Tetesi: Lazaro Nyalandu aiacha CCM kimya kimya

Mtu yeyote akijitambua CCM wanamwona hawafai
Nyalandu umechagua fungu lililo Bora
Wana singida kaskazini sasa watakuona mtu wa maana ..
Ni bora kusimama na ndugu yako.Mnyaturu Mwenzako LISSU..Ni kaka yako wa damu huyo.Kuliko kuandamana na miskuma ya huko wai sijui isiyo na utu
Pumbavu zako, usitukane kabila lisilo lako, natamani nikutukane na wewe bahati mbaya sitaki kuwaumiza wengine.
 
Lazaro Nyarandu mbunge wa Singida Kwa tiketi ya CCM, ameiacha CCM kimya kimya na kinachosubiriwa ni kutangaza rasmi kuhamia Chadema, imebainika.

Taarifa toka Singida na Jimboni kwake zinabainisha kwamba mbunge huyo amesitisha kabisa kushiriki vikao vya CCM na kujihusisha na masuala yote ya kichama na badala yake yuko bize Kwenda Nairobi kufanya mazungumzo na Viongozi wa upinzani.

Taarifa za uhakika toka Singida zinamtaja Mbunge huyo kusitisha mahusiano na chama chake na hahudhurii vikao muhimu ndani ya wilaya yake hasa vikao vya kamati ya siasa ya wilaya Kwa muda wa miaka 2 sasa hajahudhuria kikao cha kamati ya siasa na Halmashauri kuu ya CCM wilaya. Vikao hivi ni muhimu sana katika kutoa dira ya uongozi wa kisiasa na masuala ya Maendeleo.

Mfano katika uchaguzi Mkuu wa CCM 2017 ngazi ya wilaya. Nyarandu anatajwa kugoma kutoa ushirikiano Kwa CCM Singida kaskazini katika mchakato wa uchaguzi ndani ya eneo lake la wilaya. Haikuishia hapo, wakati CCM Singida kaskazini Wameitisha Mkutano mkuu wa CCM wilaya Kwa ajili ya kuwachagua Viongozi wa wilaya mnamo October 5,2017 Mbunge huyo hakuhudhuria Mkutano huo muhimu ndani ya wilaya yake na badala yake alionekana Mkoani Mwanza Kwenye makongamano ya kidini akihubiri madhabahuni. Kitendo chá Mbunge kukataa kuhudhuria Mkutano wa uchaguzi muhimu ndani ya wilaya yake kinathibitisha ukweli kwamba kiongozi huyo ameitoa CCM ndani ya moyo wake.

Katika uchaguzi Mkuu wa CCM Singida kaskazini maswahiba wa karibu sana wa Nyarandu wanatajwa kupigwa chini na kupoteza nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho, akiwemo mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo ambae ndiyo pumzi ya Nyarandu Kwa zaidi ya miaka 20, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambae ni swahiba mkubwa wa Nyarandu amepoteza uongozi ndani ya chama hicho kupitia uchaguzi wa mwaka huu.

Ndani ya Mkutano mkuu wa CCM Singida kaskazini inatajwa wana CCM walikuwa wakipashana Habari kuhusu mbunge wao Kuwa na mpango Kwenda upinzani ndiyo maana amekataa kuhudhuria Mkutano huo muhimu ndani ya wilaya yake. Watu wake wa karibu waliogombea walisulubiwa Kwenye kura kutokana na Matendo ya mbunge huyo kutowajibika Kwa wananchi na Mienendo yake isiyoeleweka.

Watu wake wa karibu waliogombea na kushindwa Kwenye uchaguzi wamenukuliwa wakisema watahamia upinzani Kwa muda mwafaka. Kauli hizi Kwa watu wa karibu mno na mbunge huyo zinaleta picha kamili wanachopanga na watu wake, Kinachoendelea Kwa sasa ni kukamilisha mipango hiyo hatua Kwa hatua. Matendo ya Kiongozi huyo Kwa sasa yanaashiria uhalisia huo.

