The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Ndugu Laurence Mafuru Ambae amewahi kua mkurugenzi Mkuu wa NBC Bank na Msajili wa Hazina ameteuliwa kua kamishna wa Sera wizara ya fedha.
Hakuna mahala uteuzi huo umetangazwa ila nimebahatika kuona tangazo kutoka kwenye taasisi yake ya Bankable Institute kwamba amejiuzuru majukumu ya mshirika mtendaji (managing partner) kutokana na kuteuliwa kua kamishna wa sera wizara ya fedha.
Sina tatizo na uteuzi wa Mafuru, najua ni mtaalam mbobezi, mjuzi, ana uzoefu maarifa makubwa lakini swali langu ni kwa nini watu ni wale wale.
Kwamba nchi hii mtandao ni ule ule ndio unatakiwa kula keki ama neema ya nchi hii, watu wale wale. Nilishangaa juzi Balozi Batrida anateuliwa katibu tawala wa mkoa baadae mkuu wa mkoa, unajiuliza mtu amekua hadi balozi bado hawezi kuishi bila kuajiriwa?
Mafuru ana taasisi yake ya Bankable Institute, ambayo bado kama atahitajika kusaidia taifa basi ni rahisi kumpata ama kupata ushauri wake kupitia hiyo taasisi na akaendelea kuneemeka na mema ya nchi hii.
Sijawahi kusikia mtu kutoka taasisi ama sekta binafsi amepewa nafasi serikali akaikataa, sijawahi kusikia, simaanishi hawapo ila sijawahi kusikia.
Hii inatupatia picha kwamba kujiajiri bado ni changamoto ndio maana watu watazuga wamejiajiri ila ikitokea ofa za serikali hawawezi kuzikataa, kwa maana kwamba maisha ya utumishi serikalini ni mazuri na matamu kuliko kujiajiri.
Hii nchi ina watu milioni 60, kwa nini kila siku ni wale wale tu, wanatoka hapa wanaenda pale, wanatoka huku wanaenda kule.
CCM wametemgeneza mfumo wa hovyo sana wa nchi hii.