Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Duuh,Le mutuz sasa unatuliza machozi,kiumbe wa mungu kupitia yote haya!!!!!!!!!! Putting myself in your shoes ningekuwa nimeshajinyonga-God bless you,na utusamehe tuliokuhukumu negatively before
Kwa kweli tusamehewe,ni kutokujua,apo kwenye kudhalilishwa mama ndo pameniumiza,mana kama ningekua mimi mama angu ndo anafanyiwa hivyo,saiv nipo gerezani kwa kesi ya kuua[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
upload_2018-3-2_16-16-54.jpeg

PART 62:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Picha hii ni Wiki 3 Bongo with the people I grew up with Spearman, Michuzi, Majid, Holera and Seydou... Peter akawapigia simu watoto wangu wakashuka chini waliponiona wakaingia ndani ya Gari kwa furaha sana nikawapa Dola 100 kila mmoja nikawaambia nasafiri nitarudi Jumatatu, I kissed them wakashuka tukaondoka na Peter to JFK Airport.

Njia nzima sikumpa nafasi Peter ya kufikiria ninafanya nini nikawa namchekesha sana kuhusu Taarabu ya jana usiku ya Mzee Yusuph nikamuambia "Unajua haya mambo ya kukaa sana USA mpaka tunanza kwenda out kwenye Taarabu ni kwa sababu hatuna pa kwenda, mimi bongo sijawahi kutoka kwenye out Taarabu" nikamwambia "Ni ujumbe kua saa ya kurudi Bongo imefika" alicheka njia nzima tulipofika nikamuambia nitakuwepo kwa muda mrefu pale Uwanjani nikimaliza nitampigia akanishusha akaondoka ...

Boom kufumba na kufumbua nilikua ndani ya Swiss Air tayari kwa safari nikampigia Bosi wa my ex kua nimo ndani ya Ndege tayari alifurahi sana sana kupita maelezo tukasali pamoja then nikampigia Peter nikamjulisha kua in the next 10 minutes nitakua hewani kuelekea Bongo ndio imetoka ila nikamuomba ampe ujumbe my ex kua kazini nimemuachia makaratasi ya Tax Returns akienda watampa na atapata pesa zangu Dola 10K azitumie kwa Watoto mimi nimerudi Bongo ..

Nikamuambia Peter ufunguo wa nyumba ulipo akauchukue ampe my ex akachukue vitu vyote ndani ya my home for my kids ...Peter was in a big Shock lakini nikamwambia nitampigia nikifika Zurich kusikia reaction ..hahahaha...kweli nilipofika tu Zurich nikampigia Peter kujua reactions U know ....hahahaha ...Kaboom!

...ITAENDELEA!
 
Kweli lekokobanga nakukubali bro maana ukiachia tuu hiyo stori yako mwenyewe na ulivyokua unapambana na shetani mchonganishi katika Maisha yako.
Humu pia kulikua na shwetani wawili Yule shetani @ the List na mwenzie shetwani @ case! Ila naona kama wamefyta until further notice!
You are humble you know!
 
upload_2018-3-2_19-31-6.jpeg

PART 63:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"
Leo nimeshindwa kulala simu nyingi kutoka kila kona ya Dunia wanaulizia kitabu na nimailizie Story ok leo nitakutana na mtu wa kitabu NAWAOMBA MTULIE GUYS KITABU KINAKUJA SOON NITAWAAMBIA HAPA HAPA ...Nikafika Zurich salama salimini nikanunua Airtime nikampigia Peter na kumuuliza VIPI HUKOOO? hahahaha majibu yalikua kama nilivyotegemea my ex na genge lake walipigwa na a Shock of their lives wakakusanyika kwa my ex kujadiliana wafanye nini huku wakijaribu kumpa nguvu my ex kua asijali sana wapo naye pamoja ..wakachukua ufunguo kwa Peter na kwenda kwenye my home wakachukua walivyovitaka isipokua kama kawaida ya Shetani wakaanza matusi na kashfa lakini hizi habari za kuondoka kwangu kininja ziliwashitua Jumuiya nzima ya Wabongo New York na USA nzima haikuwahi kutokea a Powerfull Figure Mbongo as I was kufanya niliyoyafanya.

I was an Icon kwa wabongo pamoja na Chuki zao lakini nilikua ni mfano wa kwenda USA kama an Economic Refugee kupigana na maisha mpaka kufanikiwa nilikua ni among Wabongo walioishi muda mrefu sana New York I mean 25 years so leo mimi nikikimbia USA maana yake ni kwamba kuna kitu nimeshituka kuhusu yale maisha ambayo wengi hapa Bongo wanayalilia bila kujua ukweli wa undani wake ...

Guys hakuna Mbongo anayeishi USA au Majuu ambaye hajui kwamba yale sio maisha mazuri sana kwa sisi tuliokulia Third World. Sawa kuna wachache ambao Wana Maisha mazuri sana ambao wamesoma na wana proper papers lakini kwa Wakimbizi wa Uchumi like me unahitaji kupigana sana as I did maisha yangu yote Majuu NILIJUA KWAMBA TUMESHINDWA MAISHA BONGO yes nilijua Wanaume wamebaki Bongo wanapigana wanakuja USA kufanya shopping za harusi but after 25 years in USA unarudije Bongo na Dola 1000 tu na mabegi 2 ya nguo?

Hahaha Mungu ametuumba tofauti sana in my case nguvu kubwa ya kurudi nilikua na imani ya AKILI KUBWA tu ambayo sikua nayo kabla ya kwenda Majuu but kwa Wananchi wa kawaida ambao kwao maendeleo ya kuishi Majuu kwa muda kama niliouishi ni kukuona na Magari ya kifahari ITAKUAJE? nikajipa moyo kwamba watu wasionihusu hawajawahi kua tatizo in my life kama nilienda Majuu bila kitu nikapigana hata Bongo ninaweza kupigana nikasimama

...ITAENDELEA
 
Kweli lekokobanga nakukubali bro maana ukiachia tuu hiyo stori yako mwenyewe na ulivyokua unapambana na shetani mchonganishi katika Maisha yako.
Humu pia kulikua na shwetani wawili Yule shetani @ the List na mwenzie shetwani @ case! Ila naona kama wamefyta until further notice!
You are humble you know!
Ni shetani ndo anafanya kazi ya kupelekesha akili za watu mpaka tunashindwa kuelewana[emoji2] hivyo ukiona mtu anafanya kitu kibaya ujue shetani ndo kamtuma
 
upload_2018-3-2_20-26-37.jpeg

PART 64:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Niliwahi kuishi Shanghai/China kwa miezi 3 Wachina walinifundisha Somo moja muhimu sana for my life mpaka leo "KUA NI MUHIMU SANA KUWA NA IMAGE YA MJINGA UNAPOFIKA UGENINI". Wenyeji wakiamini ni Mjinga watakuachia Milango yote wazi ila wakishituka kua ni mjanja from day One watakufungia milango hapo hapo utaumia now kwa wale Wengi mnaonijua kwa karibu mnajua kwamba UJINGA ndio my ID.

Always ukiniona kwa mara ya kwanza na kwa sababu ulishasikia mengi negatively kutoka kwa my ex na Mange in the Social Media na kwa vile wewe ni mjinga sana kupita maelezo unajiaminisha kua Le Mutuz ni mjinga mjinga fulani hivi hua nawasoma sana kwenye sura zenu na hua inanipa nguvu sana in me kua kama nimekuja ofisini kwako na shida nitafanikiwa tu WHY? Ulishani underestimate mapema ila ninakuhakikishia dakika Tano tu za kukutana na mimi uso kwa uso hutarudia tena kujifanya unanijua kua ni mjinga cause kwa mara ya kwanza utagundua kua Mjinga ni wewe ukiyenihukumu bila kunijua cause nitakua nimeshapata nilichokitaka kwako na nilishaondoka fasta ...

Now Peter was happy akaniambia ulichokifanya ni impossible ila Bongo utenda kufanya nini? nikamuambia ndio maana sikumuambia mapema maana nisingeondoka ...my ex akaenda kazini kwangu wakampa makaratasi ya Tax Returns zangu nilizomuachia na baadaye wakampa Dola Elfu Kumi nilizomuachia kwa ajili ya Watoto lakini hili hajawahi kulisema hata siku moja katika matusi yake yote ...