Jambo muhimu ambalo wengi hawajui ni kwamba Nyarandu ni mtiifu Kwa Edward Lowassa Kwa muda mrefu sana na ni mtu wake wa karibu, hapo katikati uhusiano wao Ulikuwa Kwa usiri hasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo Lazaro naye alikuwa ni mgombea urais kupitia CCM. Uhusiano wake na Lowassa Kwa sasa umeimarika maradufu na wamekutana mara kadhaa Kwenye moja ya hotel mkoani Arusha ( nitaleta uzi Maalum na evidence)

Itaendelea.............
ashajua hana chake CCM,,mafisadi wote waTAKIMBILIA KWA BOSS WAO EDO
 
Upuuzi tu kwani lazima ahuzulie kikao au akuhuzulia unamlipa pambana na hali yako nyarandu sio level zako
Muulize kikao cha Juzi ikulu katibu mkuu wao alikuwepo? kama mtu kama katibu mkuu anakosekana na kikao kinaenda itakuja kuwa nyalandu kukosekana huko wilayani? Wapuuzi tu hawa
 
Chadema hawajawahi kuacha siasa za ukabila hiyo ipo kwenye damu na kwa hiyo laana ya ukabila na udini hawatakaa washike dola asilani
Hata wewe mkuu unawaza hivi...pole sana mkuu..usiwaze sana...moyo utapasuka
 
kisa kaenda kumsalimia lissu misukule mingine inaogopa itapigwa bun aya fukueni makaburi tuone
 
Lazaro Nyarandu mbunge wa Singida Kwa tiketi ya CCM, ameiacha CCM kimya kimya na kinachosubiriwa ni kutangaza rasmi kuhamia Chadema, imebainika.

Taarifa toka Singida na Jimboni kwake zinabainisha kwamba mbunge huyo amesitisha kabisa kushiriki vikao vya CCM na kujihusisha na masuala yote ya kichama na badala yake yuko bize Kwenda Nairobi kufanya mazungumzo na Viongozi wa upinzani.

Taarifa za uhakika toka Singida zinamtaja Mbunge huyo kusitisha mahusiano na chama chake na hahudhurii vikao muhimu ndani ya wilaya yake hasa vikao vya kamati ya siasa ya wilaya Kwa muda wa miaka 2 sasa hajahudhuria kikao cha kamati ya siasa na Halmashauri kuu ya CCM wilaya. Vikao hivi ni muhimu sana katika kutoa dira ya uongozi wa kisiasa na masuala ya Maendeleo.

Mfano katika uchaguzi Mkuu wa CCM 2017 ngazi ya wilaya. Nyarandu anatajwa kugoma kutoa ushirikiano Kwa CCM Singida kaskazini katika mchakato wa uchaguzi ndani ya eneo lake la wilaya. Haikuishia hapo, wakati CCM Singida kaskazini Wameitisha Mkutano mkuu wa CCM wilaya Kwa ajili ya kuwachagua Viongozi wa wilaya mnamo October 5,2017 Mbunge huyo hakuhudhuria Mkutano huo muhimu ndani ya wilaya yake na badala yake alionekana Mkoani Mwanza Kwenye makongamano ya kidini akihubiri madhabahuni. Kitendo chá Mbunge kukataa kuhudhuria Mkutano wa uchaguzi muhimu ndani ya wilaya yake kinathibitisha ukweli kwamba kiongozi huyo ameitoa CCM ndani ya moyo wake.

Katika uchaguzi Mkuu wa CCM Singida kaskazini maswahiba wa karibu sana wa Nyarandu wanatajwa kupigwa chini na kupoteza nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho, akiwemo mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo ambae ndiyo pumzi ya Nyarandu Kwa zaidi ya miaka 20, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambae ni swahiba mkubwa wa Nyarandu amepoteza uongozi ndani ya chama hicho kupitia uchaguzi wa mwaka huu.

