Leading Without a Title: Zitto Zuberi Kabwe si wa Kubezwa

Leading Without a Title: Zitto Zuberi Kabwe si wa Kubezwa

Status
Not open for further replies.

busar

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,067
Ndugu!

Utangulizi

Nimetafakari sana juu ya Siasa za Tanzania. Nimeangalia kwa upana siasa zetu za Sasa (za kileo). Nikatazama mustakabali wa huko tuendako. Kama tunataka mabadiliko basi TUNAHITAJI WANASIASA VIJANA WAJANJA.

Dhima

Tupate watu wafaao kwa kuangalia waliopo.

Kiini.

Tumempoteza Maalimu Seif. Mwanzo Hizbu, akajakuwa ASP, CCM, CUF, baadae ACT-Wazalendo.

Tunajifunza nini? Jenga Mvuto na Nguvu kwa jamii yako bila kujali ni ndogo kiasi gani. Pemba ilimjenga Maalimu.

Turudi bara kwa Sasa.

Katika wanasiasa wa nje ya CCM naona Zitto ana Nguvu kubwa sana ya kuamua mwelekeo wa Siasa yetu kutokea upinzani.

Kwa sasa lazima ZZK awe sehemu ya mjadala muhimu wa nani anajaza nafasi ya VP Zenji. TISS hawana namna ya kumkwepa. ZZK katika hilo. Anaweza kutaka lolote. Liwe la kifedha, vitu au heshima. Lakini pongezi kwako ZZK. Nitajiunga na ACT Wazalendo.
 
Upvote 5
Mwanasiasa inconsistent na anaebadilika kirahisi sana

Unakumbuka statement ya pamoja baada ya Uchaguzi mkuu ilikuwaje na yeye akafanyaje Zanzibar?
huzijui siasa za zanzibar, kaendelee kuonja porojo za kigogo
 
CCM inalea vijana na kuwapa miongozo, kila hatua inayopiga kuna mzee au wazee wa kukuweka sawa na kukupa mawaidha. Kitu ambacho ni hadimu sana kwenye upinzani. Na hii sio kwamba CCM ni chama dola au kina hazina ya wazee, ni vyama vya upinzani kushindwa kujenga programu ya kulea vijana. (Kitu ambacho kinarekebishwa.)

Wote kina Kikwete, Magufuli mpaka kina Januari, Polepole nk.. Wakati wa kipindi chao walikuwa na waangalizi au wao wamekuwa waangalizi wa wengine.
CCM ingekuwa inatengeneza viongozi isingekuwa inawapa nafasi za juu vijana wanaotoka upinzani na kuwaacha wananchama kindakindaki waliolelewa na chama tangu Chipukizi hadi UVCCM. Kingine wazee wa CCM now hawana sauti kwa vijana na chama chao kwa ujumla, refer suala la Makonda na Mzee Warioba, na mambo mengine mengi yanayoendelea ndani ya chama na serikali kwa ujumla.
 
Una maana makonda nae alilelewa na kupewa muongozo na wazee?

Hyo unayoizungumzia ni CCM ya zamani, CCM ya sasa kila mtu ana sharubu

Now kuwa chawa kunakupa access ya fasta kupata teuzi hta km hujapitia mifumo rasmi ya chama iliyojiwekea.
 
........ Na hii sio kwamba CCM ni chama dola au kina hazina ya wazee, ni vyama vya upinzani kushindwa kujenga programu ya kulea vijana. (Kitu ambacho kinarekebishwa.)
Mkuu Sidhani kama ni hii kweli, maana kuna crop ya vijana wa CHADEMA imetapakaa kwenye post za serikali nikiamini hta CCM iliona potential yao.

Vijana kma Kafulila,Shonza,Silinde,Mnyika,Zitto,Mdee,Machali, Nassari n.k walipikwa sana enzi hizo na kina Dr slaa-Mbowe.

Changamoto iliyopo upinzani ni succession plan tu ila sio kwamba hailei vijana. Walau CCM ina dola kwa hyo ni rahisi kuwapa vyeo na experience vijana wao kupitia fursa serikalini kuonyesha uwezo wao.

