Leading Without a Title: Zitto Zuberi Kabwe si wa Kubezwa

Leading Without a Title: Zitto Zuberi Kabwe si wa Kubezwa

Status
Not open for further replies.

busar

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,067
Ndugu!

Utangulizi

Nimetafakari sana juu ya Siasa za Tanzania. Nimeangalia kwa upana siasa zetu za Sasa (za kileo). Nikatazama mustakabali wa huko tuendako. Kama tunataka mabadiliko basi TUNAHITAJI WANASIASA VIJANA WAJANJA.

Dhima

Tupate watu wafaao kwa kuangalia waliopo.

Kiini.

Tumempoteza Maalimu Seif. Mwanzo Hizbu, akajakuwa ASP, CCM, CUF, baadae ACT-Wazalendo.

Tunajifunza nini? Jenga Mvuto na Nguvu kwa jamii yako bila kujali ni ndogo kiasi gani. Pemba ilimjenga Maalimu.

Turudi bara kwa Sasa.

Katika wanasiasa wa nje ya CCM naona Zitto ana Nguvu kubwa sana ya kuamua mwelekeo wa Siasa yetu kutokea upinzani.

Kwa sasa lazima ZZK awe sehemu ya mjadala muhimu wa nani anajaza nafasi ya VP Zenji. TISS hawana namna ya kumkwepa. ZZK katika hilo. Anaweza kutaka lolote. Liwe la kifedha, vitu au heshima. Lakini pongezi kwako ZZK. Nitajiunga na ACT Wazalendo.
 
Upvote 5
CCM inalea vijana na kuwapa miongozo, kila hatua inayopiga kuna mzee au wazee wa kukuweka sawa na kukupa mawaidha. Kitu ambacho ni hadimu sana kwenye upinzani. Na hii sio kwamba CCM ni chama dola au kina hazina ya wazee, ni vyama vya upinzani kushindwa kujenga programu ya kulea vijana. (Kitu ambacho kinarekebishwa.)

Wote kina Kikwete, Magufuli mpaka kina Januari, Polepole nk.. Wakati wa kipindi chao walikuwa na waangalizi au wao wamekuwa waangalizi wa wengine.

..ccm wanabebwa na vyombo vya dola.

..bila vyombo vya dola sidhani kama ccm itaweza siasa za ushindani.
 
Kinyonga hana na hatakaa awe na rangi moja...once a traitor always a traitor...ubinafsi ni hulka yake na hatokaa abadilike
Kwanini unadhani Zzk ni mbinafsi?

1. Aliijenga CHADEMA, Akaipa Nguvu ya kupendwa hasa na vijana.
2. Ni mkomavu, alichagua tangu mwanzo Siasa Yenye staha isiyo na matusi.
3. Akafukuzwa CHADEMA
4. Akaanzisha ACT

SASA LEO ATASIMAMIA UPATIKANAJI WA VP ZENJI. IDARA NYETI ZA NCHI ZINAHITAJI KUONGEA NAE.

Ni mwanasiasa Mkubwa
 
Kwa Sasa lazima Zzk awe sehemu ya mjadala muhimu wa nani anajaza nafasi ya VP Zenji. TISS hawana namna ya kumkwepa.Zzk Katika Hilo. Anaweza kutaka lolote. Liwe la kifedha, vitu au heshma. Lkn Pongezi kwako zzk. Nitajiunga na ACT Wazalendo
Huzijui siasa za Zanzibar
Ni Mazrui au Duni Haji na genge lao ndio watakaoamua Nani awe Makumu wa kwanza wa Rais,Zitto hana ubavu wa kuwachagulia wazanzibari wa ACT mtu wa kumrithi sefu
 
Kama ZZK ni kibaraka wa Serikali basi amefunzwa vyema na anazidi kuimarika siku hadi siku anaweza kuwa mbadala wa upinzani huko mbeleni kama mazingira yataruhusu tatizo CCM bado ina hazina kubwa sana ya viongozi kuanzia vijana mpaka wazee anaweza ishia kupata madaraka ya kimkakati kama maalim seif tu.
 
Unakumbuka kauli ya kubadili gia angani ilitolewa na nani? Kwa taarifa yako kuamzia kipindi hicho mambo hayajawa rahisi kwa wapinzani na kwamuktadha huo wote wapimzani wote hubadilikabadilika
Umenikumbusha million 50 kila kijiji pamoja na laptop kwa walimu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jussa alikubaliana na SUK. Tena alihojiwa akiwa Nairobi.

Kuhusu kujiunga SUK, Zitto mnamuonea tu, hakuwa na sauti.
Maalim Seif hata kama angekuwa CHADEMA, angejiunga tu na hakuna kitu wangemfanya.

Ishtoshe mimi naona hayakuwa maamuzi mabaya sana kwasababu.

1. Kwanza walishasusa, wakajaribu kupambana bila matunda yoyote. Sana sana CCM wakatumia uwepo wao kupora hata kidogo walichokuwa wamepata.

2. Pili, kwa Seif it was an end of era. Hata kama angekuwepo, asingegombea tena na hata angegombea CCM wangepora tena.
Usnitch unamponza kila muda wananchi wnapojaribu kumuamini.
Nikimuangalia Jussa anavosagika kwenye wheel chair uVP Zanzibar ni kakitu kadogo sana
 
Amemsinitch nani wapi na lini toa mfano
Sisi tuliosoma nae Udsm 1999-2003 tunamjua.Hakuna snitch kama ZZK tanzania hii.Mtoto mbad sana.Hilo tu ndio linamkosesha sifa kwa wanaomjua.Otherwise kwa asiemjua, ZZK atasema kiongozi poa sana.
 
Usnitch unamponza kila muda wananchi wnapojaribu kumuamini.
Nikimuangalia Jussa anavosagika kwenye wheel chair uVP Zanzibar ni kakitu kadogo sana
Hivi hili la u-snitch lina ushahidi au ni siasa tu za majitaka ambazo mara kwa mara zilikuwa zinatokea CHADEMA kila anapotokea mtu wa kutaka kugombea uenyekiti? Na tusisahau, moja ya watu waliokuwa wanaimba sana hizi nyimbo ni Dr. Slaa ambae sasa anakula kuku wa Magu, pamoja na Lema aliyeikimbia vita!
 
Kama ZZK ni kibaraka wa Serikali basi amefunzwa vyema na anazidi kuimarika siku hadi siku anaweza kuwa mbadala wa upinzani huko mbeleni kama mazingira yataruhusu tatizo CCM bado ina hazina kubwa sana ya viongozi kuanzia vijana mpaka wazee anaweza ishia kupata madaraka ya kimkakati kama maalim seif tu.

CCM haina sifa unayojaribu kuipa, nje ya dola ccm ni dhaifu zaidi ya UPDP. Hazina iliyo nayo ya viongozi ccm ni kwa mtindo wa kupeana madaraka kwa mbeleko na kujipendekeza na sio kwa uwezo.
 
CCM inalea vijana na kuwapa miongozo, kila hatua inayopiga kuna mzee au wazee wa kukuweka sawa na kukupa mawaidha. Kitu ambacho ni hadimu sana kwenye upinzani. Na hii sio kwamba CCM ni chama dola au kina hazina ya wazee, ni vyama vya upinzani kushindwa kujenga programu ya kulea vijana. (Kitu ambacho kinarekebishwa.)

Wote kina Kikwete, Magufuli mpaka kina Januari, Polepole nk.. Wakati wa kipindi chao walikuwa na waangalizi au wao wamekuwa waangalizi wa wengine.
CCM ni nyumba ya wajinga. Mtu ambaye ana akili, mkweli wa nafsi yake na siye na unafiki, hawezi kukaa ndani ya CCM. Huwezi kumwona mtu super intlligent ndani ya CCM.

Hata wale wanaoitwa wasomi ndani ya CCM, ukifuatilia ni wale wenye akili ndogo, waliosoma masomo ya wanafunzi dhaifu kwenye masomo. Mtu pekee aliyekuwa na akili kubwa halafu alikuwa CCM ni Dr Bilali.

Waangalie wafuatao:

Kabudi - ni profesa aliye-specialize family law. Kwa wanasheria, hawa ni watu wanaodharaulika. Ni masomo yanayochukuliwa na law minds

Kitila - ni profesa wa saikolojia. Hii ni fani ya IQ law people. Hakuna kitu cha maana zaidi ya hadithi

Bana - huyu mwaka wa kwanza alifeli masomo aliyoyataka. Alipoona yupo kwenye hatari ya kufukuzwa, akaamua kusoma DS. Somo ambalo hkuna mwanafunzi anaweza kushindwa kufaulu, maana ni hadithi tu, hakuna cha maana

Ndugai - nilisoma naye, alijiinga chuo akiwa mtu mzima, sijui alikuwa wapi kabla ya kujiunga UDSM. Huyu alikuwa weak kimasomo. Alipoona anadharaulika na wanafunzi wenzake, akawa anasema kuwa yeye yupo karibu na mzee Malecela, ndiye amemwambia aende akasome ili awe mbunge.

CCM inapendwa na watu wajinga (TWAWEZA).
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom