chimagoli shitunguru
Member
- Feb 27, 2018
- 7
- 9
Be humble kokabanga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tulimkosea sana kaka wa watu mungu mkubwa angekufa tungedaiwa yaaniDuuh,Le mutuz sasa unatuliza machozi,kiumbe wa mungu kupitia yote haya!!!!!!!!!! Putting myself in your shoes ningekuwa nimeshajinyonga-God bless you,na utusamehe tuliokuhukumu negatively before
Ahahaaa ngozi yangu baado sana kusugua
ilianza kama vichekesho na story ya majigambo ikaja kuwa ya kutafuta sympathy kwetu kwa kale kavideo,sasa imeturn na kuwa habari ya kututoa au kukaribia kututoa machozi.Mkuu heshima kwako na pole kwa uliyopitiaView attachment 703460
PART 54:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"
I was a strongman kila Mbongo alikua analikubali hilo so now ilikua zamu yao kumkomoa a Strongman so Wanawake wote wajinga in that Society ya Wabongo wakakusanyana kupanga namna ya kunikomoa kwa kutumia Sheria za Kimarekani. Waliamini kwa vile mshahara wangu ni mkubwa basi utachukuliwa robo tatu na serikali atapewa my ex na ataishi anavyotaka na mimi nitasota kuna wabongo ambao tukiwa kwenye ndoa tulikua hatujihusishi nao kabisa infact walikua wanamchukia sana my ex kua anaringa sana kwa kua ni mke wangu ghafla wakawa marafiki zake ...
Kwa sababu nilikua kimya na very private mke wangu akawa anaongea na kusema anything negative, wakawa wanaamini maana ndiye pekee aliyewahi kuna na access na mimi ndipo nikajifunza kwa mara ya kwanza kua hakuna makosa kama ya kunyamaza kimya mbele ya mashambulizi watu wanaamini kwa urahisi so nikaanza kujibu ingawa kwa kistaarabu sana hasa Facebook na Jamiiforums lakini it was bad nikagundua mkiachana tu jamii automatically inaamini maneno ya Mwanamke kwanza na my ex was so Good in talking trash na alikua anapigania sana line ya kwamba yeye ameniacha mimi na Sheria za USA zikamfanya awe na kiburi cha ajabu.
Nilikua nimeambiwa na Polisi nisisogee Shuleni kwa watoto kwa Maili moja ulikua ni usumbufu uliowaumiza sana watoto nikaamua kuanza kuwachukua Mlangoni kama zamani siku moja my ex akamtuma rafiki yake kuja kuniangalia kama ninatii hiyo amri lahaula nilipowachukua tu Mlangoni nikasikia simu yake ninakumbuka alivyokua anafoka kwa jeuri sana akasema "Usinilazimishe kufanya nisiyoyataka" usirudie tena kuwachukua mlangoni siku hiyo nikaamua kuacha kabisa kuwachukua watoto Shuleni nikamuambia sitaenda tena kuwachukua watoto wangu kwa masharti enough!
Wenzake wakamtafutia Wanasheria wa kumsaidia kunikomoa Mahakamani hata One of my step Sister ambaye ni Mwanasheria waliyekua naye ofisi moja naye alikua anamsaidia kunimaliza the idea ilikua ni kunifundisha adabu kwa kosa la kua too Strong of a Man na Wanaume wenzangu wanyonge wanyonge walifurahia sana hii episode kua hatimaye mjanja kapatikana tuone sasa nilikua na Rafiki mmoja tu Peter Luangisa na wazungu basi
...ITAENDELEA
True atusamehe Kwa kweli wengi hatukuujua ukweli thus why tulikuwa tukimdiss,Jamaa ni fighter na akili kubwa sema kalostisha na huo ex wife wake Bila yeye angekuwa mbali sana kiuchumiTulimkosea sana kaka wa watu mungu mkubwa angekufa tungedaiwa yaani
Wanawake bana!! Ndio maana Biblia inasema, enyi waume muishi na wake zenu kwa akili!!!View attachment 703472
PART 55:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"
Pichani na rafiki pekee niliyekua naye USA mpaka leo Peter Luangisa....ni mbongo pekee tuliyekua tunaelewana na tunaelewana mpaka leo ananjiua na ninamjua tumeishia kua ndugu ndio alipofiwa na Baba yake niliruka kwenda Bukoba bila kufikiri mara mbili na hata majuzi tena kwenye kumbu kumbu ya Baba yake tena nilikua wa kwanza Bukoba kumpa support ni binadam mmoja tu aliyekubali kuchukiwa na wajinga wote kua rafiki yangu na mpaka leo jamii nzima ya Wabongo New York inamchukia kwa sababu ya kua close to me tulikua tunatumia masaa kuongea kuhusu situation iliyonikuta ...