Apart from that naamini hakuna chama hasa upinzani imeweza kutoa vijana wengi kwenye siasa tena wenye ushawishi kma CHADEMA. Na hii ni credit kwa Mbowe aliyeanzisha BAVICHA na BAWACHA imara
 
Jussa alikubaliana na SUK. Tena alihojiwa akiwa Nairobi.

Kuhusu kujiunga SUK, Zitto mnamuonea tu, hakuwa na sauti.
Maalim Seif hata kama angekuwa CHADEMA, angejiunga tu na hakuna kitu wangemfanya.

Ishtoshe mimi naona hayakuwa maamuzi mabaya sana kwasababu.

1. Kwanza walishasusa, wakajaribu kupambana bila matunda yoyote. Sana sana CCM wakatumia uwepo wao kupora hata kidogo walichokuwa wamepata.

2. Pili, kwa Seif it was an end of era. Hata kama angekuwepo, asingegombea tena na hata angegombea CCM wangepora tena.

Tatizo kubwa la hawa vijana humu mitandaoni ni kuwa ueleo wao wa siasa ni mdogo na hasa za Zanzibar.

Maalim amekua akishinda chaguzi zote since 1995, ameshatumia kila mbinu kwenye mapambano, yeye anayafahamu mengi kulikohawa keyboard warriors humu JF na kule Twiter.
Maamuzi ya kujiunga na SUK yalikua ni sahihi, mwanzo nilikua na shaka nayo na pia jazba nilikua nayo ila niliamini kutoka moyoni kuwa Maalim alikua yupo kwenye njia sahihi, mana ameshani prove wrong mara nyingi tu huko nyuma. Sasa matunda yameanza kuonekana japo bado ni mapema.
Na suala la kujiunga lilikua tayati liko planed hayakua maamuzi ya kukurupuka cha kilashakua na plane kwa kila matokeo yatakavyokuja, Na ZZK hawezi kuwa na kauli kwenye hilo.
 
Huzijui siasa za Zanzibar
Ni Mazrui au Duni Haji na genge lao ndio watakaoamua Nani awe Makumu wa kwanza wa Rais,Zitto hana ubavu wa kuwachagulia wazanzibari wa ACT mtu wa kumrithi sefu

Hao hawaelewi kitu, Mazurui ndio mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa Zanzibar. Yeye ndie atakaeamua nani awe makamu wa kwanza.
 
CCM inalea vijana na kuwapa miongozo, kila hatua inayopiga kuna mzee au wazee wa kukuweka sawa na kukupa mawaidha. Kitu ambacho ni hadimu sana kwenye upinzani. Na hii sio kwamba CCM ni chama dola au kina hazina ya wazee, ni vyama vya upinzani kushindwa kujenga programu ya kulea vijana. (Kitu ambacho kinarekebishwa.)

Wote kina Kikwete, Magufuli mpaka kina Januari, Polepole nk.. Wakati wa kipindi chao walikuwa na waangalizi au wao wamekuwa waangalizi wa wengine.
Hapa unazungumzia ccm ya mwalimu Nyerere.
 
Mkuu Sidhani kama ni hii kweli, maana kuna crop ya vijana wa CHADEMA imetapakaa kwenye post za serikali nikiamini hta CCM iliona potential yao.

Vijana kma Kafulila,Shonza,Silinde,Mnyika,Zitto,Mdee,Machali, Nassari n.k walipikwa sana enzi hizo na kina Dr slaa-Mbowe.

Changamoto iliyopo upinzani ni succession plan tu ila sio kwamba hailei vijana. Walau CCM ina dola kwa hyo ni rahisi kuwapa vyeo na experience vijana wao kupitia fursa serikalini kuonyesha uwezo wao.

Apart from that naamini hakuna chama hasa upinzani imeweza kutoa vijana wengi kwenye siasa tena wenye ushawishi kma CHADEMA. Na hii ni credit kwa Mbowe aliyeanzisha BAVICHA na BAWACHA imara
You're right, kwamba kuna vijana wanatoka upinzani na kujiunga CCM na kuwa viongozi. Lakini kuna tofauti kati ya kuwa kiongozi wa kichama eg. John Myika na kuwa kiongozi wa kiserikali kama Mwita Waitara. Misingi na kanuni zinazowaongoza ni tofauti.

