Legacy kuu za Mwalimu Nyerere: Mwiba mkali kooni mwa Watanganyika

Mtakubaliana na Tundu Lissu kuhusu chanzo kikuu cha tatizo kama alivyoainisha kwenye hotuba yake kwenye Bunge la Katiba ?​
Nyerere alitengeneza muungano wa ajabu sana.
Unaweza kushangaa kwanini alitoa zaidi haki ya watanganyika kwa wazanzibar?
Alizidiwa akili na Abeid Karume ambaye hakuwa msomi kama yeye?
Karume hakuwa na exposure kama aliyopata Nyerere kule Edinburgh.
Karume hakupitia hatua ya kupata uzoefu wa uongozi mkubwa serikalini kabla ya mapinduzi.
Nyerere alikuwa waziri mkuu kwanza kabla ya uraisi.
 
Ndivyo alivyokuwa Mzee Nyerere anatenda kwanza halafu anajutia baadaye.

Hata mwaka 1993-1996 alipoonywa na kina Kolimba kuhusu ukweli wa CCM hakusikia.

Akavuruga uchaguzi ndani ya CCM na nchi halafu baadaye akataka amtoea Mzee Mkapa.

Hivi unadhani watu watamuelewa mtu wa aina hii kweli, ambaye alituaminisha Mzee Mkapa ni mtu msafi na anafaa kuwa Raisi lakini baadaye anaanza kulalamika kwamba Mkapa hafai. UKWELI aliambiwa lakini hakutaka kusikia, akawahujumu watu ndani na nje ya chama.

Kina Kombe, Kolimba, Babu, Kambona yaliwakuta makubwa kwasababu walionesha kushindana na EGO ya Mzee Nyerere, wala siyo usaliti wa chama au taifa. Ni EGO tu.
=====================================================

Ukianza kufuatilia hata yaliyokuwa yanaendelea kwenye ukanda huu unaanza kupata wasiwasi na akili za Mzee Nyerere na malengo yake. Aliingiza Tanzania kwenye VITA YA KAGERA ili kumrudisha swahiba wake Milton Obote. Vita ambayo kiuhalisia ilikuwa inaepukika kwasababu kulikuwa na madikteta wabaya ukanda huu kuliko Iddi Amini.

Nchi imefilisika, baadaye akagombana na Obote akaanza kumuunga mkono Museveni. Sasa unakaa unajiuliza lengo lake huyu lilikuwa ni lipi haswaa, hupati majawabu. Anafanya maamuzi ya haraka halafu baadaye anageuka anaanza kulazimisha jambo jingine.

Kule Rwanda ndiyo hatutazungumzia, lakini yale madudu yote ya 1990's Mzee Nyerere alihusika mno. Sema tu hatuwezi kuyasema waziwazi hapa. Ila ukweli mchungu ni kwamba Nyerere has left behind a trail of blood and mayhem.
​
 
Ila 1995 asingefanya hiyo vurugu huoni huenda tungepata mapema zaidi yaliyo tupata 2005-2015, 2015-2021, kisha kilele chake haya ya 2021-2025(MO29)?
 
Ila 1995 asingefanya hiyo vurugu huoni huenda tungepata mapema zaidi yaliyo tupata 2005-2015, 2015-2021, kisha kilele chake haya ya 2021-2025(MO29)?
Asingevurga mchakata CCM ingekuwa kama KANU, (HISTORIA).

Hii KATIBA ingekuwa ishawekwa kwenye chumba cha KUMBUKUMBU.

Miaka ya 90's mbali na uchumi kuwa mbovu, Tanzania ilikuwa na hali nzuri sana kisiasa kuliko mataifa mengi ya Afrika. Watu walikuwa bado wanaaminiana. Upinzani wote ambao Mzee Nyerere aliwaita mbwa, waliwahi kushika nafasi kubwa za kisiasa hapa nchini na wakafanya vizuri tu. NCCR-Mageuzi ilikuwa na Naibu Waziri Mkuu, CUF ilikuwa na Waziri wa Fedha na Uchumi, CHADEMA ilikuwa na Gavana wa Fedha. Hizo vurugu zingetokea wapi kama tungesimamia demokrasia ???
​
 
Japo tunajifunza kupitia historia, in my view! Nyie wasomi ndio tatizo la haya yote, na hasa nyie wasomi wa kipindi cha mwalimu hadi miaka ya 90s.

