Legacy kuu za Mwalimu Nyerere: Mwiba mkali kooni mwa Watanganyika

Legacy kuu za Mwalimu Nyerere: Mwiba mkali kooni mwa Watanganyika

Kwa hiyo tuendelee kulalamika/kumlalamikia marehemu au tutafute njia bora kujinasua?
Marehemu halalamikiwi, kinachofanyika hapa ni kuonesha tatizo lilianzia wapi jambo ambalo Boomers, Gen-X na Millennials (A.K.A Mizigo ya Taifa) haitaki kukubali. Mzee Nyalali na Mzee Warioba walionesha matatizo yako wapi lakini hatua hazikuchukuliwa na vizazi vilivyopita. Kinachokera ni kwamba MIZIGO YA TAIFA ndiyo wamekuwa vinara wa kulalamikia serikali ya CCM ilhali hawautaki ukweli.

Unajua MUNGU alivyomwambia Nabii Mussa kwamba kile kizazi kilichotokea Misri kitafia chote jangwana kwasababu kingeingia nchi ya ahadi na zile akili za kitumwa, ambazo wanachukia kweli Misri lakini wanapenda NYAMA, MATIKITI na VITUU SWAUMU vya Misri kiasi cha kutaka kurudi utumwani walipoona matatizo. MUNGU akaamua kukifyekelea mbali kabisa kwa miaka arobaini (40) jangwani, watoto wao ambao hawakuzaliwa utumwani ndiyo wakaingia nchi ya ahadi.

Kiufupi, kwa akili (Mindset) za akina watanganyika wa sasa, ni ngumu nchi kupata maendeleo hata kama CCM watatoka. Watanganyika, are victims of their own poisonous propaganda. And most importantly, they lack discernment and hate the TRUTH.
​
 
Ewaaah !
Sio sahihi! Nadhani umetumia maneno makali zaidi kuchangia mada hii.

Unaposema alikuwa anatumiwa, niambie yeye alinufaika na nini katika kutumiwa kwake,? Maana hakuwa na Utajiri wa kujilimbikizia mali! zaidi wakati wake hakukuwa na exploitation kubwa ya natural resource! Na ni yeye alizuia exploitation mpaka tutakapo jitambua!

Please pamoja na andiko Bora kabisa la Malcom, walau tuwe na heshima kwa Mwalimu, ni wajibu wetu sisi kusahihisha mapungufu yake na sio kumdhihaki Kwa KAZI kubwa aliyofanya kufikisha Taifa hapa.

Kwanini usilaum kizazi cha wakati huo, tena akiwemo Malcom ambaye anaonekana kabisa kwa ufahamu wake, ni tunda la utawala wa Mwalimu??

Infact, pamoja na mapungufu tunayo yajadili, ni dhahiri alionesha kuwajali watanzania wote.
Sahihi kabisa ✅
 
Marehemu halalamikiwi, kinachofanyika hapa ni kuonesha tatizo lilianzia wapi jambo ambalo Boomers, Gen-X na Millennials (A.K.A Mizigo ya Taifa) haitaki kukubali. Mzee Nyalali na Mzee Warioba walionesha matatizo yako wapi lakini hatua hazikuchukuliwa na vizazi vilivyopita. Kinachokera ni kwamba MIZIGO YA TAIFA ndiyo wamekuwa vinara wa kulalamikia serikali ya CCM ilhali hawautaki ukweli. ​
Kumbe millennials ndio mizigo ya Taifa ! Daah ! Hatari sana 🙄
 
Kwa hiyo hawa wahuni aliwatengeneza Nyerere?
Na bahati nzuri, katika mstari huo huo umeandika "KUBADILI". Sasa Nyerere angewazuia vipi hawa wahuni?
Nyerere hakutengeneza hiyo mifumo na kuifanya kuwa matakwa ya taifa nyakati zote. Kama ilifaa wakati wake kwa sababu mbalimbali, haina maana kuwa itafaa nyakati zote.

Lakini hapa la muhimu ni kuwa umeeleza uwepo wa "wahuni". Nyerere hakutengeneza taifa la wahuni hata siku moja.
Kinacho shangaza pamoja na shutuma zote alizotoa kwa Nyerere mleta mada bado eti haamini katika kupata Katiba mpya !
Haya ni maajabu 🙄!
 
Kwahiyo na wewe huoni sababu au faida ya Katiba mpya ? 🤣
Kinacho shangaza pamoja na shutuma zote alizotoa kwa Nyerere mleta mada bado eti haamini katika kupata Katiba mpya !
Haya ni maajabu 🙄!
Hili ndilo tatizo kuu la Watanganyika: UFAHAMU na KUTOKUPENDA UKWELI.

