Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Kaka wakaushie humu fake id zinswafanya madogo kupayuka bila refference wengi ni wahanga wa maisha.
 
Haya maneno yana maana gani??

hayo yote ni majina ya mkuu lemutuz..

ukimuita lemutuz tu bila kuweka hivyo vinjonjo unakuwa umemkosea heshima kwa kiasi kikubwa....

lemutuz bomaye lemutuz citwa yeeen lemutuz mobimba lemutuz nye nye nye alafu unamalizia na ..hahahah i love it you know...

life is too short to be serious all the time
 
Punguza hasira mkuu, mchezo hauhitaji nguvu nyingi hivyo na hasira. Mchezo huu ni nguvu kidogo tu na akili kubwazz basi unawin game. Only you need to know the rules of the game.
 
Nimeanza kukuelewa mkuu. ...najifunza mengi!
 
Nakuongezea tena na title ya kitabu kingine "MY JAMII FORUM LIFE EXPRIENCE " Najua ushawagonga wadada wengi sana humu ndani na pia baada ya kufuatilia comment moja moja kwenye huu uzi wako naona watoto wa kike watakavyojilengesha kwako na imani hutowaacha salama......[emoji2] [emoji2] [emoji2]

Back to the topic hujanijibu ombi langu hapo juu kuhusu kunikodishia shamba lako maana kuna project nataka nifanye kwa maeneo hayo mkuu Le Mtuz Le Mobimbaaaaaaaaaa
 
Wivu unakusumbua hahaha
 

Mzee ingawa unao ushujaa, lakini naona unakosa ushujaa wa kusamehe. Kuna wengine tumeteswa sana na mama wa kambo lakini tulisahau na hivi leo yupo kwangu namuuguza. Nimeshasamehe na sitaki kumuonyesha kinyongo na pamoja yale madhira na mateso aliyotufanyia mimi na kaka zangu hatufikirii kuwaadhibu yeye na wadogo zetu. Wadogo zangu nawapenda sana na sisi tumekuwa ndio baba zao. Wanajifunza na wakati mwingine huyu mama huwakumbusha wajukuu zake jinsi alivyotulea.

Ni kama vile anatubu baada ya kumuonyesha kwamba kisasi hakifai kukilipiza! Mzee hebu jitahidi kutowaonyesha ndugu zako kwamba bado una kinyongo ili muweze kuishi kwa mahaba. Hayo yalishapita na yalishafanyika. Ni Mungu ndiye ajuaye sababu ya kuwaumba viumbe na kuwaletea wenzao masononeko. Hatuwezi jua sababu na hatupaswi kuhukumu kwa kulipiza visasi.

Samahani sana ila ni katika kuwekana sawa.
Visa vya mama zetu wa kambo vinatia maudhi sana na wakati mwingine hutusaidia kujifunza uvumilivu kama na kufanya shughuli za hatari, ni kama huo Ubaharia. Hiyoo ni kazi ngumu na unatakiwa uwe na roho ngumu.
 
Wivu unakusumbua hahaha

mdau huyo jamaa siyo wivu.. fuatilia comment na hata thread zake utagundua kuwa ile 1994 genocide imemuathiri as a result moyoni mwake amejawa na chuki na hasira ambayo haina pa kutokea na matokeo yake amekuwa wa hovyo hovyo sana...

nilimgundua vizuri nilimkuta akiwa kwenye mapigano kwenye thread moja ihusuyo kimbari genocide ndio nikagundua siyo mwenzetu na sio mtu wa kumjibu wala kubisha naye
 
Kuwasamehe waliokukosea ni sawa na kuwapa nafasi ingine ya kukuumiza coz they missed you at first
 
Kuwasamehe waliokukosea ni sawa na kuwapa nafasi ingine ya kukuumiza coz they missed you at first

Ni kweli hicho ukisemacho. Ila binaadamu tunatofautiana sana pindi tunapokosewa na hilo huleta tafsiri na fikra tofauti katika kulipiza au kutolipiza visasi. Tunaona jinsi jirani zetu wa Rwanda wanavyoishi na visasi au Israel na Palestine. Mara nyingi binaadamu tunaogopa kusamehe kwa vile aidha twaweza onekana ni waoga au wanafiki. Hapana, visasi havina mwisho, visasi hukwaza fikra mbadala.

Mafundisho yote ya dini yanatuelekeza katika kusamehe pindi tunakoseana.

Hapa alipo mwenzetu ana wakati mgumu na sio vizuri kuendelea kumuingiza kwenye dunia ya visasi. Mara nyingine inafikia kipindi mtu anafikiri kuunda fasheni ya visasi ili kumuumiza aliyemkosea. Haya sio maisha mema, ni maisha ya kuwindana na kutafutana. Waswahili husema maisha ni kuatafuta na wala sio kutafutana. Nakumbuka wimbo wa Maquis Du Zaire, enzi hizoooo "..... Mutasema mutagombana, wakielewana mutabaki na aibu, wakipatana mutabaki na aibu......" Tuwe waangalifu.

Na hapa kwenye huu ugomvi kuna watu wananufaika na hivyo visasi. Kuna watu huu ugomvi ndio mradi wao wa kimaisha, ndio kula yao inapotokea. Ipo siku hawa ndugu watasahau ugomvi wao na sijui kauli zetu za kiuchochezi tutaziwekaa wapi. Waswahili hunena ndugu wakigombana, .......

Tukumbuke hapa huyu bwana anazungumzia ugomvi wa kifamilia na wanafamilia wana mahusiana ambayo hayafi na wanaunganishwa na damu ya undugu wao. Huyu Bwana kuna kipindi anapokosewa mwanafamilia yake huamka na kuonyesha hisia zake za undugu, huonyesha ameguswa na matatizo ya ndugu yake.

Mwenzetu ni muhanga wa visasi, tunachotakiwa ni kutafuta namna ya kumnasihi na kumuokoa ili asiendelee kuishi dunia ya upweke, dunia ya visasi, dunia ya kufikiri waliomkosea! Yatakiwa tujitahidi kumnasihi na kumpeleka dunia ya kusameheana ili ifike hatua hao wanaomkosea wafikie waone aibu.
 
Le Mutuz huwa anakataa umri wake bure.

Marehemu Mzee Nyirabu alikuwa Office kati ya 1974-1989.

Mzee Jamali Waziri wa Fedha mara ya pili 1979-1983.

Roughly tuchukulie 1983 ndio aliomba Visa ya Belgium. Hadi kumaliza form 4, JKT etc si chini ya miaka 20. Jumlisha tofauti ya 2018 na 1983 inakuja 55 years Ndio Umri watu ambao huwa wanamwabia. Ila yeye anadai ana 35 yrs.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…