Lakini nikirudi nyuma na kuangalia kwa undani kwanini hawa vijana wanakimbia upinzani, umesema kuwa CCM ina resources za kutoa ajira. Mimi napingana nalo, kwasababu hawa vijana wengi wametoka upinzani out of frustration. Na yote hii inatokana na vyama either kushindwa kutatua migogoro yao ndani, au kukosa utaratibu wa kutatua matatizo ya vijana ndani ya chama.

Vijana by nature ni watu curious, kila mara watakuwa na maswali ambayo yanataka majibu. Hata CCM kuna vijana wanakuwa frustrated, lakini kabla kijana hajafika hatua ya kutoka nje ya mstari, atakutana na hazina kubwa ya wazee ambao wanaweza either kumpa majibu yanayostahiki au hata kutatua tatizo lote kwa ujumla. Chukulia yanayotokea kwa wabunge wa viti maalum Chadema, chama kikuu kina msimamo wake ambao kwa mtazamo wangu ni wa kibinafsi, huku wabunge ambao wengi ni vijana wanapingana nao na kuona kama wanaonewa. Kama kungekuwa na utaratibu wa kuzuia moto panapofuka moshi, hili swala lisingefika lilipofika sasa. Vyama vya upinzani vimefanikiwa kupata vijana wabichi kujiunga navyo, lakini hiyo ni nusu ya hadithi, vijana wengi wakishaingia wanakutana na vikumbo na matatizo yanayo wakatisha tamaa, na mojawapo ni matumizi mabaya ya fedha. Wakijaribu kuandaa programu zao, unakuta fedha inakuwa kigugumizi kutoka makao makuu. Kwahiyo sio swala moja la kupata vijana wa kujiunga na chama, ni pamoja na kuwalea kwa utaratumibu ulio wazi na kujibu hoja zao pamoja kwa wakati. CCM ni muajiri mkubwa wa vijana hapa nchini, kuanzia wanasheria, wahasibu, watafiti na waandaaji wa sera nk. Hawa sio watu unaona majina yao magazeti au mitandaoni, lakini wapo nyuma ya pazia. Na ndio maana hata wakati wa uchaguzi, kulikua hakuna shida ya wanasheria wa kuhakiki fomu za watia nia.
 
CCM ingekuwa inatengeneza viongozi isingekuwa inawapa nafasi za juu vijana wanaotoka upinzani na kuwaacha wananchama kindakindaki waliolelewa na chama tangu Chipukizi hadi UVCCM. Kingine wazee wa CCM now hawana sauti kwa vijana na chama chao kwa ujumla, refer suala la Makonda na Mzee Warioba, na mambo mengine mengi yanayoendelea ndani ya chama na serikali kwa ujumla.
Kuna elimu ya shule na kuna elimu ya ulimwengu, ukisoma vizuri post yangu nimesema CCM ni chama kinacholea vijana na kuwapa misingi mizuri ya uongozi. Ndani ya CCM kuna hazina kubwa ya wazee na walezi wa kukurudisha kwenye misingi ya uwadilifu. Mzazi wako anaweza kukupa mafunzo ambayo hakuna vitabu vya shuleni vinaweza kukupa.

Hata hivyo nikija kwenye hoja yako ya viongozi wengi wa CCM ni incompetence, je unaweza kutuhakishia kwamba vyama vya upinzani wao wamechukuwa top cream the country can offer?

Tanzania ni nchi yenye watu wenye uwezo wa aina mbalimbali, kuna wenye akili za kuchanganua mambo haraka na wengine wanachukua muda kupata matoke. Swala sio nami ana akili za haraka, swala ni kuwa na mwalimu anayeelewa uwezo wako na kukupa muda wa wewe kuelewa. Kama mwanafunzi mmoja anachukiwa dakika moja kupata jibu na mwingine anachukiwa dakika kumi, wote mwisho wa siku watapata majibu sawa. Vyama vya upinzani kwasababu wana haraka ya kupata matokeo na hawana resources za kumshika kila mtu mkono, ndio maana wanapita njia za mkato na kupuuzia wale ambao sio wakimbiaji na wanaharakati kama wengine.
 
You're right, kwamba kuna vijana wanatoka upinzani na kujiunga CCM na kuwa viongozi. Lakini kuna tofauti kati ya kuwa kiongozi wa kichama eg. John Myika na kuwa kiongozi wa kiserikali kama Mwita Waitara. Misingi na kanuni zinazowaongoza ni tofauti.

