Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Atakayetoka nje ya mada na kutaja mambo ya kilimo cha Bamia... mod piga Ban haraka. Manake hamchelewi humu!
Unatoka ubaharia unaishia Mount Vernon na unaendesha malori sijui ya taka? Kulikoni halafu unaachika na mke anachukuliwa na mkurya sasa yupo Pelham kwenye appartments za watu wenye uhitaji mbona huendi kusaidia wanao wapate hata nyumba New Rochelle ?
 
PART 6.jpg


PART 6:- "MY AMERICAN EXPERIENCE" ...

Ndani ya Basi la Greyhound kutoka Ottawa/Canada tunaelekea New York City/USA nilikuwa ninawaza nitakapofika New York City itakuwaje? Simjui mtu so sitakuwa na mahali pa kulala JE ITAKUWAJE? but nikajikumbusha jinsi nilivyokwenda Belgium mara ya kwanza Miaka 5 nyuma so ghafla tukafika Border kama kawaida ya Uhamiaji ya USA wakishaona Passport yako inaonyesha uliwahi kuingia USA na kutoka huwa hawana tatizo na wakati huu Rais wa USA alikuwa ni President Ronald Reagan baada ya kugongewa mhuri wa kuingia nikalala usingizi mpaka Saa Nne Usiku tulikuwa tayari tupo Port Authority, West Manhattan New York City/USA mtaa wa West 42ND Street ambapo ndio mwisho wa Mabasi yote ya Mikoani yanayoingia New York City....

Kuna Mbongo mshikaji wangu nilikuwa na namba yake ya simu aliahidi kuja kunipokea lakini dakika ya mwisho HAKUJA nikashuka na begi langu dogo la nguo kama kawa nikakuta Ma Homeless kibao wanajitayarisha kulala so nikatafuta mahali saafi nikatoa Blanketi langu cause ilikuwa ni Winter time January so kulala ni kwenye masofa ya Abiria wanaposubiria mabasi ya Usiku na Asubuhi so na mimi nikawa kama Abiria ninayesubiri Basi ilinichukua miezi 3 ya Beach life kama tunavyoita kwenye Ubaharia ...

Mwishoni tu mwa wiki ya kwanza nikawa nimepata kazi Dukani as a "STOCK PERSON" kwa Mshahara wa USD $ 5 kwa saa so kwa masaa 40 kwa Wiki nilikuwa ninalipwa USD $ 200 per Week so nikaamua kukusanya pesa kwanza kwa kuendelea kukaa bure pale Stendi ya Basi ...nikiwa kazini Dukani I was charming Kiingereza cha Kimarekani ni tofauti na cha Dunia nzima so to Americans I mean wateja wa Duka nilikuwa bonge la kichekesho na English yangu ya Europe sikuwa muoga kuongea huku nikiendelea kua kichekesho kwa Wateja hasa Wakina Mama pole pole nikaanza urafiki na Wasichana Wakizungu na Weusi cause Duka nililokuwa nafanya kazi lilikua linauza Vifaa vya Nyumbani sana ambavyo Wanawake ndio wateja wakubwa nikaishia kuwa rafiki na Mama mmoja Mzungu aliyeishia kunipeleka kwa mtoto wake aliyekua bosi wa Kiwanda cha Vifaa vya Umeme akanipatia kazi iliyoanza kunilipa USD 10 kwa Saa Moja ...ITAENDELEA!
 
PART 7.jpg


PART 7: "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Baada ya kuanza kazi ya mshahara wa Dola 10 kwa saa sasa nikawa napata Dola 400 kwa Wiki pia nikatafuta kazi ya Usiku kuanzia Saa Sita Usiku mpaka asubuhi Kituo cha Petrol mtaa wa Stanford Boulevard Mt. Vernon baadaye nikaacha nikawa nakaanga kuku KFC Usiku so kwa kazi zote mbili nilikuwa ninapata Dola 550 kwa Wiki ndio nikatafuta Studio ya Dola 100 kwa Wiki nikahamia kwangu sasa kwa mara ya kwanza after 3 Months za kuhangaika na pa kuishi in US maisha yanaenda fasta sana Unafanya kazi mahali Wiki moja then unahamia pengine hivyooo...

