Leading Without a Title: Zitto Zuberi Kabwe si wa Kubezwa

Leading Without a Title: Zitto Zuberi Kabwe si wa Kubezwa

Status
Not open for further replies.

busar

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,067
Ndugu!

Utangulizi

Nimetafakari sana juu ya Siasa za Tanzania. Nimeangalia kwa upana siasa zetu za Sasa (za kileo). Nikatazama mustakabali wa huko tuendako. Kama tunataka mabadiliko basi TUNAHITAJI WANASIASA VIJANA WAJANJA.

Dhima

Tupate watu wafaao kwa kuangalia waliopo.

Kiini.

Tumempoteza Maalimu Seif. Mwanzo Hizbu, akajakuwa ASP, CCM, CUF, baadae ACT-Wazalendo.

Tunajifunza nini? Jenga Mvuto na Nguvu kwa jamii yako bila kujali ni ndogo kiasi gani. Pemba ilimjenga Maalimu.

Turudi bara kwa Sasa.

Katika wanasiasa wa nje ya CCM naona Zitto ana Nguvu kubwa sana ya kuamua mwelekeo wa Siasa yetu kutokea upinzani.

Kwa sasa lazima ZZK awe sehemu ya mjadala muhimu wa nani anajaza nafasi ya VP Zenji. TISS hawana namna ya kumkwepa. ZZK katika hilo. Anaweza kutaka lolote. Liwe la kifedha, vitu au heshima. Lakini pongezi kwako ZZK. Nitajiunga na ACT Wazalendo.
 
Upvote 5
Naona CCM angekua neutralized kma Nape,Kafulila,Bashe, au Filikunjombe Yaani makali yasingeonekana.

Mara zote naamini kma angebaki CHADEMA akiwa na uvumilivu kma Mnyika then leo hii angekua mwenyekiti.

Kupitia uenyekiti CHADEMA angekua na nguvu sana na influence kuliko hata Peak-Dr Slaa otherwise mabadiliko ya katiba yakiwa agenda ya kudumu ya upinzani then ''kufika mbali'' kutakuwa more realistic kwa pande zote za kisiasa.
Na hapo ndipo alipozika career yake kwa kiwango kikubwa sana.

Sasa hivi amebaki kuwa busy body tu asiye na madhara yoyote kwa watawala no wonder hawahangaiki nae tena.

Mpaka sasa Lissu ana influence kubwa kuliko Zito.
 
CCM inalea vijana na kuwapa miongozo, kila hatua inayopiga kuna mzee au wazee wa kukuweka sawa na kukupa mawaidha. Kitu ambacho ni hadimu sana kwenye upinzani. Na hii sio kwamba CCM ni chama dola au kina hazina ya wazee, ni vyama vya upinzani kushindwa kujenga programu ya kulea vijana. (Kitu ambacho kinarekebishwa.)

Wote kina Kikwete, Magufuli mpaka kina Januari, Polepole nk.. Wakati wa kipindi chao walikuwa na waangalizi au wao wamekuwa waangalizi wa wengine.
Programme ya kuandaa wezi ?

Mbona kila kijana anayehama kutoka upinzani anapewa na cheo wengine mpaka uwaziri.?

Sema wananufaika na ccm kuwa chama dola hakuna cha uangalizi huko.

Kama ccm ina programme nzuri za kuandaa vijana mbona wananunua vijana wengi kutoka upinzani ?
 
Una maana makonda nae alilelewa na kupewa muongozo na wazee?

Hyo unayoizungumzia ni CCM ya zamani, CCM ya sasa kila mtu ana sharubu

Now kuwa chawa kunakupa access ya fasta kupata teuzi hta km hujapitia mifumo rasmi ya chama iliyojiwekea.
Kwanza atambue kwa sasa ccm siyo chama cha siasa tena ni genge la wahuni.
 
Na hapo ndipo alipozika career yake kwa kiwango kikubwa sana.

Sasa hivi amebaki kuwa busy body tu asiye na madhara yoyote kwa watawala no wonder hawahangaiki nae tena.

Mpaka sasa Lissu ana influence kubwa kuliko Zito.
Lkn anaongoza chama kilichotoa

kisichMakamu Rais Zenji.

Hatuoni Kama ananguvu kisiasa?
 
Lkn anaongoza chama kilichotoa

kisichMakamu Rais Zenji.

Hatuoni Kama ananguvu kisiasa?

Wazanzibari hasa wapemba wana tabia moja ambayo haibadiliki hata wakienda chama gani kiwe CUF au ACT.

Mosi hawana connection ya moja kwa moja na waTanganyika.

Pili wakiwemo katika Chama chochote ajenda yao ni moja upemba kwanza na baadae uzanzibar.

Tatu kiongozi yoyote mwenye nguvu kutokea Tanganyika watahakikisha wanamdhoufisha na ikiwezekana watamfukuza na kukifanya chama mali ya wapemba zaidi kuliko uTanzania.

Mwisho muelekeo wa ACT baada ya Maalim utategemea zaidi waPemba waliosalia na hatima ya Zitto nafikiri inaelekea mwisho kisiasa katika siasa zijazo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom