milele amina
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 6,045
- 8,080
Dr wake anawaonea huruma watanganyika.Mimi kwa kweli yule Biteko kwa macho tu huwa namuona kama ni mgonjwa hivi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dr wake anawaonea huruma watanganyika.Mimi kwa kweli yule Biteko kwa macho tu huwa namuona kama ni mgonjwa hivi.
MSIBA WA KWANZA MKUBWA kuwahi KUTOKEA kwenye WIZARA TANGU MAMA aingie MADARAKANI March 2021View attachment 3147717
Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango amefariki Dunia leo Novemba 9, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Rais Samia Suluhu Hassan ameandika katika Mitandao yake ya Kijamii kuhusu Kifo cha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango,
View attachment 3147755
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea leo tarehe 09 Novemba, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Ninatoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
Bw. Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali.
Mwenyezi Mungu aijalie familia yake subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho yake mahali pema."
Wasifu wa Mafuru
Lawrence Mafuru ni mtaalamu mashuhuri wa masuala ya fedha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika benki, uwekezaji, na sera za serikali. Ni Certified Chartered Banker kutoka Taasisi ya Wataalamu wa Benki ya London na pia ni Certified Financial Markets Dealer aliyeidhinishwa na ACI Financial Markets.
Alianza safari yake mwaka 1998 katika Benki ya Standard Chartered, akijikita katika Ufadhili wa Biashara za Kimataifa. Kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili iliyofuata, alishika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika sekta ya fedha nchini Tanzania, ikiwemo kuwa Mkuu wa Hazina katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, na Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA).
Uzoefu wake unaenda zaidi ya benki za biashara, kwani pia aliwahi kuhudumu kama Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha. Kama mamlaka inayotambulika katika masuala ya benki na fedha, Bw. Mafuru huombwa mara kwa mara kuwa mzungumzaji kwenye mijadala ya sekta hiyo. Ana shauku ya kutumia utaalamu wake ili kuleta manufaa kwa wateja na wadau wake.
Kabla ya nafasi yake ya sasa, Bw. Mafuru alichangia pakubwa katika kuunda sera za uchumi za Tanzania. Alihudumu katika Wizara ya Fedha kama Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na baadaye kama Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera za Usimamizi wa Uchumi.
Hadi kifo kinamkuta, Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru alikuwa akihudumu kama Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.
Wanawake wengi sana walimpenda Baltasary.Kumbe hata wewe unaangalia video za desh desh why zed.
Unaziangalia ukiwa umejifungia chumbani au sitting room. Ningetamani kuona uso wako ukiwa unazifaidi.
Salama Mkuu ,Bibi yetu Faiza naye yumo kwenye sector...😀😀😀Mkuu heshima yako.
Very stupid and insensitive commentMWAMBIA ASIMAMISHE KIFO CHAKE KAMA ALIVYOMSIMAMISHA LUHAGA MPINA KUHUDHURIA VIKAO VYA BUNGE.
Nyambafu sana.
Genta una taarifa nyingi za muhimu,inaonekana wewe Ni mtu mmoja well informed hapa Tanzania.Kaondolewa na Genge la Madaraka ya 2025 ambalo Mama kabaki nao kama Watatu Ndani na Nje wako kama 7 hivi.
Not fair kabisa, anaondoka Mafuru, Mwijaku au Juma Lokole wanabaki, kweli??View attachment 3147717
Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango amefariki Dunia leo Novemba 9, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Rais Samia Suluhu Hassan ameandika katika Mitandao yake ya Kijamii kuhusu Kifo cha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango,
View attachment 3147755
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea leo tarehe 09 Novemba, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Ninatoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
Bw. Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali.
Mwenyezi Mungu aijalie familia yake subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho yake mahali pema."
Wasifu wa Mafuru
Lawrence Mafuru ni mtaalamu mashuhuri wa masuala ya fedha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika benki, uwekezaji, na sera za serikali. Ni Certified Chartered Banker kutoka Taasisi ya Wataalamu wa Benki ya London na pia ni Certified Financial Markets Dealer aliyeidhinishwa na ACI Financial Markets.
Alianza safari yake mwaka 1998 katika Benki ya Standard Chartered, akijikita katika Ufadhili wa Biashara za Kimataifa. Kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili iliyofuata, alishika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika sekta ya fedha nchini Tanzania, ikiwemo kuwa Mkuu wa Hazina katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, na Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA).
Uzoefu wake unaenda zaidi ya benki za biashara, kwani pia aliwahi kuhudumu kama Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha. Kama mamlaka inayotambulika katika masuala ya benki na fedha, Bw. Mafuru huombwa mara kwa mara kuwa mzungumzaji kwenye mijadala ya sekta hiyo. Ana shauku ya kutumia utaalamu wake ili kuleta manufaa kwa wateja na wadau wake.
Kabla ya nafasi yake ya sasa, Bw. Mafuru alichangia pakubwa katika kuunda sera za uchumi za Tanzania. Alihudumu katika Wizara ya Fedha kama Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na baadaye kama Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera za Usimamizi wa Uchumi.
Hadi kifo kinamkuta, Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru alikuwa akihudumu kama Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.
Huyu kilichomuondoa wala siyo 🥁Ifike hatua mtu akifariki wawe wanaweka wazi Watu Tuogope kufanya Uovu, Kama mtu kafariki kwa Ukimwi isemwe kweli, kafatiki kwa pombe isemwe kweli, acheni kuwa mnasingizia mafua au kisukali wakti Mtu kafariki kwa Ukimwi.
R.I.P Grace Mapunda na Lawrence Mafutu💔💔
Kila mtu ameandikiwa siku yakeNot fair kabisa, anaondoka Mafuru, Mwijaku au Juma Lokole wanabaki, kweli??
HapanaKama wanavyosema ni kweli kuwa umeme umemuondoa, basi hata mwenza wale atakuwa ameathirika!
Hatuelewi, hii ni lugha gani?Inna li Llahi wa inna Ilayhi rajiun.
Kiswahili.Hatuelewi, hii ni lugha gani?
Kinaandikwa kwa lugha ya shetani toka lini?Kiswahili.
Mafuru sio binadamu hadi asiondoke? Basi ndo hivyo kaondoka.Not fair kabisa, anaondoka Mafuru, Mwijaku au Juma Lokole wanabaki, kweli??