Pale pale nikiwa Zurich nikaona Jamiiforums kuhusu kukimbia kwangu na kutelekeza mke na watoto hahahaha nikaona picha ya ndani ya nyumba yangu zimepostiwa tayari jinsi nilivyoiacha Masikini ya Mungu akili ndogo my ex bado haelewi kua adui wake namba moja ni yeye mwenyewe na hasa ujinga wake I mean kuhusu hasira ya Wabongo wengine niliwaelewa walikua na point kwamba Misery Loves Company maumivu yanapendeza mkiwa wengi mnayapitia now kuishi Majuu wote mnajua kua mpo kama Jela fulani hivi Kisaikolojia na Sheria ya Jela ni mnalindana kuona hakuna anayetoka sasa siku mmojawenu akiondoka inakua huzuni nyuma ndio maana nilielewa Hasira ya Wabongo wengine against me na wao wakaanza kunishambulia left and right na wote hasira yao waka

...ITAENDELEA
 
upload_2018-3-2_20-42-21.jpeg

PART 65:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"

Ninaipenda sana hii picha cause ndio alama yangu pekee ya Amani bila mali baada ya kufika Bongo ..Bado sijaondoka Zurich nikaendelea kuona hasira za Wabongo niliowaacha USA my ex na genge lake wakaelekeza kwenye Watoto tu kua kakimbia Watoto so kwa kila anayesikia hii Watoto Theory ni rahisi sana kunihukumu kua ni kweli now leo naomba niliweke tena sawa hili la Watoto Theory..

Yes ninao Watoto 2 ambao nilizaa na my ex Wa Kiume mkubwa na Wa Kike. Nilipokua ninaondoka Walikua wakubwa at the Age of mkubwa alikua 14 na mdogo 12, hawakua watoto wachanga na uamuzi wa yaliyotokea ulikua ni wa Mama yao sio mimi na Sheria ya USA ilikua upande wake. My thinking ni sikua na Choice tofauti na niliyoifanya cause ilikua aidha niishi kwa shida kwa sababu ya kua karibu na Watoto au Niachane nao na niwasaidie kwa mbali lakini nikiwa na amani nikachagua la Pili na mimi sio wa kwanza kwenye maisha, hata mimi sikuelelewa na Baba yangu mzazi lakini leo we are close friends pamoja na Juhudi kubwa za marehemu Mama yangu kutaka nimchukie yes kuna wakati nilimchukia lakini later on nikagundua makosa mengi yalikua ni ya Mama yangu Mungu Amuweke Pema Peponi (AMEEN)

Kuna siku niliwahi kumuweka chini Mama yangu mzazi na kumpa somo zito sana almost maasa 3 kuhusu the ishu ya yeye na maisha yangu. Toka siku ile nikawa na Amani kubwa sana cause nakumbuka alivyolia sana kwa uchungu wa kujua kua kumbe ninajua yote kuliko alivyokua akifikiria ...so here the Ishu ya Watoto wangu as much as I am not very proud of lakini it was a reality of life I had to face it na kuitolea maamuzi magumu sana cause the thing was MY LIFE FIRST sikuwa tayari kuishi kama nilivyowaona Wabongo wengi waliotumbukia mtego kama wa my ex wa kuishi kama mtumwa wa Mama wa watoto wako kisa Sheria za USA na ujinga wa your ex.

Nilisema not me nitarudi Bongo sikumuua mtu nitapigana na kuanza upya nitakua tu nitawatumia pesa watoto nikiwa Bongo which mwanzoni I did kabla kichaa cha my ex hakijamshika tena na kunianzishia matatizo mapya kabisa na Watoto .so makelele kutoka USA nikiwa Zurich hayakunishitua na besides Wangenyamaza kimya ningejisikia vibaya sana ingenisumbua sana kua yaani kuondoka kwangu.ITAENDELEA
 
upload_2018-3-2_21-17-3.jpeg

PART 66:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"
Picha ya maneno yanayoniongoza sana in my life ...Swiss Air ikaruka from Zurich I was happy that kuondoka kwangu USA kumeacha a big impact sikua na wasi wasi sana. Nilijua wasioelewa watakuja kuelewa tu baadaye kilichotokea lakini yalikua maamuzi magumu mazito I had to take kujilinda mimi kwanza. Kwa mara nyingine nikajifunza its not about Mali na Dunia its about Peace Of Mind First ..

