FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
- Thread starter
- #41
Kitila Mkumbo na Nehemiah mchezhu ndiye wenye jukumu la mashirika ya umma kwa sasa.Wazo lako zuri sana lakini hao uliowagusa hawana cha kufanya na hata wakiwa nacho hakitoleta tija Kwa Tanesco hii unayoisikia chukua hii kitendo cha MANARA kupiga kelele kwenye social media dhidi ya umeme kimepelekea dada mwezio meneja wa mkoa wa Kinondoni kaskazini (MIKOCHENI) kutolewa kwenye nafasi hiyo je? hapa kuna watu makini wa kushughulika na masuala ya umeme wa uhakika au siasa zimewajaa vichwani mwao.
Kila mkoa upo na kiwango cha umeme kinapokea toka gridi ya Taifa ukiachana na Ile isiyokuwa ndani ya gridi(Mtwara, Lindi , KATAVI n.k) hawa wakipewa MW wazibadilishe kuwa pesa itakuwa kituko cha karne Kwa jinsi upotevu wa umeme ulivyokuwa mwingi kwenye njia za usambazaji Kwa uzembe wa watendaji haswa utawala Kwa ngazi zote,Tanesco haina tija ya kugaiwa Kwa mikoa hapa hapatikane Waziri mwenye elements za ukali na ufuatiliaji wa karibu Kwa shughuli zote za shirika ndani ya mwaka shirika litakuwa ruler lile.
Mwenyekiti wa CCM Taifa hamelikabidhi shirika Kwa watu si Sahihi ni mizigo tupu, hawana mipango ya dharura kulitoa katika kero za mgao sugu huu wa nusu mwaka sasa.
Manara si wa kwanza wala hatakuwa wa mwisho kulalamikia umeme Tanzania hii.
Ninachokishauri hapa ni utatuzi wa tatizo wa kudumu, siyo wa zima moto.
Hata ufukuze Tanesco nzima uiete mpya, yatakuwa yake yake. Shirika limekuwa kubwa kuliko uwezo wetu.
Ni lazima likatwe likatwe. Hakuna ujanja mwingine uliobakia amabo haujafanywa bado.