Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Mkuu Hute hapa kwenye swala la "maisha mazuri" naona umechemka mbaya. Mimi binafsi naamini mtu unaweza kuwa unaishi hata kwenye nyumba ya "nyasi" lakini bado ukawa na maisha mazuri. Maisha mazuri siyo kuwa na majumba kama ya Trump, maisha mazuri ni kuridhika na kile ulichonacho. Unaweza kuwa na mali kuliko hata za Bill Gates lakini bado usiwe na maisha mazuri.mkuu tusibishane, mimi ninakufahamu vizuri sana, usifikiri nimekufahamia kwenye mitandao. sasa kulinda heshima yako ngoja tujadili mengine, ila msg yangu ndio ilikuwa hiyo. lakini yote katika yote, still kuna vitu vingi nimejifunza toka kwako hasa kufanya kazi kwa bidii na kuvumilia vitu, pamoja na kwamba kuna mapungufu mengi sana ambayo sihitaji kabisa kujifunza toka kwako kwasababu kuna baadhi ya tabia zako mimi nimeziepuka na zimenipa faida kubwa sana maishani mwangu. ndo maana nilikuwa nasema usisema una akili kubwa, acha watu ndio wakuite una akili kubwa, wewe binafsi huwezi kujijua.
vilevile, unaweza kuwa unamiss point ya definition ya "maisha mazuri", what does maisha mazuri mean to you? ni kutoka na wabebez, kwenda vacation dubai au souz, kuiishi 30 years majuu? kula vizuri kwenye appartment ya kupanga?, definition yako ya maisha mazuri ni ipi? kuishi na mwili mkubwa kama tembo kama unakula garbage kila siku?
Mimi nakubaliana kabisa na Le Mutuz, yeye ameridhika na maisha yake na tena anaishi huku akiyafurahia, wazungu wanasema "he is living large", kila mwisho wa mwaka anakwenda "vacation", ameishi USA for 25 years, ana mashamba yake anayoyamiliki, ana nyumba, ana watoto wake 2 na isitoshe ana biashara yake inayomuingizia kipato; kwake yeye na ukilinganisha na average ya maisha ya Wabongo wengi, yeye yuko juu sana tu, tena sana. Hivi nikuulize swali dogo tu na rahisi, ni Wabongo wangapi wanaweza kumudu kuishi kwenye "apartments" kama anazokaa Le Mutuz???
Kwa kifupi kuwa na maisha mazuri ni kuridhika na kufurahia kile ulichonacho na siyo jamii inayokuzunguka kuridhika na kile ulichonacho. Mimi namkubali sana Le Mutuz kwa kuwa ameridhika na maisha na anafurahia sana maisha yake. Wengi wa Wabongo wanaomchukia Le Mutuz, walitamani sana kuishi maisha kama yake lakini hawawezi hata robo tu.