao ni mzigo kama MD wao.
 
Mawazoduni ya mtu asiyeenda hatashule
 
Nimeshangaa siku hizi Mpaka watu wazima na wazee umeme ukirudishwa wanashangilia Kama yanga au simba amefunga goli !
 
Naona wahuni mnatafuta sababu ya kuiuza Tanesco kwa waarabu. Kwendeni zenu.
 
Mkuu, kua mali za umma haiondoi uhalisia wa gharama za umeme.
 
Acheni lawama, mama alishasema mwisho wa umeme kukatika ni mwezi wa tatu...waacheni TANESCO watekeleze majukumu yao halali
Hata wapewe miaka 20 hawatakuja na Suluhu yoyote..

Kwani haya matatizo ya umeme yameanza juzi wakati wa Samia Suluhu Hassan?

Yameanza seriously wakati wa Jakaya Kikwete pale ambapo watumiaji umeme walipoongezeka sana huku vyanzo vya umeme vikiwa vilevile..

Watu wakatumia fursa ya matatizo haya kufanya ufisadi badala ya tatizo hilo liwafanye watumie akili zao kwa kasi na ubora zaidi ili kuleta suluhu ya kudumu..

Since then (almost 30 yrs now) sababu zinazotolewa ni zilezile na ahadi ni zilezile lakini tatizo liko palepale..

Mzee baba, Hayati John P. Magufuli alijitajidi kidogo lakini amekufa na kufa na reforms zake. Waliokuja wanaendeleza tatizo tu na story zilezile za wakati wa Mkapa na Jakaya Kikwete zimerudi tena..

In my opinion, FaizaFoxy (mwana CCM huyu) ana hoja ya akili sana na inachohitaji ni kuongezewa nyama tu ktk kuiboresha. Na ofcoz hiyo ndiyo itakuwa suluhu ya kudumu Kwa ishu hii na zingine zote inazohusi maendeleo ya kijamii..

Kwa mfano, si tu Shirika hili livunjwe vunjwe na mamlaka ya usimamizi wa sekta ya nishati iwekwe kwenye mikoa na wilaya...

Hili la kuvunjwa vunjwa ni sawa kabisa.

Lakini kama mfumo wa utawala wa kuteua viongozi DSM au Dodoma na kuletwa na mtu mmoja aitwaye Rais kuja kutawala/kuongoza wananchi wa mikoa husika utaendelea, pendekezo la FaizaFoxy linaweza lisilete tija inayotarajiwa..

Tunataka watawala wa mikoa na wilaya wachaguliwe na wananchi wa mikoa na wilaya husika na wawajibike kwao katika mambo yote ya usimamizi wa utawala na maendeleo ya jamii ya mikoa husika..

Sambamba na hilo☝️☝️, lazima pia mifumo ya mamlaka ya usimamizi wa kifedha kuanzia vyanzo vya mapato (kodi), bajeti na ajira za wafanyakazi wote ziwe mikononi mwa mamlaka ya mikoa na wilaya husika na sio kama ilivyo sasa kwamba, kodi zote, ajira zote ni mpaka DSM au Dodoma iamue ndo baadae Rais (kwa sasa Samia) ndo aamue mikoani na wilayani tupeleke ngapi na amlete nani na kwa wakati gani ili awatawale wenyeji..

Kwa mfumo huu uliopo sasa ni ngumu sana kutoboa kimaendeleo kwa haraka kwa sabb una - encourage impunity na kutowajibika kwa viongozi..!

Suluhu ni kuwepo na mamlaka za serikali za mitaa zilizo huru na kamili kwelikweli na sio usanii huu uliopo sasa wa serikali za mitaa Kwa jina tu lakini maamuzi yote ya kiutawala na kifedha yanatoka DSM au Dodoma..
 
Mkuu, kua mali za umma haiondoi uhalisia wa gharama za umeme.
Motive ya shirika la umma na motive ya kampuni ya mtu binafsi [ private sector] ni tofauti. Shirika la umma linatakiwa lijiendeshe kiufanisi hivyo kutoa huduma kwa bei nafuu lakini bila hasara; unlike the private sector who are always driven by the maximization of profit!
 
Acheni lawama, mama alishasema mwisho wa umeme kukatika ni mwezi wa tatu...waacheni TANESCO watekeleze majukumu yao halali
Wametumwa hao ukweli wanajua kwanini wasisubili miezi 6 waliyopewa Tanesco ikaisha ndio waje na mapendekezo yao?
 
Sikubaliani na wewe.

Hilo unalotaka practically halitawezekana. Kuna mikoa haina vyanzo vya umeme. Yenyewe itaishia kununua kwenye mikoa yenye Ina vyanzo vya umeme. Gharama za umeme mikoa hiyo itakua juu kuliko ile yenye Ina vyanzo.

Hapo tayari ni udhaifu kwamba unagawa shirika lakini mmoja anapata na mwengine anakosa.
 

Kutukana hovyo hovyo kunaashiria mapungufu makubwa. Ukiwa na mapungifu mengi, hasa mapungufu ya utulivu wa akili na reasoning, unaishia kutukana hovyo hovyo ukiamini una-compensate vitu ulivyovikosa. Jambo ambalo siyo kweli.

Tuliza akili, argue professionally, sensibly and reasonably. Wengine watakuwa kwenye nafasi ya kujua nani ana ufahamu wa kutosha na nani anafanya argument based on ignorance.

Mleta mada ana hoja, japo siyo lazima kila mkoa kuwa na kampuni yake. Hoja ya msingi ni kwamba, TANESCO, kama yalivyo mashirika mengine yanayosimamiwa na serikali, has miserably failed. Tunahitaji sekta binafsi ipewe hili jukumu, huku tukijua kuwa ni vigumu sana kampuni moja kufanya majukumu yote yatakayosababisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa eneo lote la nchi. Hivyo ni vyema kuwa na makampuni binafsi zaidi ya moja. Lakini kutegemea Serikali hii ambayo uteuzi wa wa wakuu wa taasisi za serikali unaangalia zaidi ukada wa CCM kuliko maarifa, ni kusubiria embe chini ya mchongoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…