Lawama zote za umeme ziwaendee Kitila Mkumbo na Nehemiah Mchechu

Acheni lawama, mama alishasema mwisho wa umeme kukatika ni mwezi wa tatu...waacheni TANESCO watekeleze majukumu yao halali
Hii kauli ya "mwisho wa umeme kukatika ni ..... "
Isharudiwa mno.
Huwezi muamini muongo hata akisema ukweli.
 
Nioneshe nchi moja duniani yenye shirika moja tu la umeme linalofanya production mpaka distribution lililofanikiwa.

Huwa sikisii.
Mashirika ya umeme kwenye nchi zilizoendelea yapo mengi yana pishana size and strategies approaches.

Kwanza distribution ya umeme sehemu kubwa inamilikiwa na central government kama incentive.

Lakini kuna maeneo mengine kuna mashirika yana miliki production, supply and retail (kama TANESCO).

Hayo sio maamuzi ya ufanisi ni uwezo wa resources.

Sasa embu tueleze source za uwezo kila mkoa kuwa na uwezo wake wa umeme, distribution infrastructure and retail.

Unajiropokea tu
 
Umesahau kuna shirika la umeme la mkoa mmoja uliozungukwa na maji, ambalo halizalishi umeme wake na halilipi kwa shirika mama, kazi yake ni kuchukua mapato na kuyaweka kibindoni
 
Kigoma haikuwa imeunganishwa kwenye gridi ya taifa hadi September 2022.

Mlioko huko tuambieni hali ya upatikanaji wa majenereta umeme ilikuwaje.
Tatizo siyo kuunganishwa au kutokuunganisha kwenye gridi ya taifa. Gridi ya taifa hakuna zaidi ya switching tu, na hilo linaweza kufanyika hata kwa mashirika tofauti.

Chukulia mfano wa EU (nchi za muungano wa Ulayo) kila moja ina kampuni zake za ufuwaji wa umeme na ina grid yake na pia wana grid ya Ulaya nzima wanaiita {Synchronous Grid). na haijawa tatizo.

Ushauri wangu ni tanesco ibomolewe iwe kuna shirika la umeme kila mkoa, iwe la serikali au binafsi haijalishi. Bila hivyo hatuna ujanja zaidi, hatuwezi kwa sasa na hatutoweza kwa miaka 100 ijayo kuendesha mashirika ya umma makubwa, hususan ya huduma, kama lilivyofikia Tanesco.

Kumbuka, uchumi kila unavyokuwa na mahitaji ya umeme yanaongezeka. Tanesco kitaalam tunasema limesha "bust".
 
Naunga mkono hoja.

Lakini, WaTanganyika ndio wapewe kipaumbele ya kuunda hizo and I'll coin them, regional energy distriburtion (RedCo?)companies.

Vilevile Tanesco ibakie kama mzalishaji tu, wa maeneo yanayohitaji ulinzi wa Kitaifa, mfano JKNH power plant.

Kwa kweli huyu "elephant" anahitaji nyuki. Hatahivyo Faiza unasema tusi ilaumu Serikali wakati huo huo unahamisha goli na kuwalaumu watu serikalini. Nadhani ingekuwa fair zaidi kusema hao K. Mkumbo na N.Mchechu wachukue ushauri wako na wafanyie kazi.
 
It was evident kwamba Uko shallow kwenye reforms za mifumo Muhimu na mikubwa kama tanesco

Hakuna unachojua

The two unaowataja hawana hata mwaka kwenye ofisi and are also undergoing their own reforms

Regional tanesco is another stupidest idea

Najua umetumwa…. But sometimes sio kila parcel unabeba

It will take at least three years kuanza kuona changes za tanesco tena IKIWA attachwa afanye kazi bila interference
 
Mkumbo na Mchechu wameteuliwa na huko Tanesco kuna wateule pia. Tatizo mteuaji.
 
Wawe na mwaka au wawe na mwezi mmoja, jiulize wewe ambae upo "deep" waliwekwa kufanya kazi gani zaidi ya kuweka sawa mashirika ya umma yasiyotenda ipasavyo?

Nahitaji jiu ya hilo swali kutoka kwako uliye "deep".
 
Umesahau kuna shirika la umeme la mkoa mmoja uliozungukwa na maji, ambalo halizalishi umeme wake na halilipi kwa shirika mama, kazi yake ni kuchukua mapato na kuyaweka kibindoni
Siufahamu huo mkoa.
 
Naona unajichanganya tu, nisome tena, nasema kila mkoa uwe na shirika lake la umeme. Nini huo mkoa inafanya na umeme itaununua mkoa upi au itauuza mkoa upi itakuwa ni jukumu la huo mkoa.

Haihitaji rocket science kuelewa niliyoyaandika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…