Upande wa pili my ex na kundi lake wakawa wanatengeneza mkakati wa pigo moja ili kunimaliza kwangu yalikua ni maajabu ya Dunia Wanawake ambao wana ndoa zilizooza kabisa kwenye ile jamii yetu sasa ndio waliokua Waalimu wakubwa wa my ex I mean Kiongozi wake namba moja alikua ni yule Dada aliyefurahia sana kurudishwa kwake Bongo iile Deportation aliyekua na ndoa mbovu kuliko zote lakini hapa ndiye aliyekua kiongozi wa kumshauri my ex afanye Divorce magari mabovu yanajaribu kuvutana na ujumbe kwangu ulikua very clear kwamba nikifanya kosa moja tu kwenye kufikiri this time Shetani atanimaliza kweli sawa nimepigana sana na Shetani huko nyuma na kumshinda lakini hili la safari hii lilikua sio mchezo.
Kwa mara ya kwanza nikaanza kukubali ndani ya nafsi yangu kua Shetani amenibana lakini nikajiuliza swali moja la msingi sana je ni UJUMBE KUTOKA KWA MUNGU KUA SAA YA KURUDI NYUMBANI BONGO IMEFIKA?...but swali likawa ninarudi wapi na kufanya nini after 30 years? kwani majuu nilikuja kufanya nini? Ok kwanza nilienda kutafuta maisha mazuri na Elimu pesa zangu karibu zote ziliishia kwenye Elimu lakini nilinunua shamba na nilijenga Nyumba ila cha msingi ni hakuna price ya Akili Kubwa niliyoipata USA.
Sasa nilikua na uwezo wa kufikiri na kuona mbali sana as opposed na kabla sijaenda then nikaanzaa kutafakari yote yaliyofanywa na my ex na kundi lake cause kwenye Criminology nilifundishwa binadam sio mkamilifu siku zote kuna mahali atakosea tu ila inahitaji umakini kuona alipokosea nikagundua kosa kubwa la my ex na wanaomshauri kua kuna kona hawajaliona nikaanza ku smile!
..ITAENDELEA
W. J. Malecela mbn inaonekana kama mpk ndugu zako wa karibu kama huyo step sister wako walikuchukia sana why? Au tatzo ni wewe je mdogo wako samwel nae anakuchukuliaje
Historia yako inasikitisha, inasononesha na wakati mwingine inafurahisha..
Nikupe pole kwa yote uliyopitia hasa wakati wa utoto wako na naweza sema shida/matatizo uliyopitia hasa kutoka kwa watu wazima ambao wajibu wao walitakiwa wakulinde lkn ndo walikuona adui wao..rejea mama wa kambo...
Na hii imekufanya kuwa ulivyo...Sasa ninakuelewa ni kwanini huko hivyo ulivyo...Ulichagua njia sahihi ambayo umekufanya uwe strong..
Ukiangalia unapitia njia ngumu maana maadui zako ni ndugu zako wa karibu...mama wa kambo, dada zako, mkeo, na si ajabu watoto wako na mzee wako pia...Sasa Girlfriend na video yako..
Hii itakufanya kutojenga imani tena kwa mkeo mtarajiwa...kitu ambacho hata kwa mkeo ulikuwa hivyo..hii yote ninaweza sema inatokana na wazazi kutowajibika kwa watoto wao wakiwa wadogo...
Mpaka hapo wewe ni mshindi...