Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Lazaro Nyalandu arudi rasmi Chama cha Mapinduzi akitokea CHADEMA

Ukiwafuatilia sana wanasiasa unaweza kufa mapema sana kwa ugonjwa wa moyo.

Alichofanya Nyalandu ni katika kile kinachoitwa "kujitafutia mkate wake wa kila siku". Kila mtu ana mbinu zake na ni busara kutopangiana mbinu za kusurvive hapa duniani.

Muda si mrefu vyama karibia vyote vitapiga u-turn, vitaanza kumsifia Mama na kuunga mkono juhudi huku tukisahau kwamba mifumo hasa ya uchaguzi bado ni ileile na hatupaswi kubank hopes zote kwa mtu mmoja
Uwiiii [emoji1][emoji1] hapo dj na team yake wameshaanza kuunga
 
Nakumbuka uzi kuna mtu alianzisha kuuliza mbona katika kashi kashi zinazowakumba chadema Nyalandu hua hayumo?
 
Hawa watu tumeshasema sana kuwa wanafuata upepo tu..ipo siku tena atarudi sisiemu. .
 
Ukweli kabisa...! Chadema inakazi Sana kujijenga!!

Nnachoamini, Bado tena kuna kundi litakaloondoka huko, ndilo litakalowakatisha tamaa hata viongozi watakao kuwa wamebakia huko chamani

Hayo yoote ni Kwa sababu pia, kuna mambo ambayo viongozi wengi wa siasa huyafanya huku wakidhani ndiyo yenye kukiimarisha Chama na kukieneza, kumbe wasijue kwamba ni kukaribisha laana Kwenye Chama

Ubora wa myenendo Yetu hauishii tu tunapokuwa makanisani na miskitini, hapana, ubora huohuo unapaswa ufike Hadi Kwenye Vyama vyetu, kutendeana wema, kusameheana na kujizuia Sana kuwa sehemu ya wasababisha maafa Kwa wengine, na Jambo hili haliishii tu chadema Bali Kwa Vyama Vyote!!

Kuonea watu, kutafuta njia ya kuingiza nchi Kwenye maandamano yenye lengo la kuuwana, Kwa sababu tu mtu anataka madaraka, Haiwezi kukubalika Kwa Taifa la waombaji na Taifa linaloamini katika Mungu

Tanzania ni salama zaidi katika Mungu, wowote wenye lengo Baya kutaka kuhatarisha umoja na Amani Yetu, Sina hakika kama watabaki salama Mbele ya wanaokesha wakiliombea Taifa Lao,

Haiwezekani mtu umekunywa gongo huko uanguke halafu useme ulivamiwa na usalama wa Taifa, huko ni kuwachonganisha wananchi na serikali Yao, ni vyema matendo yenye kuashilia machafuko, ni vyema viongozi wetu wakaachana Nayo, la sivyo, Vyama wanavyoviongoza havitakaa kutulia Hadi watubu

Najua wenzangu hasa wapinzani mtachukizwa Sana na hichi, lkin huo ndio ukweli, ukitaka kufanya siasa za uchonganishi, Hama Tanzania,

Tutakapokubaliana kwamba Tz ni nchi ya watu wastarabu, ndipo tutaanza kufanya siasa za kistarabu
Umeandika hoja yako kishabiki Sana....ila NI mawazo yako,ngoja NIYAHESHIMU
 
Back
Top Bottom