Now kazi nilizokuwa ninafanya hazikuhitaji Viza wala Papers cause zilikuwa ni kazi za Wafanya Biashara wanaokwepa kulipa Kodi guys haya mambo ya kukwepa Kodi hata Majuu yapo kwa hiyo walikuwa wananiajiri "Chini ya Meza" kule wanaita "UNDER THE TABLE" yaani unaajiriwa tu kishikaji shikaji ...nikaamua kutafuta kazi ya kunilipa vizuri kusudi nisome Shule always akili na mawazo yangu ndoto zangu zilikiwa ni EDUCATION kwanza cause nilifikiria sana kua nisiposoma nikiwa mdogo sitasoma tena na nilikuwa ninajua kua ndugu zangu wa Mama wa Kambo walikuwa wanasoma wakisukumwa sana na Mama yao aliyekua akitumia all influences za Nafasi ya kazi ya Baba yangu kuhakikisha wanasoma nilikuwa ninajiuliza nisiposoma nitakuwa mgeni wa nani one day? ..

Mungu alinipatia bahati kubwa sana in my life mpaka leo Sijawahi kunywa Pombe wala Kuvuta Sigara so pesa zangu zote nilikua naingiza Benki tu baada ya kulipia kodi ya Chumba cause now nilikua na uhakika wa Dola 2,000 kwa Mwezi Chumba Dola 400 zingine 600 mambo yote mengine na 1000 Benki but likaja tatizo la ID Card huwezi kuishi USA bila kuwa nayo nikajaribu kutafuta New York City ikawa taabu kidogo kuna rafiki yangu Baharia Alex alikuwa anaishi Boston/Massachusets State akaniambia niende kule ni rahisi kupata so nikaomba likizo ya Wiki kazini nikaenda Boston na kupata ID Card I was happy cause now kwa mara ya kwanza I was in the American System maana ID Card inaenda kwenye Databese ya System ya Taifa ..so nikarudi New York City nikaibadili na kuwa ya New York then nikaomba Social Security Card nikapata sasa nikaanza mbio za kusaka Leseni ya kuendesha Gari! ...ITAENDELEA!
 
PART 8.jpg


PART 8: - "MY AMERICAN EXPERIENCE" ..

Baada ya kupata leseni ya Gari ya kawaida nikaamua kuanza kutafuta leseni kubwa ya kunifanya niendeshe Semi Trailers kazi ambayo ndio ilikua inalipa mshahara mzuri so nikaenda kufanya mtihani wake darasani nikashinda na kupata Kibali cha kuniruhusu kujifunza ili baadaye nikafanye mtihani wa Practical nikishinda niwe Dereva kamili so nikaenda kampuni ya American Harzardous Waste nikaomba kazi ya "UTINGO" ya kuwa msaidizi wa Dreva ili kusudi nipate nafasi ya kujifunza kuendesha nikafanye mtihani wa Leseni niwafanyie kazi Mzungu Jack Supervisor wa Madereva akaniajiri hapo hapo nikaanza rasmi kazi ya Utingo na kazi yangu ilikuwa kusafiri na Dreva na kumsaidia kushusha Makontena ya Harzadous Waste kwa kutumia Hydraulic Lift ambayo imefungwa nyuma ya Truck nilipewa Mzee wa Kijamaica kwa Jina Errol aliyeishia kunisaidia sana kuelekea kupata leseni yangu ...

Now tulikua tunaanza kazi Saa Moja Asubuhi tunatokea Yard The Bronx Market Terminal nyuma ya The Yankee Stadium Bronx tunaingia Manahattan au Brooklyn inategemea kila siku route zilikuwa zinabadilika na kazi yetu ilikuwa ni service kwa Hospitali Kubwa na Ndogo zote it was a fun Job kwanza ilikuwa inanipa nafasi ya kuijua New York City na Vitongoji vyake na pili ilikuwa ni kazi yenye Overtime sana kwani ni almost impossible kuifanya kwa masaa 8 tu kama inavyotakiwa so sasa nikawa na uhakika wa Dola 600 kwa wiki na bado pia nilianza kazi mpya ya kusafisha Jumba la Cinema Co-op City/Bronx ni kazi ambayo nilikua naingia Saa Sita Usiku mpaka Asubuhi ..

Kazi yangu usiku ilikua kusubiri Cinema iishe kuonyeshwa like Saa Sita na Nusu au Saba ninapewa Ukumbi wangu mkubwa mmoja kuusafisha mpaka Asubuhi I was fast nilikua na uwezo wa kusafisha kwa Masaa 2 tu ni kazi ambayo ilikua na changamoto moja kubwa kuondoa Big Gee kwenye Kapeti lakini tulikua tunapewa Special Spray inaondoa mara moja the best of this job was chenji wanazoangusha Watazamaji wa Cinema wakiwa kwenye viti ambavyo vinakua vimepinda ni kazi ambayo nilikua naifanya kwa siku 7 na nilikua na uhakika wa kuokota angalau Dola 10 to 20 kila siku ambazo zilikua nyingi sana kwa maisha yangu madogo sana....ITAENDELEA!
 
Kuna watu wanashindwa tofautisha maana ya neno Hustle/Pambana/Hangaika wanazani ni kubeba mizigo na kukimbia polisi tu!.. kwa jamaa aliyofanya basi alianza hustles toka utotoni aseh!!..
 
PART 9.jpg


PART 9:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Now nilikua napiga kazi ya kusafisha usiku fasta in 2 hours ukumbi una AC na Kapeti saafi so namaliza kazi like Saa Tisa natafuta kona moja safi nalala mpaka Saa 10 na Nusu naamka naingia kazini kwenye Trucks kule nako nilijiwekea tabia ya kuwahi mapema kusudi nipate nafasi ya kujifunza kuendesha mwenyewe na nilianza na kujifunza kurudi nyuma kwa muda mrefu by the time saa ya kuanza kazi ikifika nilikua nimeshatumia like lisaa limoja na mazoezi.

Baada ya Mwezi mmoja nikawa na uwezo wa kuanza kuendesha ila masharti ya Permit ni lazima niendeshe nikiwa na Dreva mwenye leseni kamili kwa sasa kazi zangu zote mbili zilikua zinanilipa Dola 1000 kwa Wiki kama kawaida naziweka Benki tu cause lengo langu lilikua kusoma tu! ...

Nilikua ninafanya kazi kama Punda mpaka sifa zangu zikaanza kuwafikia Wazungu na hasa mwenye Kampuni Msichana Mdogo Dina Muamerika Mtaliano aliyeachiwa Urithi na Baba yake na Mumewe Russ so siku moja Supervisor wangu Jack akaniita na kunipa Great News kua mwenye Kampuni ameniruhusu kuanza kufanya kazi peke yangu yaani nitakua ninaendesha Truck lenye Mataili 18 peke yangu yaani nitakua ninavunja Sheria kwa kuendesha na Permit tu Mzungu Jack akaniambia kuwa makini sana isipokua ukikamatwa tu akanipa namba maalum ya simu ya kupiga Mungu mkubwa sana .

Niliendesha kwa miezi 6 bila kukamatwa na sasa ndio umaarufu wangu wa kupiga kazi Fasta na Perfectly na Consistency ukaanza kua ndio the talk of all my Co-workers mpaka Viongozi wangu wa kazi ...lakini kwa mara ya kwanza in my life nikaanza kugundua kua KUMBE NINA UWEZO MKUBWA WA KUFIKIRI cause Wazungu ndio walioanza kunijadili sana nikiwa sipo na nikawa ninapata feed back kutoka kwa wafanyakazi wenzangu ambao hawakuwa wanapendezwa na sifa zangu za kupiga kazi.

Baada ya Miezi 6 sasa nikawa tayari kwenda kufanya mtihani wa Leseni CDL CLASS A & HAZARDOUS MATERIALS ni Leseni kubwa sana USA ni wachache sana wanazo maana ukishaipata unakuwa a Professional Driver unaweza kusafirisha mpaka Uranium au Silaha kitu ambacho the American Authority wanakiogopa sana sikulala usingizi siku ya kwenda kufanya mtihani sikua naamini kwamba hatimaye nitaipata hiyo Leseni...ITAENDELEA!
 
Anasema zamani kulikua kilikuwa hakuna digree ya leseni ok


Lemutuzi mwisho wa hayo ma digree ilikuwa miaka ya 1972

Kwa hiyo hadi umalize standard 7 na secondary kisha chuoni kwa hiyo umezaliwa mwaka 1956

Huyu jamaa ni babu wa miaka 57 kutokana na story yake ya chuo cha ubaharia


Swissme
acha ujinga mbona mdogo bado mimi nina miaka 89
 
Back
Top Bottom