Katiba mpya ni muhimu sana kwa nchi yetu, japo siyo mwarobaini wa kudumu endapo hizi akili hazitabadilika. Nitakupa mifano hai, mwaka 1995 nchi ya Uganda ilitengeneza katiba bora kabisa hapa Afrika, na Mzee Museveni alisifiwa mno. Ila katiba ilifuata utaratibu wote wa kisheria wa kutengeneza, na watu walihusishwa. Lakini mpaka kufika leo nini kinatokea Uganda, Museveni na genge lake wanafanya marekebisho kila uchaguzi mkuu ukikaribia.

Hili ndilo tatizo kuu la hapa Afrika. Wala siyo kwamba Mzungu katushinda Akili. Tatizo ni kwamba akili zetu haziwezi kuutazama ukweli na kukubali kubadilika.

Kuna nchi kama Uingereza, Israel, New Zealand hazina katiba (Unwritten/Uncodified Constitutions) kama kwetu sisi lakini nchi zao zina utulivu na maendeleo ya hali ya juu mno. Tatizo siyo tu kutunga sheria, tatizo ni kuwa na jamii yenye uelewa wa umuhimu wa kuheshimu sheria na katiba ya nchi. Ndiyo maana hata Father Padre Kitima aliwahi kusema inabidi tufanye kazi ya ziada kuelimisha kwanza watanzania juu ya umuhimu wa katiba.

Kisheria, KATIBA kama sheria inalindwa na wananchi. Haijilindi yenyewe. Hii dhana iliandikwa na Muingereza John Locke, na inaitwa CONSTITUTIONALISM. Sasa bila kuwepo na jamii inayofahamu kwanini tunahitaji katiba mpya, nini madhaifu ya katiba ya zamani, na kwanini tumefika hapa tulipo leo, hata waletewe Nabii wa kale usidhani kama watafanya chochote kile.

ENIWEI sidhani kama umenielewa!

Hizo ni propaganda kwamba mbona kwa Waganda haijafanya kazi ? Jibu ni kwamba ile Katiba ilikuwa ni Danganya toto it was not for real ndio maana haiwezi kuwa na sheria zenye kuleta haki kwa wote. !
Sijui kama utanielewa nikisema hapa kwetu Rasimu ya Mzee Warioba ndio muarobaini wa yote haya yanayotokea ambayo yanalalamikiwa !
Sijui umenielewa ??!
 
Inawezekana!

Katiba mpya ni hatua ya msingi mno, japo siyo ya mwisho katika kuleta mabadiliko!
===================================================
Leo nimemuuliza Roboti Grok akanijibu hivi kuhusu hili swali:
Creation of the new constitution in Tanzania is an important step but not a decisive one.
======================================================

I agree — adopting a new constitution in Tanzania would be a significant milestone, but far from a decisive turning point on its own.

Why It's Important:

Tanzania's current constitution dates back to 1977 (with amendments), rooted in the single-party era under Julius Nyerere. It gives extensive powers to the executive, limits judicial independence in key areas (such as challenging election results), and has been criticized for favoring the long-ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM).

A new constitution could:

​
  • Strengthen checks and balances.
  • Create a more independent electoral commission.
  • Clarify the structure of the Union with Zanzibar.
  • Expand rights protections and decentralize power

Why It's Not Decisive ?

Constitutions are frameworks, not magic wands. Many African countries have adopted "model" constitutions on paper while governance remains poor in practice. Key reasons this alone wouldn't transform Tanzania:

  • Implementation gap: Even the best constitution fails without independent institutions, a professional civil service, and a judiciary willing to enforce it. Tanzania's challenges include corruption, weak rule of law, and executive dominance that often bypasses legal limits.
  • Political culture and incentives: CCM has dominated since independence. A new constitution negotiated or drafted under ruling party influence might entrench advantages rather than level the playing field. Opposition groups (e.g., CHADEMA) push for the earlier "Warioba draft" as more people-centered, while skepticism remains high about the process being genuine.
  • Timing and sequencing: Reforms have repeatedly been delayed (post-2014 stalled process, postponed again before 2025 elections). Post-election dynamics in 2025–2026 will matter more — if the process lacks broad consensus, it could deepen divisions rather than heal them.
  • Deeper drivers: Economic development, education, youth employment, and reducing ethnic/regional patronage matter as much as formal rules. Authoritarian tendencies can persist under democratic-looking constitutions if power structures (party, military, business elites) don't shift.