Lakini nikirudi nyuma na kuangalia kwa undani kwanini hawa vijana wanakimbia upinzani, umesema kuwa CCM ina resources za kutoa ajira. Mimi napingana nalo, kwasababu hawa vijana wengi wametoka upinzani out of frustration. Na yote hii inatokana na vyama either kushindwa kutatua migogoro yao ndani, au kukosa utaratibu wa kutafuta matatizo ya vijana ndani ya chama.

Vijana by nature ni watu curious, kila mara watakuwa na maswali ambayo yanataka majibu. Hata CCM kuna vijana wanakuwa frustrated, lakini kabla kijana hajafika hatua ya kutoka nje ya mstari, atakutana na hazina kubwa ya wazee ambao wanaweza either kumpa majibu yanayostahiki au hata kutatua tatizo lote kwa ujumla. Chukulia yanayotokea kwa wabunge wa viti maalum Chadema, chama kikuu kina msimamo wake ambao kwa mtazamo wangu ni wa kibinafsi, huku wabunge ambao wengi ni vijana wanapingana nao na kuona kama wanaonewa. Kama kungekuwa na utaratibu wa kuzuia moto panapofuka moshi, hili swala lisingefika lilipofika sasa. Vyama vya upinzani vimefanikiwa kupata vijana wabichi kujiunga navyo, lakini hiyo ni nusu ya hadithi, vijana wengi wakishaingia wanakutana na vikumbo na matatizo yanayo wakatisha tamaa, na mojawapo ni matumizi mabaya ya fedha. Wakijaribu kuandaa programu zao, unakuta fedha inakuwa kigugumizi kutoka makao makuu. Kwahiyo sio swala moja la kupata vijana wa kujiunga na chama, ni pamoja na kuwalea kwa utaratumibu ulio wazi na kujibu hoja zao pamoja kwa wakati. CCM ni muajiri mkubwa wa vijana hapa nchini, kuanzia wanasheria, wahasibu, watafiti na waandaaji wa sera nk. Hawa sio watu unaona majina yao magazeti au mitandaoni, lakini wapo nyuma ya pazia. Na ndio maana hata wakati wa uchaguzi, kukiwa hakuna shida ya wanasheria wa kuhakiki fomu za watia nia.

..kijana wa ccm akiwa-frustrated anapewa nafasi ya uteuzi.

..kijana wa upinzani akiwa frustrated Mbowe au Zitto hawana kitu cha kuwapa.

..vilevile ccm has tons of money, zinawatosha kufuja, na zikabaki za kujenga chama na kuwalainisha vijana wao.

..vijana wanaohama upinzani ni kwamba wamekata tamaa kama wanaweza kuzishinda dhuluma na fitina za ccm.
 
Naona CCM angekua neutralized kma Nape,Kafulila,Bashe, au Filikunjombe Yaani makali yasingeonekana.

Mara zote naamini kma angebaki CHADEMA akiwa na uvumilivu kma Mnyika then leo hii angekua mwenyekiti.

Kupitia uenyekiti CHADEMA angekua na nguvu sana na influence kuliko hata Peak-Dr Slaa otherwise mabadiliko ya katiba yakiwa agenda ya kudumu ya upinzani then ''kufika mbali'' kutakuwa more realistic kwa pande zote za kisiasa.

..nadhani kipindi kile rafiki zake wazee wa ccm walimponza.

..alianza kuwa karibu na watu wa ccm kuliko wakubwa zake ndani ya chadema.

..kwa upande mwingine Zitto is a moderate politician, na Chadema wakati ule radicals ndio waliokuwa wameshika hatamu.

..sasa hivi nadhani hali ni tete sana, hakuna mwenye uhakika wa muelekeo ambao ACT Zanzibar itachukua baada ya kifo cha Maalim Seif.
 
..kijana wa ccm akiwa-frustrated anapewa nafasi ya uteuzi.

..kijana wa upinzani akiwa frustrated Mbowe au Zitto hawana kitu cha kuwapa.

..vilevile ccm has tons of money, zinawatosha kufuja, na zikabaki za kujenga chama na kuwalainisha vijana wao.

