ENIWEI sijui kama tutaelewana......
Ni ujinga mtupu!
Nimesoma hayo ya Nyerere; hayo mengine sijui kuna uchafu gani huko.
Kuhusu hayo ya Nyerere; wewe mwenyewe umekwisha kubali kwamba mabadiliko hutokea na wakati; lakini humo humo unakaza shingo na hayo ya Nyerere!
Kuna mahali popote aliposema yabaki hivyo milele?
Hayo unayolalamikia, yalipokuwa yanatengenezwa, kuliwekwa maagizo yasibadilishwe?
Unapozungumzia hayo ya Nyerere kwa kupindisha kukidhi hoja zako, bado unataka watu waamini ujinga?
Kwa mfano: huo muungano unaotumia hapa, unao ujasiri wa kusimama na kusema huu uliopo ndio uleule ulioasisiwa?. Huna akiliza kujuwa kwamba mambo mengi yamebadilishwa na kuwa kinyume kabisa na ilivyotazamiwa?
Ni sehemu gani ya utawala wa Nyerere inayoelekeza uongozi wa nchi utakuwa ni wa kupokezana kidini?
Jambo la kipuuzi kama hili nalo unaleta kuwa kielelezo cha kuonyesha lawama na kushindwa kuelewa kuwa swala kama hili limetumiwa tu na wahuni wasiokuwa na sifa za kusimama kama viongozi!
Hili swala la kidini lilikuwepo toka enzi za kutafuta uhuru; na ndiko chimbuko la ulalamishi mwingi hadi walipofikia sasa na kudai kupokezana. Hakuna mahali popote Nyerere alipozungumzia swala la kupokezana, wewe leo hii unaliibua na kumwangushia yeye!
Mifano yote uliyoiweka hapo ili kuhalalisha hoja zako zote umezitumia kwa kupindisha.
Huwezi kuzungumzia katiba ya enzi za chama kimoja wakati unajuwa nyakati zilikwisha badilika.
Kama iliwezekana kuwepo na vyama vingi, ni huyo huyo Nyerere aliyekataza katiba isibadilishwe kuendana na wakati wa vyama vingi?
Kwa kifupi ni kwamba mada yako yote ni takataka tu kwa sababu misingi yake umeizamisha kwenye upotofu.
Samia anang'ang'ania kukaa madarakani kwa nguvu, hadi kuua waTanzania, tatizo linabaki kwa huyo huyo Nyerere. Hii ni akili ya wapi hii!