Malcom huwa najifunza mengi sana kupitia maandiko yako, lakini Kuna namna hata nyie kizazi chenu ni hasara, tena nyie ndio source ya haya yote, kwakuwa yameanzia wakati wenu.

Mmebaki kulaum Gen Z wachukue hatua! Nyie wakati wenu mlifanya nini, mbona hamkuchukua hatua?

By the way, tunataka reform ya Nchi! Ukiangalia wahusika ni kizazi chako ndicho asilimi 80 wameshika nafasi muhimu za maamuzi.

Tukubali! Mabadiliko yatakuja, lakini mpaka hii asilimi 80 (mindset hii) wapungue walau wabaki asilimia 20.

Watu mnatumia nguvu sana kuandika wakati mnajua fika hayo mambo hayawezekani kwa sasa kwa sababu anuai, zikiwemo lliteracy na poverty, etc.
 
Mtakubaliana na Tundu Lissu kuhusu chanzo kikuu cha tatizo kama alivyoainisha kwenye hotuba yake kwenye Bunge la Katiba ?​
Polepole alisema huu Muungano una maslah binafsi ndan yske. Na kuugusa kwa namna yoyote ile ni kuleta mgogoro wa kimaslah miongon mwa wanufaika. Nina wasiwas sehem kubwa ya bajet ya muungano kwenda zanzibar inaingia mifukon mwa watu ndo mana wanaushikilia.

Mana hata kuwa rais wa Muungano kupitia ccm lazima uamini katika muungano kwanza ndo upite
 
Nakubaliana nawe kwa asilimia 1000% bila kupinga chochote.

Ili Tanzania isonge mbele kile kizazi cha kuanzia 1955-1989 inabidi kipukutike chote.
​
 
Mwaka jana kikwete alimpitisha sami kwa njia ambazo watu wengi waliulalamikia lakini watu wengi hawajui zile ndo njia Nyerere alikuwa anazitumia wakati akiwa mwenyekiti

Kikwete alitumia njia za mentor wake Nyerere

Nyerere alikuwa kutwa kulalamika katiba mbovu inampa mamlaka makubwa Rais cha ajabu kwenye amendment zote za katiba chini yake hakuwa kuaddress hili tatizo la kuwa na mamlaka makubwa

Na Nyerere alikipenda chama kuliko nchi alihakikisha ccm kinakuwa chama dola hata baada ya kuja kwa vyama vingi kitu ambacho kinaitesa nchi mpaka leo unapokimilikisha chama viwanja na majengo ni ujinga wa kiwango kikubwa sana
 
Nguruvi3 Mkandara zitto junior
 
NJIA KUU ya kutatua tatizo lolote lile kwenye maisha ni kukubali UKWELI hata kama ni mchungu
MALCOM LUMUMBA

Swali :Ungekuwa wewe ndiyo Nyerere, West (America) vs USSR wapo mlangoni mwako na wanaitaka Zanzibar iwe battle field yao, ungechukua uamuzi gani??

MALCOM LUMUMBA

Ukweli: West vs USSR pressure yao ilimchanganya Nyerere na timu yake, na hata wewe ungechanganyikiwa.

MALCOM LUMUMBA

Najua unafahamu kuwa dunia inaongozwa na picha kuu mbili ambazo ni :

1) Picha ya nje ( Hii huwa ni ya uongo)

2) Picha ya ndani ( Huwa ndiyo ukweli wenyewe ambao hujulikana na watu wachache)

MALCOM LUMUMBA

Ukweli: Nyerere alikuwa ni binadamu na siyo malaika, mapungufu ni sehemu ya ubinadamu wake.

MALCOM LUMUMBA

Naongezea ukweli na uwajibikaji unaotokana na huo ukweli ndiyo tatizo kuu kwa sasa hapa nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…