..vijana wanaohama upinzani ni kwamba wamekata tamaa kama wanaweza kuzishinda dhuluma na fitina za ccm.

Haha, haya ni majibu mepesi kwa hoja nzito ya vyama vya upinzani. Leo hii tungeona kina Nape, Januari etc wamepachikwa makazi ya ajabu ajabu kama hoja yako ingekuwa na kweli.

Vijana kama kina Zitto wamekutana na upanga ambao umekuwa unashikiliwa na uongozi wa chama tokea Mbowe took the helm. Wabunge 19 hivi sasa wako kwenye meza ya machinjioni kutokana na misimamo ya chama ya upanga kwa upanga. Hii sio kwamba CCM ina fedha nyingi au uwezo wa kuwapachika vijana serikali. Chama kama CDM kemegeuzwa kuwa kambi ya mapambano badala ya kuwa chama cha kisiasa. Kila kitu ni kususa, kufanya maadamano, kufukuza bila kusikilizwa. Kwa kifupi sio vijana wote wakubaliane na mwelekeo huo wa chama. Leo ACT-Zanzibar imejiunga na CCM-Zanzibar unaona vile wana CDM wanasema wamesalitiwa kama vile CDM ndio walikuwa na ubia wa mwelekeo wa ACT. Kama CDM ingekuwa inafanya siasa na wao wangekuwa na jinsi ya kutengeneza deal na chama kingine including CCM. It comes down to politics rather than militant approach.
 
..hata ccm kuna upanga kama mhusika hatakuwa mtiifu kwa mwenyekiti.

..zaidi, haiwezekani vyama vyote viwe na mtizamo na misimamo sawa kuhusu uchaguzi wa 2020.

..suala la "wabunge" 19 lilipaswa kujadiliwa ktk chama ili kiwape baraka kwenda bungeni.
 
CCM haina sifa unayojaribu kuipa, nje ya dola ccm ni dhaifu zaidi ya UPDP. Hazina iliyo nayo ya viongozi ccm ni kwa mtindo wa kupeana madaraka kwa mbeleko na kujipendekeza na sio kwa uwezo.
Kuwa serious kidogo sio kila mda utani CCM chama kikubwa na kikongwe Africa. Na ina utaratibu mzuri wa demokrasia nchi nyingi za Africa wameshindwa kufanya ameishia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
 
Haha, haya ni majibu mepesi kwa hoja nzito ya vyama vya upinzani. Leo hii tungeona kina Nape, Januari etc wamepachikwa makazi ya ajabu ajabu kama hoja yako ingekuwa na kweli.

Vijana kama kina Zitto wamekutana na upanga ambao umekuwa unashikiliwa na uongozi wa chama tokea Mbowe took the helm. Wabunge 19 hivi sasa wako kwenye meza ya machinjioni kutokana na misimamo ya chama ya upanga kwa upanga. Hii sio kwamba CCM ina fedha nyingi au uwezo wa kuwapachika vijana serikali. Chama kama CDM kemegeuzwa kuwa kambi ya mapambano badala ya kuwa chama cha kisiasa. Kila kitu ni kususa, kufanya maadamano, kufukuza bila kusikilizwa. Kwa kifupi sio vijana wote wakubaliane na mwelekeo huo wa chama. Leo ACT-Zanzibar imejiunga na CCM-Zanzibar unaona vile wana CDM wanasema wamesalitiwa kama vile CDM ndio walikuwa na ubia wa mwelekeo wa ACT. Kama CDM ingekuwa inafanya siasa na wao wangekuwa na jinsi ya kutengeneza deal na chama kingine including CCM. It comes down to politics rather than militant approach.
Una Akili sana wewe! Asante
 
Kuwa serious kidogo sio kila mda utani CCM chama kikubwa na kikongwe Africa. Na ina utaratibu mzuri wa demokrasia nchi nyingi za Africa wameshindwa kufanya ameishia kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Chama kikongwe kilicho madarakani kwa kunajisi uchaguzi?
 
Daah! Nilikuwa namuwazia huyu kuwa ndiye atakitwaa kiti cha Maalim, sasa kama hali yake bado basi Mazurui atachukua.
Mazrui hawezi kuteuliwa kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hana sifa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom