PART 27: "MY AMERICAN EXPERIENCE"
Hiyo ni karatasi yangu ya kuwemo Melini CMB Antwerpen/Belgium.
Chanzo cha AKILI KUBWAZZ in me siku zote nilikua ninaamini binadam wote tunafikiria na kuyaona mambo kwa jicho moja kumbe sio kweli na ni kwa mara ya kwanza in my life Joe Orlando akanifanya nigundue hii theory kua nina uwezo mkubwa sana wa kufikiri na kuona mbali kuliko watu wengi.
Ubaguzi wa rangi USA ni tatizo kubwa moja kati ya Hospitali niliyokua naifanyia kazi Lenox Hill Hospital Downtown Manhattan at 76th E Street akaanza kunichukia bila sababu kwa sababu alikua anajua kua kazi yangu inalipa kuliko hata Ubosi wake akaanza kunitafutia visa nilishamgundua loong time ila nilikua namkwepa tu from no where siku moja akampigia Joe Orlando my Boss na kumwambia kwamba kama Hanifukuzi kazi au Hanibadilishii ile route nisije pale atavunja mkataba na Kampuni infact akampa Siku 7 kutimiza hilo.
Orlando akaniita ofisini kwake na kuniuliza tatizo ni nini nikamjibu nikiwa kama kawaida yangu Calm and Collected kuwa tatizo ni Rangi yangu bosi akaniambia nenda kama kawaida usimjali siku ya 7 ilipofika nukamkuta yule Bosi Martinez ananisubiri Loading Dock aliponiona tu akaingia kwenye gari mpaka The Bronx ofisini kwa Joe na Bosi akanipigia simu nirudi haraka niende ofisini kwake nilipofika juu nikamkuta Martinez na Joe.
Boom Joe akaanza kwa kumwambia kua huyu ndiye mfanyakazi ninayemuamini kuliko wote kama humtaki basi unaweza kufuta mkataba wako now!.
Martinez akaanza kujichekesha kumbuka Joe was a Tough Guy mtaani kwenye Mafia Mob so akampa kusuka au kunyoa nikaona Spanish anaanza kujikanyaga kua sio yeye ila bla! bla! bla! Joe akamtunishia msuli kua aseme uamuzi wake haraka! Martinez akaanza kuomba radhi kwa Joe na kwangu kua yaishe hatafanya alichotishia baada ya Martinez kuondoka Joe akaanza kunipa lecture kua tatizo ni Akili zangu nyingi sana ndio maana Weupe wengi waliozoea Weusi wajinga wanakua intimidated na Joe akanipiga marufuku kushiriki Mkutano wowote wa Wafanyakazi wenzangu akaniambia hakuna mtu wa level yako hii Kampuni na kuanzia ile siku akanipa ruhusa ya kufanya kazi Jumamosi na Jumapili ninapoamua mwenyewe siku moja ikaja habari ya MGOMO!..ITAENDELEA