Legacy kuu za Mwalimu Nyerere: Mwiba mkali kooni mwa Watanganyika

Legacy kuu za Mwalimu Nyerere: Mwiba mkali kooni mwa Watanganyika

Labda Samia ndio maana anatikisa chupa ya chai tuanze upya ila tupo usingizini. Yaliyotokea 29th October na mpaka sasa hakuna uwajibikaji hadi tunategemea international communities watusaidie kwangu ndio niliamini watawala wanao uwezo wa kutufanya chochote na yoyote. Sioni dalili za miaka ya karibini kutokea mabadiliko ya kweli
Tanganyika bado wamelala sana Chama cha CCM kininaitaji kuwajibika bora mara mia wangemsikilizi pole pole
 
Zimejaa masharti ambayo yanataka MUUNGANO wa Tanganyika na Zanzibar uweje.

Zikipatikana basi katiba zetu zote mbili zinakosa uhalali wa kisheria.

Kama Nyerere alikuwa na nia njema kwanini alizificha ???
​
Malcom, Nyerere is no more.
Yeye, Lisu amehoji uwepo wa hizo articles kipindi hiki baada ya Nyerere kufa. Nakumbuka rais alikuwa Kikwete. Naona unamlaumu Nyerere lakini Lisu kahoji wakati wa Kikwete. Nyerere alificha inawezekana maana kwa upeo wangu sikumbuki mtu aliyehoji uwepo wa hizo articles bungeni kipindi Cha Nyerere kama yupo nielimishe maana sikuishi Mwalimu's era. Kwanini haumlaumu Kikwete aliyemjibu Lisu kuwa articles ziko salama na hakuzionesha kwa Lisu binafsi Wala kwa bunge maana Lisu alihoji angali mbunge.
 
Nyerere alikua muhuni tu na hapo ndo huwa namkubali mandera
Baada ya miaka 50. Wasaouth Africa wataenda kunya ktk kaburi la Mandela kama halitakuwa na ulinzi. He betrayed all of his fellow fighters compromising with the oppressor in the question of land and so many others. Time will tell.
 
Malcom, Nyerere is no more.
Yeye, Lisu amehoji uwepo wa hizo articles kipindi hiki baada ya Nyerere kufa. Nakumbuka rais alikuwa Kikwete. Naona unamlaumu Nyerere lakini Lisu kahoji wakati wa Kikwete. Nyerere alificha inawezekana maana kwa upeo wangu sikumbuki mtu aliyehoji uwepo wa hizo articles bungeni kipindi Cha Nyerere kama yupo nielimishe maana sikuishi Mwalimu's era. Kwanini haumlaumu Kikwete aliyemjibu Lisu kuwa articles ziko salama na hakuzionesha kwa Lisu binafsi Wala kwa bunge maana Lisu alihoji angali mbunge.
Binadamu wa kwanza kuhoji kuhusu Articles of the Union ni Sheikh Abeid Karume.

Wote tunafahamu nini kilimkuta.

Mwingine ni Jumbe.....
​
 
Binadamu wa kwanza kuhoji kuhusu Articles of the Union ni Sheikh Abeid Karume.

Wote tunafahamu nini kilimkuta.

Mwingine ni Jumbe.....
​
Sasa isije ikafika hatua zikahakiwa au zikapotea naamini zinatakiwa kuonekana maana ni urthi wetu. Pia, inawezekanaje wanasheria nguli ktk nchii hawajawahi peleka kesi mahakamani kudai masuala ya uwepo wa articles?
 
Mtakubaliana na Tundu Lissu kuhusu chanzo kikuu cha tatizo kama alivyoainisha kwenye hotuba yake kwenye Bunge la Katiba ?​
Tutakubaliana nae ndio. Na hati ya makubaliano ya Muugano inatakiwa iwe wazi, wananchi waione, sio blah blah za kusema eti wakachukue ule mchanga uliotupwa baharini.
Zile ni futuhi.
 
Ndivyo alivyokuwa Mzee Nyerere anatenda kwanza halafu anajutia baadaye.

Hata mwaka 1993-1996 alipoonywa na kina Kolimba kuhusu ukweli wa CCM hakusikia.

Akavuruga uchaguzi ndani ya CCM na nchi halafu baadaye akataka amtoea Mzee Mkapa.

Hivi unadhani watu watamuelewa mtu wa aina hii kweli, ambaye alituaminisha Mzee Mkapa ni mtu msafi na anafaa kuwa Raisi lakini baadaye anaanza kulalamika kwamba Mkapa hafai. UKWELI aliambiwa lakini hakutaka kusikia, akawahujumu watu ndani na nje ya chama.

Kina Kombe, Kolimba, Babu, Kambona yaliwakuta makubwa kwasababu walionesha kushindana na EGO ya Mzee Nyerere, wala siyo usaliti wa chama au taifa. Ni EGO tu.
=====================================================

Ukianza kufuatilia hata yaliyokuwa yanaendelea kwenye ukanda huu unaanza kupata wasiwasi na akili za Mzee Nyerere na malengo yake. Aliingiza Tanzania kwenye VITA YA KAGERA ili kumrudisha swahiba wake Milton Obote. Vita ambayo kiuhalisia ilikuwa inaepukika kwasababu kulikuwa na madikteta wabaya ukanda huu kuliko Iddi Amini.

Nchi imefilisika, baadaye akagombana na Obote akaanza kumuunga mkono Museveni. Sasa unakaa unajiuliza lengo lake huyu lilikuwa ni lipi haswaa, hupati majawabu. Anafanya maamuzi ya haraka halafu baadaye anageuka anaanza kulazimisha jambo jingine.

Kule Rwanda ndiyo hatutazungumzia, lakini yale madudu yote ya 1990's Mzee Nyerere alihusika mno. Sema tu hatuwezi kuyasema waziwazi hapa. Ila ukweli mchungu ni kwamba Nyerere has left behind a trail of blood and mayhem.
​
Wee sema yotee, usiache kitu UKWELI lazima USEMWE.
 
Mimi mpaka leo bado ninajiuliza Mwalimu Nyerere alionekana mtu mwenye akili sana,hasa ukisikia simulizi za walio kuwa kipindi cha utawala wake.

Hili la muungano huwa linafanya niwe na ukakasi juu ya historia hizi kwamba ni kweli au Zina chumvi kwa sababu iweje mtu mwenye akili ashindwe kung'amua kasoro za muungano ambazo zilioneshwa hata na G 55
Muungano huu hata Asiyejua kusoma na kuandika, akiona tu matendo anaelewa.

Ilikuaje msomi wa Makerere akazidiwa ujanja na baharia au Sheikh wa madrasa. Inashangazaa mnoo.
 
Hoja kubwa hapa ni maslahi tu...
Nani anafaidika na muungano?
Kwanini wanatumia nguvu nyingi sana kuulinda?
Kwanini hawataki mabadiliko na kuendelea kudai katiba haitatupa chakula cha siku?
Kwanini hawataki hata maoni ya kuanzia na serikali 3? Wanaogopa nini?
Kwanini hawataki kusikiliza hata kufanya referendum bara na visiwani raia tuamuwe tunachotaka na siyo WANACHOTAKA?
Kwanini ukitaja TANGANYIKA waonekana mbaguzi, msaliti, mvunja amani, siyo mzalendo?
Hayo wanatotetea Sasa YATAKUJA KULETA MTAFARUKI, MACHAFUKO NA MADHARA MAKUBWA SANA SANA KWA PANDE ZOTE 2...
 
Mwenye macho haambiwi tazama.

Haya ndiyo mambo makuu ambayo Mzee Nyerere aliiachia Tanzania na yamedumu hata baada ya yeye kuondoka, na kuna hatihati kwamba yataendelea kuwepo kwa muda zaidi hapa nchini. Ukweli mchungu ambao wafuasi wa Mzee Nyerere hawapendi kuukubali ni kwamba mambo haya yana mabaya mengi kwa watanzania, hasahasa watanganyika kuliko mazuri. Habu zingatia:

1. MUUNGANO WA TANZANIA (1964)

2. CHAMA CHA MAPINDUZI (1977)

3. KATIBA YA JAMHURI (1977)

4. KUPOKEZANA URAISI KIDINI


Kinachosikitisha ni kwamba, katika haya matatu hakuna hata kimoja kilipitishwa, kuundwa au kutengenezwa kwa ridhaa ya wananchi. Watanzania na Wazanzibari wangekuwa wametoa baraka zao, basi kusingekuwa na minong'ono mingi na malalamiko mengi kama ambavyo tunasikia kipindi hiki. Watanganyika wanapenda kulalamika kuhusu MUUNGANO, KATIBA na CCM, na wanataka kutokana na haya matatizo ila ukiwaambia ukweli huwa hawataki kusikia.

=====================================================

NJIA KUU ya kutatua tatizo lolote lile kwenye maisha ni kukubali UKWELI hata kama ni mchungu, unakera na kuumiza. UKWELI una sifa ya kuweka watu huru. Ukiona taifa au jamii yoyote haiendelei basi fahamu fika kuwa iko mbali na UKWELI.

Umasikini, Maradhi na Ujinga vyote vinatokana na kutokufahamu UKWELI. Wanadamu wa kale waliokuwa wanaishi maporini, walianza kubadilika baada ya kutambua ukweli kuhusu mazingira yake. Alianza kugundua MOTO, baadaye CHUMA na mwishowe akaanza kujenga jamii kubwa mpaka leo hii.

Wenzetu wa Ulaya walianza waliwahi kuwa kama sisi kwa karne zaidi ya kumi. Walikuwa wanaabudu watawala wa kifalme huku UJINGA ukiwa umewajaa vichwani mwao. Walipoanza kuukubali UKWELI wakaingia kwenye kipindi kiitwacho THE RENAISSANCE na baadaye THE ENLIGHTENMENT PERIOD, vipindi ambavyo waliachana kabisa na UJINGA ambao ulikuwa umeungamanishwa kama sehemu ya tamaduni zao za kila siku.

======================================================


KATIBA ZA ULAYA, zilikuwa zina sifa kuu zifuatazo: Utawala wa Kifalme(Divine Right), Utawala wa Kanisa Kikatoliki (Supremacy of the Church), na Utawala wa Kabaila na Mkulima (Feudalism). Huu mfumo ulidumu kwa miaka mingi na hata watawaliwa waliupenda na kukubaliana nao, bila kuzingatia kwamba sehemu kubwa ya matatizo yao kwenye jamii yanatokana na vitu ambavyo wanavipenda na wanaamini hawawezi kuishi bila vyenyewe.

Wasomi aina ya Voltaire, Locke, Hobbes, Montesquieu, Galileo, Bacon, walipoanza kuuliza maswali mengi, walianza kuangaliwa kwa macho ya tofauti. Kwamba kwanini wanataka kushindana na ukweli ambao upo. Wasomi wengi waliuwawa, kufungwa na kuteswa na serikali zao zikishirikiana na Kanisa Katoliki. Ila mwishowe baada ya miaka mingi kupita, kikaja kizazi kipya mapinduzi makubwa yakafanyika dhidi ya mifumo.
======================================================


HATA HAPA TANZANIA, huwa nasema kwamba kizazi ambacho kinalalamika na hakiridhishwi na hali ya sasa ilivyo kinatakiwa kichukue hatua. Jambo la kushangaza ni kwamba kizazi hicho mbali na kulalamika na kupiga siasa za vyama hakuna kinachofanya. Tanzania haiwezi kubadilika kwasababu bado watu wengi wanaukumbatia WONGO. Hatutaki kukubali kwamba Mzee Nyerere alitengeneza MFUMO MBOVU, tangu siku ya kwanza anaingia Magogoni.

