View attachment 703143
PART 50:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"
Picha ni Marehemu Mama yangu mzazi akiwa London ambako alikua akienda mara kwa mara...Matatizo ya Ndoa na Matatizo ya kazi yote kwa mpigo nikaanza kumkumbuka Mama yangu siku moja aliingia Chumbani kwangu ghafla nikiwa mdogo ninakaa kwa Uncle Lusinde, akanikuta na Cash nyingi sana alipigwa na mshangao akaniambia "William unapenda maisha makubwa sana utayapata lakini yatakugharimu sana" .
Infact Mama yangu mzazi hakutaka kabisa kusikia habari za kumuoa mke wangu na hata Baba yangu hakutaka na Dada yangu mmoja pamoja uadui wetu bado na yeye alipinga openly. Wazazi wangu ya kumkataa waliyasemea in Private lakini Dada yangu alimuambia yeye mwenyewe kabla ya kufunga ndoa kua haungi mkono ndoa cause anajua kua nitakuja kuumia tu lakini wote in the end wakaheshimu uamuzi wangu so now yamenikuta ninamkimbilia nani? ...
Marehemu Mama yangu amechafuliwa sana na my ex wife na anaowatumia Mama yangu alikua Miss Tukuyu, akawa Miss Mbeya, then Miss Tanzania na Miss East Africa baadaye Mwalimu Baba wa Taifa alimtumia sana kwenye kujenga UWT na Mama Sophia Kawawa ninakumbuka sana nikiwa mdogo akawa Muwakilishi wa UWT Taifa Mikutano ya Kimataifa sawa hakua na Elimu kubwa sana lakini alikulia Malawi alikua na uwezo wa kuongea Fluent English alikua anasafiri all the times nje ya Nchi ...lakini kwa makusudi kabisa ametukanwa sana kwamba eti alikua ni muhudumu wa Gesti ...
Marehemu Mama yangu alikua ni mfanyakazi wa NBC tawi la Clock Tower kwa muda mrefu sana huku akiwa ni Kiongozi wa UWT Taifa alijenga makazi mazuri sana Kigamboni siku moja Jeshi wakachukua lile eneo na kumlipa pesa ndefu sana akajenga Nyumba kubwa na Shamba Minazi Mirefu/Ukonga ...lakini ukisoma matusi ya my ex kwa mama yangu hutaamini kua anyezungumziwa ni huyu Marehemu Mama yangu aliyekua anasafiri nje kila wakati ....
Sawa sikatai kua in the end hakuwa na maisha mazuri sana kama aliyokua nayo zamani lakini ilitokana na matatizo mengi aliyoyapitia mimi nikiwa nje ambayo yalimvuruga sana kisaikilojia na ambayo hayakunihusu na ndio yaliyompelekea kuuza kila kitu na kuhamia Tunduma by the time ninarudi nikamkuta huko!
.....ITAENDELEA