Now nikaanza kupiga picha ya nitakapofika Bongo yes Baba yangu alikua anajua na nilikua ninafikia nyumbani kwake Seaview kwa sababu nyumba yangu Kinyerezi haijaisha lakini hata ingekua ningeanzaje? ..baada ya kumnunulia zawadi Baba yangu Duty Free nikawa nimebaki exactly na Dola 1000 tu! Kila nilipojaribu kufikiria Bongo akili ilikua inagonga ukuta nikaamua kuacha kabisa kufikiria Bongo na kujali kufika kwanza na Amani yangu kwanza mengine baadaye.

Nilikua ninajua Uadui wa baina yangu na Dada zangu from my Step Mother lakini sikujua how big umefikia mpaka nilipofikia nyumbani kwa Baba yangu ...nikafika JKN straight home ilikua usiku nikapewa Chumba nilichoishia kuishi kwa Mwaka mzima huku nikiwa natafuta Apartment Mjini kimya kimya bila kumuambia mtu. Isipokua nikatulia sana baada ya kufika nilikua nalala sana Maisha yangu yote nilikua nakimbia Maili 10 kwa siku kila asubuhi lakini toka matatizo ya my ex yaanze nikaacha...

Baada ya Wiki moja tu ya kupumzika nikaanza kupiga hesabu wapi pa kuanzia? Nikaenda GMO pale Samora Avenue nikanunua a Used Laptop aina ya Dell nikafungua "LE MUTUZ BLOGU YA WANANCHI". Makelele kutoka USA yakawa yanakuja kwa magunia duh sikuamini my ex genge lake waliposikia nimefungua Blog wwkaandika Barua Interpol na Google kuomba ifungwe kwa bahati nzuri Ofisa mmoja mkubwa wa Serikali anayenifahamu akanionyesha Copy iliyotumwa Kitengo kimoja Serikalini..

The next thing is my ex ikawa inabidi asaidiwe na Serikali na ili kupata ule msaada kutoka kwenye my penshion ilikua ni lazima mimi nisaini makaratasi fulani ya Serikali kumruhusu asaidiwe so akamtuma Kaka yake aliyenifuata kwa upole sana nimsadiie kusaini ila nilitakiwa nikayasaiini Ubalozi wa USA nikaenda nikasaini bila ubishi akaanza kusaidiwa na baada ya kama wiki 2
..ITAENDELEA
 
Le mutuz we ni mwanaume yaan nawaza tu hapo mama alivyokulisha sumu kuhusu baba lakini mwisho wa siku haujayasikiliza ulikuwa sawa na baba yako ni watoto wachache wenye moyo huo

Ila huyu x wife wako alikuwa na roho mbaya sana sana anasahau kama mmezaa wanawake sisi
 
Le mutuz we ni mwanaume yaan nawaza tu hapo mama alivyokulisha sumu kuhusu baba lakini mwisho wa siku haujayasikiliza ulikuwa sawa na baba yako ni watoto wachache wenye moyo huo

Ila huyu x wife wako alikuwa na roho mbaya sana sana anasahau kama mmezaa wanawake sisi
X wife ni katili kabisa,sema ndoa za ughaibuni zina changamoto-Amani ni kitu cha nadra sana,rights zote tumepewa wanawake,mwanaume akipatikana huteseka sana-i have seen these scenario's with my own eyes.Happily married and after a couple of years,a brutal messy divorce battle
 
huyu jamaa amepitia maisha ya ajabu sana, mke wake ni mgumu sana, dada zake ni wa kuwakimbia kama nyoka. roho hiyo walichukua wapi? thank God babake alimpenda/anampenda the same way I will love my son from another woman.
Inapendeza ulivyojirudi ......
Boma yee anatoa fundisho sio kwa vijana tuu hata kwa aged kutokana na masahibu uliyopitia na kwa kweli zaidi ya nusu ya waliokuwa wanammbeza nahis watakuwa wanajisikia vibaya kwa kadiri episode zinavyoelekea mwisho
 
X wife ni katili kabisa,sema ndoa za ughaibuni zina changamoto-Amani ni kitu cha nadra sana,rights zote tumepewa wanawake,mwanaume akipatikana huteseka sana-i have seen these scenario's with my own eyes.Happily married and after a couple of years,a brutal messy divorce battle

Sahihi kabisa,

Ndoa nyingi za watanzania wenzetu zimepitia changamoto kama hii ya bro William huko Ughaibuni, esp Western Europe na America.

Huwa najiuliza tatizo ni madada zetu wakifika Ughaibuni, wanadanganyika/kushawishika sana na desturi "mpya" za kimagharibi, kwamba mwanamke akiachika anapewa nyumba na child care support? ....Au ni frustration tu za Wabongo ughaibuni, ambao majority hawapendi maendeleo ya wabongo wenzao. changanya hapo na mke ambaye akili zake anachanganya na za wengine!

Nashawishika kusema, asilimia kubwa ya ndoa za wa Kitanzania zilizovunjika Ughaibuni zingeweza kudumu iwapo wahusika wangekuwa nyumbani Tanzania, ambapo wamezungukwa na jamii inayoheshimu mila na desturi zake.

Naamini, ipo siku tathmini na takwimu zitathibitisha ukweli huu usiopingika kwamba Bro William ni mmojawapo wa wahanga wa tatizo hili sugu la ndoa nyingi za vijana wa Wabongo kuvunjika Ughaibuni.

Wanaume wengi wa kibongo either wame lost kabisa, au wanaendelea kuugulia kimya kimya Ughaibuni kwa maswahiba haya!
 
upload_2018-3-3_9-20-12.jpeg

PART 67:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"
Wiki mbili after makaratasi ya Divorce yakaja again nikaenda Ubalozi wa USA nikasaini. La msingi kwenye makubaliano lilikua kuwasidia watoto wangu nikiwa huku Bongo as much as I could na kweli nikaanza pole pole kuwatumia kuanzia Dola 100 mpaka nikaanza kutuma Dola 1000, na siku zote nilikua namtumia Peter mshikaji wangu ndiye anampa. Msimamo wangu ulikua SITAKUJA KUINGEA NA MY EX DIRECT, NEVER na mpaka leo lakini nikimuhitaji kuhusu Watoto ninamtumia Boss wake kazini na yeye pia nilimtaka afanye hivyo. DIRECT COMMUNICATIONS ILIKATAA KATA KATA MPAKA LEO ...

My Justifications are Shetani amenishambulia sana kwa kumtumia mama wa watoto wangu kabisa now amenishindwa lakini Biblia inasema Shetani hua hakubali kushindwa atarudi nyuma na kujipanga tena atakurudia kwa njia mbali mbali so kuepusha yote ni kumkwepa kabisa mapema. Simuamini my ex hata for a minute in life. Tunatakiwa kuwapima Binadam wengine kwa kujiangalia wenyewe kwanza ninarudia MIMI SIO MKAMILIFU lakini sijawahi kua na nia mbaya na mtu NEVER nina mapungufu ya Revenge kulipa kisasi lakini hata hilo huwa ninalifanya very quietly bila kukufanya uliyenikosea kushituka mapema na hua ninalifanya only ukivuka mistari ya ustaarabu ...

Nilikua ninawasiliana na watoto wangu bila tatizo siku moja rafiki yangu Peter akaniambia my ex ameanza kuwa karibu naye sana nikamuonya awe muangalifu sana maana ninamjua sana asipokua makini tutaishia kugombana na kuvunja urafiki wetu Peter hakunielewa... Siku moja my ex akanipigia simu nilipojua ni yeye nikaikata alipiga mara 6 nikakataa kabisa na kumfahamisha Bosi wake kua mbona tulishakubaliana no direct communications kwanini ananipigia? ...the next thing Peter akanipigia simu siku moja akaniambia kuna mtu anataka niongee naye ghafla my ex nikatupa simu woow my ex akaanzisha ugomvi na Peter kua mimi ni mkorofi nimekata simu bila kuuliza ni kwa sababu mtoto anaumwa, NONSENSE. So ningeongea naye ningemsaidia nini hasa nikiwa Bongo? ...

Ok, kesho yake nikamtumia Peter Dola 200 awagawie watoto baada ya kutuma Dola 1000 a week kabla alipomuambia my ex kua ana hela za watoto my ex akaja juu kua hazitaki kwa sababu ninamdhalilisha na vipesa

..ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom