Lazaro Nyalandu, Mwanaccm pekee aliyepinga Udikteta wa awamu ya 5 kwa vitendo

Tutamfikia kila Mhusika
Muda hautoshi !
Tulijaribu kushauri humu kuhusu kuwasamehe Covid 19 ili muda usipotee bure !
Tulijua ile habari ilikuwa ni kupoteza muda tu maana wale watakuwepo tu Bungeni mpaka 2025 !
Kumjadili Jiwe pia ni kupoteza muda tu maana yule jamaa alishajaa kwenye mioyo ya wanyonge wa Nchi hii !!
Hivyo kuwabadili watu eti wamchukie hiyo ni ndoto !

Jiwe is no more he has gone forever !
Let him rest where he belongs to !
 
Mamluki wa Jiwe akiwemo Hamis Kigwangwala alitangaza bungeni kwamba atamshitaki Nyalandu Mahakamani kama sehemu ya vitisho vya kumshughulikia , Lakini hadi Kigwangwala anazeeka hakuwahi kwenda hata kwa mjumbe wa nyumba 10 kumshitaki Nyalandu
Hajawahi kuwa na akili
 
Chadema tunawauliza, mkipewa nchi mtaendesha km Kikwete? au Samia? ama Magufuli? Mkapa au Nyerere?

Maana hamueleweki mnataka nini?
Mi siipendi Ccm ila nilimkubali Magufuli.
Hii nchi bila ubabe haiendi
 
Wakati wa Harakati za Makaburu kuna Wapambanaji wa aina mbili

Wapo kina Thabo Mbeki waliokimbia Nchi kupinga ukaburu na wapo waliobaki ndani ya South Africa kama kina Winny Mandela kuumaliza Ukaburu

vivyo hivyo 2015-2021
 
..Na Lowassa na Sumaye waliokuwa upinzani walipobinywa walirudi Ccm kulikokuwa na kinga.

..Kwa taarifa yako, Twiga walitoroshwa wakati Waziri wa Maliasili akiwa Ezekiel Maige.
Sumaye alisema walikuja Chadema Ili kuuwa Upinzani na walifanikiwa kwake sababu 2015 Ndio ulikuwa mwaka wa Chadema kutwaa Dola
 
Kijujuu uaadhani kuwa hoja kuwa Nyalandu ni mzalendo ina mashiko yoyote. Hata tone. Nyallandu wakati wa Kikwete likuwa anawaleta maseneta kutoka Marekani na kuwapeleka Ikulu kwa Rais. akitoka huko wana kwenda kwenye mbuga na mali asili nyingine na kubeba wanachotaka. Ilifikia wakakaribia kumilikishwa kitalu kwenye mbuga za wanyama bahati nzuri mbunge wa CHADEMA nadhani Sugu au Mchungali Mwesigwa wakailipuwa bungeni na mpango ukafa moja kwa moja. Sasa alipoingia Magufuli Nyalandu akiwa mbunge vilevile akawaita maseneta wake ila alipotaka kuwaeleka Ikulu akaelezwa awapeleke kwa waziri wa maliasili. Hiyo ilimuuma sana kwa sababu wale maseneta walishaaminishwa kuwa Nyalandu ni kila kitu sasa ikaonekana sio chochote. Akawa frustrated sana. Wakati huo huo Lowasa alijiamini yeye alikinunua CHADEMA kama mali yake na angekifanyia transformation. Baada ya Masha kuondoka CDM ambaye Lowasa alitarajia amfanye mwenyekiti wa CDM basi Lowasa akamshawishi Nyalandu ahamie CDM ili aje kuwa mwenyekiti. Ilipoonekana wazi kuwa CDM hakijauzwa na kuwa Lowasa hakuwa na uwezo a ku-influence uongozi wake hapo wote wakabaki njiapanda. Sasa hapo uzalendo wa Nyalandu uko wapi?
 
Aliwahi kudhtakiwa na huyo mliyemwita Mzalendo?

Kama sivyo ccm wote ni kapu moja...ila Nyarandu aliukataa udikiteta kwa kumanisha
 
Hakupinga udikiteta, aliogopa kubanwa kuhusu twiga waliosafirishwa wakati akiwa Waziri wa Maliasili akakimbilia kwenye kinga ya upinzani.
Nyalandu humjui... Huyo mtu anajiamini, sio chawa, sio dhaifu. Kama kweli alifanya hayo mbona jiwe halikumpandisha kotini??? Nyalandu ni mwanaume na nusu wewe.... Jiwe mwenyewe alimpigia salute. Nyalandu Hana makelele lakini nakwambia he is a man and a half, na haiitaji kuwa kiongozi Ili awndeshe maisha yake na ndo MAANA alijivua wadhifa zake zote kupinga alichoamini hakipo sawa... Halafu kichwani yupo vizuri yule... Elimu yake sio ya kukariri
 
Hawa ndiyo wanaume... Bila kumsahau Bernard Membe.. Jiwe huko aliko kuni ziendelee kuchochelewa kwa kasi
 
Duuuh chongo kuitwa kengeza ndio hii haya ile listi ya mwembe fisadi no 1 alikua nani?

..sio wote waliounga mkono upinzani walifurahishwa na maamuzi ya kumteua Lowassa kuwa mgombea wa Chadema.

..pia ni ukweli ulio wazi kwamba wapinzani nchi hii wananyanyaswa na kupitia misukosuko, wakati ndugu zao walioko Ccm wakitetewa na kulindwa na dola.

..sio sahihi kumbebesha Lazaro Nyalandu lawama za kutoroshwa kwa wanyama kupelekwa Uarabuni wakati inajulikana kwamba yeye hakuwa Waziri wa Maliasili wakati hayo yanatokea.

..Mh.Ezekiel Maige ndiye anayestahili lawama kwasababu alikuwa Waziri mwenye dhamana na Maliasili. Lakini nadhani na yeye anadai " dili " la kutorosha wanyama halikuwa la kwake.
 
ilikua bado kidogo kidogo apeperushe bendera ya cdm 2020, nadhani cdm kuna la kutafakari hapa
 
Aliyesema nyalandu ni fisadi anauza wanyama na kugawa vitalu maneno hayo yalitoka kwenye jukwaa la chadema na viongozi wake kwa style ile ile ya lowassa sisi wananchi huwa tunawaamini sana viongozi wa chadema wakituambia jambo vipi leo hii utubadilishie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…