Le Mutuz: Hayati Magufuli alikuwa rafiki yangu binafsi

Le Mutuz: Hayati Magufuli alikuwa rafiki yangu binafsi

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Siku moja nipo Mikocheni nikapigiwa simu na mtu mmoja anaongea kigogo, akaniambia sogea pembeni hapo kuna kelele, akaniuliza unajua unaongea na nani, nikasema mpaka hapa nishaelewa wewe ni Rais Magufuli, akaniambia uko wapi nikamwambia Mikocheni akasema kaa hapo hapo namwagiza mtu aje akuchukue,mara paa huyu hapa Magufuli,tukaongea pale kama masaa mawili,hadi mwisho nikaelewa nia njema aliyokuwa nayo Rais Magufuli kwa Watanzania,hakuwa na nia ya kuiba, mwisho, akanipa zake zote za simu za binafsi na za msaidizi wake, akaniambia hata saa nane usiku nipigie ukinikosa piga namba ya msaidizi wangu.

Siku moja niliandika makala moja nzito kupinga kikokotoo kipya, ikamfikia akaisoma akanipigia simu, nikaenda kumuona, nikamwambia Mzee wasaidizi wako wamekudanganya kwenye suala hili la kikokotoo kipya,kwa maana wastaafu tegemeo lao lipo kwenye mafao sasa yanapochezewa wanakuwa hawana pa kwenda, wasaidizi wako wanakufanya ugombane na Wananchi wako ambao daima wana imani na wewe,kwa hakika alinisikiliza na akakifuta kikokotoo kipya, nilifundishwa na Baba yangu, kiongozi anapokosea basi tafuta maneno ya busara kumweleza ikiwamo kumwambia wasaidizi wako wamekudanganya,hata unajua kabisa hili suala ni yeye kakosea.

Nilipokuwa naumwa nilimwambia akanisaidia, nilipelekwa hospital ya Jakaya, Mama yake Rais Magufuli alikuwa amelazwa pale akahamishiwa Chato, Magufuli akawaambia madaktari wanipe mimi ile suit aliyokuwa anakaa Mama yake Magufuli pale hospital ya Jakaya, nilikaa miezi miwili baadae Magufuli na rafiki yangu mmoja mfanyabiashara walinisaidia kwenda Afrika kusini kwa matibabu zaidi, nilipopata nafuu nikarudi bongo, tarehe 22 February 2021 nilikutana na Rais Magufuli uso kwa uso nikamwambia nataka kwenda India kwa matibabu, akanipa kiasi fulani cha pesa akaniambia nikifika India kama hela haijatosha nimpigie simu, kwa hakika Magufuli aliokoa maisha yangu, namshukuru sana.

Tarehe niliyosikia amekufa, it was my difficult day, mpaka leo siamini kama Magufuli amekufa, kuna watu wawili Mzee Mengi na Magufuli, siamini kama kweli wamekufa, sijawahi kwenda kwenye makaburi yao kwa sababu naogopa nikienda kwenye makaburi yao nitaamini kweli wamekufa, Magufuli alikuwa na nia njema kwa Watanzania,ndio kuna sehemu alicheza faulo lakini kwa maslahi ya Wananchi na Watanzania kwa ujumla,tunapotaka kumuhukumu mtu,tuangalie kwanza nia yake na dhamira yake, seriously , Magufuli hakuwa na nia ya kuiba katika kila jambo alilofanya, I live my American spirit, hii ni interview yangu ya kwanza baada ya miaka mitatu niliyokuwa nimepumzika.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078853

-Bachelor of Business Administration in International Business

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the effect of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Siku moja nipo Mikocheni nikapigiwa simu na mtu mmoja anaongea kigogo, akaniambia sogea pembeni hapo kuna kelele,akaniuliza unajua unaongea na nani,nikasema mpaka hapa nishaelewa wewe ni Rais Magufuli,akaniambia uko wapi .
Tatizo la Lemutuz ni kamba hujui lipi la kweli na lipi ni uzushi. Inshort ukweli na uongo wa Lemutuz viko between the lines.
 
Nilipokuwa naumwa nilimwambia akanisaidia, nilipelekwa hospital ya Jakaya, Mama yake Rais Magufuli alikuwa amelazwa pale akahamishiwa Chato, Magufuli akawaambia madaktari wanipe mimi ile suit aliyokuwa anakaa Mama yake Magufuli pale hospital ya Jakaya,
Akamhamisha mama yake ili wewe ulale humo ina maana hospitali nzima ina suit moja tu.
 
akaniambia sogea pembeni hapo kuna kelele, akaniuliza unajua unaongea na nani, nikasema mpaka hapa nishaelewa wewe ni Rais Magufuli, akaniambia uko wapi nikamwambia Mikocheni akasema kaa hapo hapo namwagiza mtu aje akuchukue,mara paa huyu hapa Magufuli,tukaongea pale kama masaa mawili,
😂
🤣
 
Mi naamini maana magufuli alikuwa mtu wa busy for nothing! Alilala usiku wa manane kwaajili ya petty issues kama kusoma faragha za watu, umbea na uchimvi.

Alikua na muda mwingi wa kuchezea.
Wewe acha kujifanya huna mcho.Miradi yote hiyo inayomaliziwa sasa hivi bado unasema hakulala for nothinng?

Hakujawahi kuwa na crisis ya maji wala umeme kwa kiasi hiki.

Mawaziri wote wanakili kupigiwa simu usiku ili kutatua kero za wananchi.
 
Mi naamini maana magufuli alikuwa mtu wa busy for nothing! Alilala usiku wa manane kwaajili ya petty issues kama kusoma faragha za watu, umbea na uchimvi.

Alikua na muda mwingi wa kuchezea.
Navyosema"sisi tutaamini vipi" , wewe hapo sikuhesabii maana najua akili hauna
 
Wewe acha kujifanya huna mcho.Miradi yote hiyo inayomaliziwa sasa hivi bado unasema hakulala for nothinng?

Hakujawahi kuwa na crisis ya maji wala umeme kwa kiasi hiki.

Mawaziri wote wanakili kupigiwa simu usiku ili kutatua kero za wananchi.
Uko brainwashed we kima! Miradi ilikuwepo nchi kabla na baada ya ukoloni!!
 
Uko brainwashed we kima! Miradi ilikuwepo nchi kabla na baada ya ukoloni!!
Wewe unachuki binafsi tu.

Miradi kama ya SGR ilikuwepo wakati wa ukoloni?

Waache wenzako walale sasa huku tukikosa huduma mhimu kila kona.
 
Back
Top Bottom