Ndani ya Mkutano mkuu wa CCM Singida kaskazini inatajwa wana CCM walikuwa wakipashana Habari kuhusu mbunge wao Kuwa na mpango Kwenda upinzani ndiyo maana amekataa kuhudhuria Mkutano huo muhimu ndani ya wilaya yake. Watu wake wa karibu waliogombea walisulubiwa Kwenye kura kutokana na Matendo ya mbunge huyo kutowajibika Kwa wananchi na Mienendo yake isiyoeleweka.

Watu wake wa karibu waliogombea na kushindwa Kwenye uchaguzi wamenukuliwa wakisema watahamia upinzani Kwa muda mwafaka. Kauli hizi Kwa watu wa karibu mno na mbunge huyo zinaleta picha kamili wanachopanga na watu wake, Kinachoendelea Kwa sasa ni kukamilisha mipango hiyo hatua Kwa hatua. Matendo ya Kiongozi huyo Kwa sasa yanaashiria uhalisia huo.

Jambo muhimu ambalo wengi hawajui ni kwamba Nyarandu ni mtiifu Kwa Edward Lowassa Kwa muda mrefu sana na ni mtu wake wa karibu, hapo katikati uhusiano wao Ulikuwa Kwa usiri hasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo Lazaro naye alikuwa ni mgombea urais kupitia CCM. Uhusiano wake na Lowassa Kwa sasa umeimarika maradufu na wamekutana mara kadhaa Kwenye moja ya hotel mkoani Arusha ( nitaleta uzi Maalum na evidence)

Itaendelea.............
Anajua kinachofuata
 
Hata Nape mlisema atahama CCM juzi alipoenda Kenya na kuhojiwa KTN mkabaki mnasema hajajitambua wakati ni nyie mlimwita kamanda anasubiri kuhama tuu.
 
Kingu na Mwigulu ni Wanyiramba
Nyalandu na Lissu ni Wanyaturu
Wanyiramba huwa wanasifika kwa roho mbaya
Kwa hapa namuona Lazaro akisimama na ndugu yake Lissu..Mnyaturu Mwenzake
Ukabila tu umekujaa
Nitafurahi sana Nyalandu akituachia chama chetu
 
Hii habari haina mashiko, imekaa kimajungu kwa lengo la kumchafua Mh. Nyalandu
 
Kila mwenye kusoma sasa sio wakati wa kubaki ccm. Wamechoka tumewachoka....akitoka huko atakuwa amefanya jambo la maana kwa nchi yake.
Wengine nao watoke tu....tunahitaji mabadiliko ya kweli sio ya 50/50
 
Kwa hiyo ulitaka asije Mwanza, tulikuwa naye Mwanza na aliongea na Vijana wa kanisa la M.I.C.C, nyegezi kona na watu tulifurahia kuwa naye na alitujenga sana Vijana hasa alivyoelezea maisha yake ya utoto hadi hivi sasa...
 
Mtu yeyote akijitambua CCM wanamwona hawafai
Nyalandu umechagua fungu lililo Bora
Wana singida kaskazini sasa watakuona mtu wa maana ..
Ni bora kusimama na ndugu yako.Mnyaturu Mwenzako LISSU..Ni kaka yako wa damu huyo.Kuliko kuandamana na miskuma ya huko wai sijui isiyo na utu
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukabila tu umekujaa
Nitafurahi sana Nyalandu akituachia chama chetu
unaongelea theory.sisi tuko huku mikoani tunajua.tunaona.
Chama chenu..hahahahahah..wewe kama nani?
watu wengine bana
 
Hata hivyo kuwa mwanaccm unahitaji uwe na akili za kimisukule.
 
Angekuwa mzalendo na skafu yake shingoni angekuwa ameshawakamata waliomshambulia Lissu kwa risasi. Wanafiki safari yao huwa fupi sana lazima wajikwae kama wafungao goli la mkono
Kama naona Kingu yuko nyuma ya propaganda hii! nadhani anatafuta umaarufu wa kimkoa kumzidi yule mwenye skafu shingoni anaejifanya mzalendo zaidi..kumbe hewa tu!
 
Back
Top Bottom