What Would Make It Decisive?

A new constitution becomes transformative when paired with:

  • Inclusive, transparent process — Broad public participation, not just elite bargaining.
  • Independent institutions — Especially an electoral body not controlled by the incumbent.
  • Civic education and political maturity — Citizens and parties ready to use new rules.
  • Follow-through — Judicial review, enforcement mechanisms, and gradual power alternation.
History shows that credible elections and peaceful transfers of power often drive deeper change more than constitutional text alone. Tanzania has relative stability and economic potential, but its democratic deficits (low trust, polarized politics) require sustained effort beyond one document.

In short, a new constitution is a necessary enabling step — it resets the rules of the game. But the decisive factors will be whether elites and citizens actually play by (and enforce) those rules afterward. Without that, it risks becoming another impressive document gathering dust. What specific aspects of the process or content do you see as most critical?
 
Hata huyo robot amekubali kwamba a new constitution is a necessary enabling step 👍 !
A NECESSARY ENABLING STEP ! Huyo ni Robot 🤖 msomi 😁🫡
Kamatilia hapohapo 😁
 
Mwenye macho haambiwi tazama.

Haya ndiyo mambo makuu ambayo Mzee Nyerere aliiachia Tanzania na yamedumu hata baada ya yeye kuondoka, na kuna hatihati kwamba yataendelea kuwepo kwa muda zaidi hapa nchini. Ukweli mchungu ambao wafuasi wa Mzee Nyerere hawapendi kuukubali ni kwamba mambo haya yana mabaya mengi kwa watanzania, hasahasa watanganyika kuliko mazuri. Habu zingatia:

1. MUUNGANO WA TANZANIA (1964)
​
👍

2. CHAMA CHA MAPINDUZI (1977)​
Hii huwezi kuita LEGACY, Maana ukiita LEGACY maana yake hata MULTIPARTISM ni LEGACY ya NYERERE.

3. KATIBA YA JAMHURI (1977)​
Katiba haiwezi kuwa LEGACY, kwasababu ni kitu kinachobadilika.

4. KUPOKEZANA URAISI KIDINI​
Hii ni POLITICAL WILL tu ndani ya CCM, kama amabvyo serikali iliondoa DODOSO LA DINI kwenye sensa na kuifanyanchi ouwa SECULAR.

Kama ambavyo, Urais wa kupokezana Bara na Zanzibar haukuonekana baada ya Magufuli na Kikwete, hata hili linaweza lisiwepo.

Mazoea fulani, kuwepo haimaanishi ndio LEGACY ya suala husika.

======================================================

Hatutaki kukubali kwamba Mzee Nyerere alitengeneza MFUMO MBOVU, tangu siku ya kwanza anaingia Magogoni.

MSIDANGANYIKE, bila kukubali UKWELI Tanzania haiwezi kujinasua hapa ilipo. Ni lazima tukubali ukweli kwanza kwamba Mzee Nyerere alikosea na MFUMO aliotuachia ulikuwa MBOVU. Ukishakubali huu ukweli bila kukwepa (Deflecting) ndiyo macho yako yatafunguka na utaanza kuangalia Tanzania katika jicho la tofauti sana. Binafsi tangu niko sekondari nimekuwa nasoma vitabu vya UHURU NA UMOJA (FREEDOM & UNITY) ambavyo ni mkusanyiko wa hotuba za Mzee Nyerere tokea 1962.
​
Shida yenu kubwa ni kuwa MMESHINDWA kuwajibisha wanasiasa.wenu, mnakimbilia kumlaumu Nyerere.

Leteni USHAHIDI wa maandishi unaoonesha kuna MAANDISHI yoyote mabovu aliyaacha Nyerere?

Katiba haishiki BUNDUKI. Inalindwa na watu.

Hata uwe na katiba nzuri kiasi gani, ila ikitokea una watawala WAOVU kama SAMIA, hakuna namna itasaidia maana WATAWALA WAOVU hawafuati MFUMO RASMI.

Nimefika CHUO KIKUU ni MJAMAA kindakindaki. Nilikuwa siamini kabisa hata katika UTAJIRI jambo ambalo hadi watu wa nyumbani kwetu walikuwa wananishangaa. Darasani walikuwa wakimkosoa Mzee Nyerere hasa waalimu wetu ambao siyo watanzania nilikuwa naghafirika mno. Wakati niko chuo, ulikuwa ukiniambia twende leo tuchukue bunduki tuue matajiri wote, nilikuwa naweza hata kufanya bure bila mshahara. I WAS A DEVOUT COMMUNIST, kiwango ambacho nilikuwa sina mzaha kabisa na maisha.​
UJAMAA hauchukii MATAJIRI.

Kazi ya UJAMAA ni kujenga mfumo.HYBRID kama DOLA kusimama kama REFA ili kila mtu apate haki yake.

Kazi ya UJAMAA ni kuhakikisha MIFUMO ya kiuchumi ya NCHI inamilikiwa na UMMA, ili.maisha yawe AFFORDABLE kwa kila mtu.

Nchi za kibepari zinajiemdesha KITAPELI, kwa kutiza kodi wananchi, na kuwauzia huduma.za umma ata market prices.

Kwenye Ujamaa, Nyerere was 600% RIGHT.
======================================================

Mambo yalianza kubadilika baada ya kuanza kukutana na watawala wa Tanzania ambao ndiyo wako sehemu za maamuzi. Nikaanza kujiuliza maswali mengi sana. Kwanini mambo hayaendi kama yanavyotakiwa kwenda. Nikafahamu jambo moja baya sana. WATAWALA WOTE WA TANZANIA wana akili moja (A Herd Mindset/A Hive Mindset) ambapo dunia wanaitazaman katika kurunzi moja tu. Hahawezi kufikiri wenyewe jambo jipya. Mfumo mzima wa nchi, unatawaliwa na fikra za mtu ambaye amelela kule BUTIAMA.
​
Hapa wewe ndio mwenye TATIZO, na lazima kila mwenye akili timamau a-question akili yako, kwasababu ni zero reasoning.

Kuhusu watawala.wa Magaribu kutokumuelwa Nyerere nakubakiana nao.

Ila nadhani kwasasa after the RISE of China, wengine wameanza kujifunza kwa njia ngumu kuwa kwenye CAPITALIST WORLD, hauna NCHI, bali una CORPORATE CAPITALIST CORPORATION.

Sasa hoja ambazo wafuasi wengi wa Mzee Nyerere wamekuwa wakizitoa pindi unawaambia ukweli ni hizi:

a) MZEE NYERERE ALIONDOKA MADARAKANI MIAKA 41 ILIYOPITA
Wakisahau kwamba Mzee Nyerere alitawala nchi kwa kutumia taasisi(Institutions). Siku zote taasisi zinaundwa na vitu muhimu kama Sera (Policies) na Sheria (Laws). Kwa pamoja, INSTITUTIONS+POLICIES+LAWS=SYSTEM. Bahati mbaya mno sera, sheria na taasisi nyingi ambazo zilitumika na Mzee Nyerere ndiyo zinaendelea kutumika mpaka leo hii Tanzania.

Mbaya zaidi. Wakati Tanzania inapata Uhuru, Mzee Nyerere alirithi MFUMO WA KIKOLONI ambapo aliendelea na taasisi na sheria za kikoloni. Unaposoma historia, moja ya jambo kubwa ambalo tunajifunza ni ESTABLISHMENT OF COLONIAL ECONOMY, ambapo jambo la kwanza kujifunza ni sifa kuu za dola la kikoloni (Features of A Colonial State), ambazo ni hizi zifuatazo: Exploitative in Nature (Dola la kinyonyaji), Pyramidal (Dola lenye matabaka) na Violent in Nature (Dola dhalimu na kandamizi).

Yote haya yaliwezeshwa na sheria na taasisi za kikoloni ambazo zilianzishwa na Wajerumani au Waingereza. Mzee Nyerere alipata nchi, sheria nyingi za kikoloni alibadilisha jina na kuendelea kuzitumia kutawala watanganyika. Sehemu walipoandika Governor yeye akaweka Prime Minister/President. Hili hata The Nyalali Commission ililisema kwa kina, tatizo ni kwamba watanzania ni watu wasiopenda kusoma na kudadisi vitu.

Huwezi kusema unatengeneza taifa la watu huru, ilhali bado unatumia taasisi na sheria za kikoloni kutawala. Hata kama una malengo mazuri, mfumo lazima utakuangusha. Taasisi za kiuasalama kama TPDF, PT, TISS zote zina mzizi kwenye ukoloni. Ndiyo maana hata zinapofanya mambo ya ajabu mimi sishangai kwasababu kimsingi lengo lake ni kulinda dola na siyo wananchi. Mabadiliko ya kitaasisi walau yalianza kufanyika kidogo kuanzia mwaka 1996-2015 chini ya Mkapa na Kikwete.

SASA KWANINI NASEMA HIVI: Kikawaida unapotaka kufanya mabadiliko makubwa kwenye nchi, jambo la msingi kabisa na kupambana na mfumo (Policies, Laws, Institutions and People/Gate-Keepers). Hii ndiyo sababu ya msingi kwanini mapinduzi yote huwa yamejaa vurugu na umwagikaji wa damu mkubwa. Wanamapinduzi huhakikisha kwamba wanabomoa mfumo wote pamoja na walinzi wake, kuanza kujenga upya tokea chini.

Mfano wa hili nalilisema ni kilichotokea nchini Ujerumani baada ya mwaka 1945, kilichoitwa THE DENAZIFICATION OF GERMANY, ambapo USSR, BRITAIN, FRANCE na USA waliigawanya Ujerumani vipande vinne ambavyo walivitawala kwa nguvu za kijeshi na kuhakikisha SERA, SHERIA, TAASISI na WALINZI WA MFUMO wanapukutishwa ndani na nje ya Ujerumani. Maelfu ya Wajerumani walihamishwa, wengine waliuwawa, na sheria mpya zikatungwa kuhakikisha kilichotokea mwaka 1933 chini ya Adolf Hitler hakirudii tena.

Mwaka 1991, wakati USSR inaanguka, ili Marekani kuzuia haya yanayoendelea leo dhidi yake alitakiwa ahakikishe taasisi kama KGB, GRU, CPSU, COM-INTERN zinavunjika na watu wake wanashughulikiwa vilivyo. Ila Marekani akasherehekea ushindi, na taasisi za USSR za kikomunisti na watu wake zikaendelea kuwepo huku zikiwa zimebadili majina tu. Watu waliokuwa na mawazo ya kuvamia Marekani na kuishambulia kinyuklia miaka ya 70's hawawezi kubadilika na kuanza kuwa marafiki zenu ndani ya usiku mmoja. Putin na genge lake la The Siloviki, ni WALINDA MFUMO WA USSR.

=========================================================================

Haya ni machache tu, ambayo siyo mimi ambaye nimeyaona, lakini hata wasomi nguli wa sheria nchi hii kama Jaji Nyalali, Jaji Lugakingira na Chris Maina wameyaona kuhusu Mzee Nyerere na mfumo wake aliourithi kutoka kwa mkoloni na kuutumia kuendesha Tanzania. Nafahamu fika kwamba haya ni magumu kumeza kwasababu FALSAFA ZA NYERERE zinawianishwa na TANZANIAN IDENTITY, ambapo watu wameaminishwa kwamba wakiachana nazo bado Utanzania ndiyo umekwisha na taifa litaparanganyika, jambo ambalo halina ukweli wowote ule.​
Mnaomkosoa Nyerere, mnapenda sana kujificha kwenye maneno MFUMO, TAAISISI.

Njooni hapa na HOJA.

Nyerere alipuyanga jwe ye Jambo A.

Ilitakiwa fanye jambo B ambalo ni SUPER.

=====================================================

b) TANGANYIKA HAIPO ISHAKUFA, KATIBA IMEUA TANGANYIKA
Hii ni moja kati ya hoja ya kipumbavu kabisa ambayo watu wasiokuwa na uelewa, ambao wengi wao ni wafuasi wa Mzee Nyerere, wana-CCM na Walinda Mfumo hupenda kuitumia kubeza au kukwepa ukweli. Wao wanaamini kabisa kwamba KATIBA YA MWAKA 1964 na ile ya mwaka 1977 imeiua Tanganyika.

Juu-Juu unaweza ukadhani kwamba hawa watu wana akili na hoja, lakini ukweli ni kwamba ni WAPUMBAVU SANA na hawana uelewa. Kikawaida sheria inayoanzisha taifa huanzishwa kupitia sheria za kimataifa (International Law) na sheria za ndani (Municipal Law) kwa pamoja. Huwezi kusema kwamba taifa limezaliwa au limekufa kwa kuangalia sheria za kimataifa peke yake (International Law) au sheria za ndani (Municipal Law) peke yake.

Kama ingekuwa ni hivyo basi dunia hii ingekuwa imejaa vurugu na sintofahamu maana leo hii taifa kubwa linaweza likaamka tu na kuamua kutambua kipande cha nchi husika kwamba ni nchi huru ili tu kuivuruga nchi husika. AU anaweza akamka tu mtawala ambaye hajaridhika na uchaguzi akaamua tu kutoa mkoa mmoja na kusema hii ni nchi yake huru. Haya hayapo, na ndiyo dunia inavyoenda, NI MPUMBAVU tu anaweza kupingana na UKWELI wa jinsi dunia inaenda.

KISHERIA SASA: Tanzania ni muunganiko wa mataifa mawili yaliyokuwa huru, Tanganyika na Zanzibar. Tanzania imeanzishwa kupitia mkataba wa kimataifa uitwao, ARTICLES OF THE UNION 1964, ambapo ukizingatia nchi ambazo zinafuata mfumo wa COMMON LAW kama yetu ambayo pia ni MONIST, lazima sheria hizi zipitishwe na bunge. Hivyo mkataba wa kimataifa uitwao ARTICLES OF THE UNION 1964 ambao ulisainiwa na Mzee Nyerere na Mzee Karume kwa lengo la kuunganisha haya mataifa mawili, ulipitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar ili iweze kuwa sheria ya nchi ambayo inaanzisha taifa jipya la Tanzania.

Baada ya maridhio (Ratifications) ARTICLES OF THE UNION 1964 ilitungiwa sheria iitwayo ACT OF THE UNION 1964 ambayo iliingizwa kwenye KATIBA YA TANZANIA ya mwaka 1965 kama ndiyo msingi wenyewe wa Jamhuri, ikiwa na mambo ya muungano (Union Matters) kumi na moja tu.

Hivyo basi, hapa tunaona kilichotumika ni sheria ya kimataifa (International Law) na sheria ya ndani (Municipal Law). Sasa basi wasomi nguli kama Prof Issa G Shivji wanasema kwamba ARTICLES OF THE UNION 1964 ni mkataba muhimu sana ambapo huwezi kubadilisha sheria ya nchi hasa katiba bila kuzingatia mambo ya msingi yaliyomo mle ndani. Hivyo kile kitendo cha kuondoa Tanganyika kwenye nyaraka zote za Muungano, Kufuta ACTS OF THE UNION kwenye katiba za Tanzania, na Kuongeza Mambo ya Muungano (Union Matters) kutoka 11 hadi 22 kinyemela ni jambo la kifedhuli, ambalo madhara yake watanganyika mnaanza kuyaona sasa baada ya wazanzibari kuanza kuyaona tokea mwaka 1964 wakiwaambia badilisheni ila mnajitia kichwa ngumu.
====================================================

SASA BASI: Kama Muungano wetu ulikuwa ni wa kimkataba, Tanganyika bado kwasababu uhalali wote wa Tanzania katika unatokana na ARTICLES OF THE UNION 1964 na ACTS OF THE UNION 1964, siyo maneno ya geresha ya WATANGANYIKA WASIOKUWA NA UELEWA.

Sheria za kimataifa zina kitu kiitwacho SOVEREIGNTY, ambayo ni nguvu ya dola kufanya mambo yake bila kuingiliwa na dola jingine, AU Kiingereza tunasema, "The ability to exercise state functions without interference of the third party". Tanzania ni nchi huru, A Sovereign State. Lakini, Sovereignty yake imegawanyika (Divisible) kwasababu Tanzania kama Dola kuu ndani yake kuna Dola jingine mwanachama, Zanzibar. Msomi nguli wa Sheria za kimataifa wa karne iliyopita Prof Herch Lauterpatch anayaita madola ya namna hii Composite States, ambayo huwa yanakuwa na uwezo wa kujiendesha yenyewe na kujiamulia mambo mengine yenyewe.

Hili kwenye sheria za kimataifa tunaliita INTERNAL SOVEREIGNTY, ambapo dola mwanachama linakuwa na uwezo wa kuendesha mambo yake ya msingi kama katiba inavyosema bila kuingiliwa na dola kuu. Sasa kitendo cha kukubali kwamba KATIBA YA MWAKA 1977, ina mambo ya muungano (Union Matters) na mambo yasiyokuwa ya muungano (Non-Union Matters) ni kukiri kabisa uwepo wa Tanganyika kama dola hai. Kuiita Tanganyika, Tanzania Bara na kusema itaamuliwa na Serikali Kuu hakuondoi ukweli wa uwepo wa Tanganyika.

====================================================

TANGANYIKA iko kisheria na haiwezi kuuwawa na KATIBA YA TANZANIA, kwasababu bila Tanganyika hakuna Tanzania. Tanganyika na Zanzibar kupitia ARTICLES OF THE UNION/ACTS OF THE UNION ndiyo zinaipa uhalali Tanzania kuwepo, siyo KATIBA. This is a very simple Legal Logic.

Hivi hamjiulizi maswali marahisi kabisa: KWANINI MZEE NYERERE na CCM wake walitumia na wanaendelea kutumia nguvu kubwa kuficha Mkataba wa Muungano (Articles of the Union). Kwasababu wanafahamu ukweli, kwamba pindi mambo yatakapokuwa wazi hawatakuwa na chao hapa. Hivyo kuendelea kupumbaza watanganyika ni kuwavalisha uhusika mwingine (UTANZANIA) ambao utawalazimisha wakumbatiane na WAZANZIBARI kiutendaji.

UTANGANYIKA unafichwa kwasababu, kanuni rahisi kabisa ambayo mkoloni aliitumia duniani kote ili kufanikiwa kutawala watu, ni kuhakikisha unafuta historia yake na kukijaza kizazi kipya kujichukia wenyewe. Hii ni mbinu ya kikoloni ambayo imefanikiwa kufanya kazi kwa asilimia 10000000000% kwenye akili za watanganyika.

LEO HII, wanaoongoza kwa kulilia na kulazimisha huu MUUNGANO uendelee kuwepo ni WATANGANYIKA. Wao wanasema usivunjike ila twende kwenye serikali MOJA ilhali ukweli mchungu ni kwamba upande wa pili wa MUUNGANO, wazanzibari hata hawawachukulii ninyi kama ndugu, isitoshe binadamu.

=======================================================

KISIASA ni rahisi sana kuuongelea huu MUUNGANO, lakini ukizingatia UKWELI, utafahamu kwamba Tanzania ilivunjika miaka ya 60's na kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni geresha tu. Ndiyo maana kuna wakati Ndugu Tundu Lissu aliwahi kusema kwamba "Zanzibar ni koloni la Tanganyika" jambo ambalo lilitukera wengi hata ambao siyo wafuasi wa Muungano. Kuchonganisha watanganyika na wazanzibari wa kawaida unapata faida gani ???

Kiukweli ukiuliza watanganyika wa kawaida wananufaikaje na muungano ambao hawakuubariki unabakia na ukakasi. Kusema kwamba Zanzibari ni Koloni la Tanganyika ni kuleta taharuki na chuki baina ya watu wa kawaida. Baadaye huyohuyo Lissu akaanza kudai kwamba "Mzanzibari anauza mali za Tanganyika", ghafla Zanzibar siyo koloni tena.

Niliwaza sana na kufikia hitimisho kwamba, MKAKATI WA NYERERE unaendelea kufanya kazi, kwasababu MFUMO WA MUUNGANO umewachanganya akili watu kama Lissu. Matatizo yanayoendelea hapa, siyo UTANZANIA au UZANZIBARI, bali ni mfumo ulioachwa unaowapa nguvu watawala kufanya wanachojitakia. Mali za Tanganyika zimeuzwa tangu Mwinyi, Mkapa na Kikwete, huyu Samia anaendelea kufanya alichoona watangulizi wake wanafanya. HAKUNA JIPYA

=========================================================

HITIMISHO: Watanganyika hawawezi kupata mabadiliko ilhali hawataki UKWELI.

UKWELI huanzia pale tunapofahamu tatizo lilianzia kwa nani na lini. Tukishalifahamu hili ndiyo tunaanza kuchunguza historia ya kipindi chote hichi na kuweza kutengeneza dawa yake, na jinsi ya kufanya matibabu

JAPO, naamini Tanganyika haiwezi kubadilishwa na kizazi cha 1940-1950's, 1960-1980's. Walau watakaoweza kubadilisha Tanzania ni wale wa kizazi kipya cha 1990's kuendelea mbele. Hawa ndiyo wako radhi kuusikia ukweli kama ulivyo na ndiyo wahanga wakubwa wa UJINGA na UFEDHULI uliofanywa na vizazi vilivyopita.

Binafsi huwa naamini mabadiliko yatakuja, ila yatakuja kwa maumivu makali sana. Tena sanaaa. Tanzania ambayo mlikuwa mnaifahamu ilishajifia tayari, na kilichotokea 29 Oktoba 2025 ilitakiwa iwe UAMSHO TOSHA kwamba kama watawala wanaweza kuua watoto wenu kwa maelfu bila kuwajibika na kutupa maiti zao kama wanyama, na kuendelea kuwasimanga marehemu na wafiwa, basi fahamu fika hapo HAKUNA NCHI.

MKIENDELEA KUBISHA na KUSHUPAZA SHINGO, siku nyingine mtaendelea kushuhudia misiba mikubwa mpaka akili ziwakae sawa na mchukue hatua. UKWELI ni kwamba nchi yetu ina msingi mbaya ambao bila kurekebisha hatuwezi kufika popote. Lazima tuanze kukubali ukweli huu ndiyo mengine yafuate.

ENIWEI sijui kama tutaelewana......
​
NYERERE aliamini kwenye KUUNGANA.

Mtu yogote TIMAMU, must move towards UNITY.

Wakati tunaanza Muungano, tulikuwa na serikali 2, na nchi moja.

Ila kwakuwa kwasasa tuna watawala ambao ni VICHWA VYA PANZI, tumekuwa na NCHI 2 na watu wanaodhani hoja zinajibiwa kwa bunduki.

Hizi nchi 2, zinatokana na matamanio tu ya kisiasa ya watu kutoka Zanzibar ambao wanatumia Nationalism kusaka vyeo na jaira kwenye Muungano.

Na kibaya zaidi hali hii inatokea nyakati amabbyo tuna "a very highly INSECURE EVIL REGIME. Leadership CRISIS.

=======

LEGACY YA NYERERE. ni:

  • NATIONALISM kupitia KISWAHILI
  • ARDHI
  • UADILIFU
  • UZALENDO
  • MUUNGANO
  • SADC na
  • FOREIGN AFFAIRS POLICY
 
"The main foundation of the Constitutions of the United Republic of Tanzania of 1977 and the Zanzibar Revolutionary Government of 1984 is the Articles of the Union of 1964."

Tovuti ya serikali inasema dhahiri kwamba uhalali wa katiba ya Tanzania na Zanzibar ni Articles of the Union 1964 na Acts of the Union. Ukizitoa hizi taifa halina uhalali. Mengine huhitaji kufundishwa, unahitaji kufukiria tu.​
Lisu aliwahi kuhoji uwepo wa articles of union. Hakupewa Wala hakuoneshwa. Yeye husema hazipo. Kama zipo zioneshwe kwa watu.
 
Andiko zuri. Hongera.
Ingawa nilitarajia andiko lako la kwanza baada ya ziara ya Urusi lingeangazia Ile ziara maana upande mwingine huwa inagusa sana mambo ya diplomasia na mahusiano ya ki nchi.
 
Lisu aliwahi kuhoji uwepo wa articles of union. Hakupewa Wala hakuoneshwa. Yeye husema hazipo. Kama zipo zioneshwe kwa watu.
Zimejaa masharti ambayo yanataka MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibar uweje.

Zikipatikana basi katiba zetu zote mbili zinakosa uhalali wa kisheria.

Kama Nyerere alikuwa na nia njema kwanini alizificha ???
​
 
Ndivyo alivyokuwa Mzee Nyerere anatenda kwanza halafu anajutia baadaye.

Hata mwaka 1993-1996 alipoonywa na kina Kolimba kuhusu ukweli wa CCM hakusikia.

Akavuruga uchaguzi ndani ya CCM na nchi halafu baadaye akataka amtoea Mzee Mkapa.

Hivi unadhani watu watamuelewa mtu wa aina hii kweli, ambaye alituaminisha Mzee Mkapa ni mtu msafi na anafaa kuwa Raisi lakini baadaye anaanza kulalamika kwamba Mkapa hafai. UKWELI aliambiwa lakini hakutaka kusikia, akawahujumu watu ndani na nje ya chama.

Kina Kombe, Kolimba, Babu, Kambona yaliwakuta makubwa kwasababu walionesha kushindana na EGO ya Mzee Nyerere, wala siyo usaliti wa chama au taifa. Ni EGO tu.
=====================================================

Ukianza kufuatilia hata yaliyokuwa yanaendelea kwenye ukanda huu unaanza kupata wasiwasi na akili za Mzee Nyerere na malengo yake. Aliingiza Tanzania kwenye VITA YA KAGERA ili kumrudisha swahiba wake Milton Obote. Vita ambayo kiuhalisia ilikuwa inaepukika kwasababu kulikuwa na madikteta wabaya ukanda huu kuliko Iddi Amini.

Nchi imefilisika, baadaye akagombana na Obote akaanza kumuunga mkono Museveni. Sasa unakaa unajiuliza lengo lake huyu lilikuwa ni lipi haswaa, hupati majawabu. Anafanya maamuzi ya haraka halafu baadaye anageuka anaanza kulazimisha jambo jingine.

Kule Rwanda ndiyo hatutazungumzia, lakini yale madudu yote ya 1990's Mzee Nyerere alihusika mno. Sema tu hatuwezi kuyasema waziwazi hapa. Ila ukweli mchungu ni kwamba Nyerere has left behind a trail of blood and mayhem.
​
Kwangu Mandela ataendelea kua bora kuliko Nyerere
 
Back
Top Bottom