Leeds United: Nyota iliyozimika katika ulimwengu wa soka

Kutoka nusu fainali ya Uefa Champions League mwaka 2001, mpaka kushuka daraja mwaka 2003 na kupotea katika ramani ya soka la Uingereza, wale wapenzi wa soka wa kitambo, Unaikumbuka Leeds United hii?
Waliosimama kuanzia kushoto ni Mark Viduka, Danny Mills "kipara", Rio Ferdinand aliyevaa kitambaa cha unahodha na bila kumsahau beki Iane Harte bora wa kupiga mipira iliyokufa katika EPL baada ya zama za Denis Irwin.

Waliochuchumaa kuna kijana mtukutu Alan Smith, kuna mbabe Lee Bowyer, Oliver Dacourt na wa mwisho ni Harry Kewell.

Hapo kikosini wanakosekana Majemedari kama Lucas Radebe, Robbie Keane na wengineo.

Uwanja wao wa " ELLAND ROAD " ulikuwa mgumu sana kwa sisi Man Utd.

cc Guasa Amboni
 
Kuna kipindi walishuka hadi daraja la pili, pia timu ilikumbwa na ukata mpaka wakajaribu kuuza uwanja wao!
Kwa kifupi toka washuke daraja wamepita kwenye vipindi vigumu sana! Ni kama Portsmouth ilivyo dhofu ile hali kwasasa!
 
[emoji106]mkuu
 
Kutoka nusu fainali ya Uefa Champions League mwaka 2001, mpaka kushuka daraja mwaka 2003 na kupotea katika ramani ya soka la Uingereza, wale wapenzi wa soka wa kitambo, Unaikumbuka Leeds United hii?
Liverpool inaelekea huko huko.
 
League One ya China una maanisha?
 
Timu yangu west ham vipi
West ham au wapiga nyundo wa London/ hammers walijitahidi sana kipindi cha 2004/ 05 kwa kuwanunua Javier mascharano na Carlos tevez lakini waliwauza pia kutokana na uchumi wao ulishindwa kuwalipa, nafikiri msimu huu bado hamko vizuri sana kikosi kimekosa morali sana nafikiri mtendaji wenu sullivan ataangalia ni kocha gani anaweza mreplace slaven bilic maana jahazi litazama wasipokuwa makini
 
Kutoka nusu fainali ya Uefa Champions League mwaka 2001, mpaka kushuka daraja mwaka 2003 na kupotea katika ramani ya soka la Uingereza, wale wapenzi wa soka wa kitambo, Unaikumbuka Leeds United hii?
daah hili chama ninalizimikia mpaka leo, sijui nini kimelikumba hili chama.. Mark Viduka, Lee Bowyer, Harry kewel, Rio Ferdinand, Lucas Radebe na mtukutu Allan Smith
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…