MSIDANGANYIKE, bila kukubali UKWELI Tanzania haiwezi kujinasua hapa ilipo. Ni lazima tukubali ukweli kwanza kwamba Mzee Nyerere alikosea na MFUMO aliotuachia ulikuwa MBOVU. Ukishakubali huu ukweli bila kukwepa (Deflecting) ndiyo macho yako yatafunguka na utaanza kuangalia Tanzania katika jicho la tofauti sana. Binafsi tangu niko sekondari nimekuwa nasoma vitabu vya UHURU NA UMOJA (FREEDOM & UNITY) ambavyo ni mkusanyiko wa hotuba za Mzee Nyerere tokea 1962.

Nimefika CHUO KIKUU ni MJAMAA kindakindaki. Nilikuwa siamini kabisa hata katika UTAJIRI jambo ambalo hadi watu wa nyumbani kwetu walikuwa wananishangaa. Darasani walikuwa wakimkosoa Mzee Nyerere hasa waalimu wetu ambao siyo watanzania nilikuwa naghafirika mno. Wakati niko chuo, ulikuwa ukiniambia twende leo tuchukue bunduki tuue matajiri wote, nilikuwa naweza hata kufanya bure bila mshahara. I WAS A DEVOUT COMMUNIST, kiwango ambacho nilikuwa sina mzaha kabisa na maisha.
======================================================


Mambo yalianza kubadilika baada ya kuanza kukutana na watawala wa Tanzania ambao ndiyo wako sehemu za maamuzi. Nikaanza kujiuliza maswali mengi sana. Kwanini mambo hayaendi kama yanavyotakiwa kwenda. Nikafahamu jambo moja baya sana. WATAWALA WOTE WA TANZANIA wana akili moja (A Herd Mindset/A Hive Mindset) ambapo dunia wanaitazaman katika kurunzi moja tu. Hahawezi kufikiri wenyewe jambo jipya. Mfumo mzima wa nchi, unatawaliwa na fikra za mtu ambaye amelela kule BUTIAMA.

Sasa hoja ambazo wafuasi wengi wa Mzee Nyerere wamekuwa wakizitoa pindi unawaambia ukweli ni hizi:

a) MZEE NYERERE ALIONDOKA MADARAKANI MIAKA 41 ILIYOPITA
Wakisahau kwamba Mzee Nyerere alitawala nchi kwa kutumia taasisi(Institutions). Siku zote taasisi zinaundwa na vitu muhimu kama Sera (Policies) na Sheria (Laws). Kwa pamoja, INSTITUTIONS+POLICIES+LAWS=SYSTEM. Bahati mbaya mno sera, sheria na taasisi nyingi ambazo zilitumika na Mzee Nyerere ndiyo zinaendelea kutumika mpaka leo hii Tanzania.

Mbaya zaidi. Wakati Tanzania inapata Uhuru, Mzee Nyerere alirithi MFUMO WA KIKOLONI ambapo aliendelea na taasisi na sheria za kikoloni. Unaposoma historia, moja ya jambo kubwa ambalo tunajifunza ni ESTABLISHMENT OF COLONIAL ECONOMY, ambapo jambo la kwanza kujifunza ni sifa kuu za dola la kikoloni (Features of A Colonial State), ambazo ni hizi zifuatazo: Exploitative in Nature (Dola la kinyonyaji), Pyramidal (Dola lenye matabaka) na Violent in Nature (Dola dhalimu na kandamizi).

Yote haya yaliwezeshwa na sheria na taasisi za kikoloni ambazo zilianzishwa na Wajerumani au Waingereza. Mzee Nyerere alipata nchi, sheria nyingi za kikoloni alibadilisha jina na kuendelea kuzitumia kutawala watanganyika. Sehemu walipoandika Governor yeye akaweka Prime Minister/President. Hili hata The Nyalali Commission ililisema kwa kina, tatizo ni kwamba watanzania ni watu wasiopenda kusoma na kudadisi vitu.

Huwezi kusema unatengeneza taifa la watu huru, ilhali bado unatumia taasisi na sheria za kikoloni kutawala. Hata kama una malengo mazuri, mfumo lazima utakuangusha. Taasisi za kiuasalama kama TPDF, PT, TISS zote zina mzizi kwenye ukoloni. Ndiyo maana hata zinapofanya mambo ya ajabu mimi sishangai kwasababu kimsingi lengo lake ni kulinda dola na siyo wananchi. Mabadiliko ya kitaasisi walau yalianza kufanyika kidogo kuanzia mwaka 1996-2015 chini ya Mkapa na Kikwete.

SASA KWANINI NASEMA HIVI: Kikawaida unapotaka kufanya mabadiliko makubwa kwenye nchi, jambo la msingi kabisa na kupambana na mfumo (Policies, Laws, Institutions and People/Gate-Keepers). Hii ndiyo sababu ya msingi kwanini mapinduzi yote huwa yamejaa vurugu na umwagikaji wa damu mkubwa. Wanamapinduzi huhakikisha kwamba wanabomoa mfumo wote pamoja na walinzi wake, kuanza kujenga upya tokea chini.

Mfano wa hili nalilisema ni kilichotokea nchini Ujerumani baada ya mwaka 1945, kilichoitwa THE DENAZIFICATION OF GERMANY, ambapo USSR, BRITAIN, FRANCE na USA waliigawanya Ujerumani vipande vinne ambavyo walivitawala kwa nguvu za kijeshi na kuhakikisha SERA, SHERIA, TAASISI na WALINZI WA MFUMO wanapukutishwa ndani na nje ya Ujerumani. Maelfu ya Wajerumani walihamishwa, wengine waliuwawa, na sheria mpya zikatungwa kuhakikisha kilichotokea mwaka 1933 chini ya Adolf Hitler hakirudii tena.

Mwaka 1991, wakati USSR inaanguka, ili Marekani kuzuia haya yanayoendelea leo dhidi yake alitakiwa ahakikishe taasisi kama KGB, GRU, CPSU, COM-INTERN zinavunjika na watu wake wanashughulikiwa vilivyo. Ila Marekani akasherehekea ushindi, na taasisi za USSR za kikomunisti na watu wake zikaendelea kuwepo huku zikiwa zimebadili majina tu. Watu waliokuwa na mawazo ya kuvamia Marekani na kuishambulia kinyuklia miaka ya 70's hawawezi kubadilika na kuanza kuwa marafiki zenu ndani ya usiku mmoja. Putin na genge lake la The Siloviki, ni WALINDA MFUMO WA USSR.

=========================================================================

Haya ni machache tu, ambayo siyo mimi ambaye nimeyaona, lakini hata wasomi nguli wa sheria nchi hii kama Jaji Nyalali, Jaji Lugakingira na Chris Maina wameyaona kuhusu Mzee Nyerere na mfumo wake aliourithi kutoka kwa mkoloni na kuutumia kuendesha Tanzania. Nafahamu fika kwamba haya ni magumu kumeza kwasababu FALSAFA ZA NYERERE zinawianishwa na TANZANIAN IDENTITY, ambapo watu wameaminishwa kwamba wakiachana nazo bado Utanzania ndiyo umekwisha na taifa litaparanganyika, jambo ambalo halina ukweli wowote ule.

=====================================================

b) TANGANYIKA HAIPO ISHAKUFA, KATIBA IMEUA TANGANYIKA
Hii ni moja kati ya hoja ya kipumbavu kabisa ambayo watu wasiokuwa na uelewa, ambao wengi wao ni wafuasi wa Mzee Nyerere, wana-CCM na Walinda Mfumo hupenda kuitumia kubeza au kukwepa ukweli. Wao wanaamini kabisa kwamba KATIBA YA MWAKA 1964 na ile ya mwaka 1977 imeiua Tanganyika.

Juu-Juu unaweza ukadhani kwamba hawa watu wana akili na hoja, lakini ukweli ni kwamba ni WAPUMBAVU SANA na hawana uelewa. Kikawaida sheria inayoanzisha taifa huanzishwa kupitia sheria za kimataifa (International Law) na sheria za ndani (Municipal Law) kwa pamoja. Huwezi kusema kwamba taifa limezaliwa au limekufa kwa kuangalia sheria za kimataifa peke yake (International Law) au sheria za ndani (Municipal Law) peke yake.

Kama ingekuwa ni hivyo basi dunia hii ingekuwa imejaa vurugu na sintofahamu maana leo hii taifa kubwa linaweza likaamka tu na kuamua kutambua kipande cha nchi husika kwamba ni nchi huru ili tu kuivuruga nchi husika. AU anaweza akamka tu mtawala ambaye hajaridhika na uchaguzi akaamua tu kutoa mkoa mmoja na kusema hii ni nchi yake huru. Haya hayapo, na ndiyo dunia inavyoenda, NI MPUMBAVU tu anaweza kupingana na UKWELI wa jinsi dunia inaenda.

KISHERIA SASA: Tanzania ni muunganiko wa mataifa mawili yaliyokuwa huru, Tanganyika na Zanzibar. Tanzania imeanzishwa kupitia mkataba wa kimataifa uitwao, ARTICLES OF THE UNION 1964, ambapo ukizingatia nchi ambazo zinafuata mfumo wa COMMON LAW kama yetu ambayo pia ni MONIST, lazima sheria hizi zipitishwe na bunge. Hivyo mkataba wa kimataifa uitwao ARTICLES OF THE UNION 1964 ambao ulisainiwa na Mzee Nyerere na Mzee Karume kwa lengo la kuunganisha haya mataifa mawili, ulipitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar ili iweze kuwa sheria ya nchi ambayo inaanzisha taifa jipya la Tanzania.

Baada ya maridhio (Ratifications) ARTICLES OF THE UNION 1964 ilitungiwa sheria iitwayo ACT OF THE UNION 1964 ambayo iliingizwa kwenye KATIBA YA TANZANIA ya mwaka 1965 kama ndiyo msingi wenyewe wa Jamhuri, ikiwa na mambo ya muungano (Union Matters) kumi na moja tu.

Hivyo basi, hapa tunaona kilichotumika ni sheria ya kimataifa (International Law) na sheria ya ndani (Municipal Law). Sasa basi wasomi nguli kama Prof Issa G Shivji wanasema kwamba ARTICLES OF THE UNION 1964 ni mkataba muhimu sana ambapo huwezi kubadilisha sheria ya nchi hasa katiba bila kuzingatia mambo ya msingi yaliyomo mle ndani. Hivyo kile kitendo cha kuondoa Tanganyika kwenye nyaraka zote za Muungano, Kufuta ACTS OF THE UNION kwenye katiba za Tanzania, na Kuongeza Mambo ya Muungano (Union Matters) kutoka 11 hadi 22 kinyemela ni jambo la kifedhuli, ambalo madhara yake watanganyika mnaanza kuyaona sasa baada ya wazanzibari kuanza kuyaona tokea mwaka 1964 wakiwaambia badilisheni ila mnajitia kichwa ngumu.
====================================================

SASA BASI: Kama Muungano wetu ulikuwa ni wa kimkataba, Tanganyika bado kwasababu uhalali wote wa Tanzania katika unatokana na ARTICLES OF THE UNION 1964 na ACTS OF THE UNION 1964, siyo maneno ya geresha ya WATANGANYIKA WASIOKUWA NA UELEWA.

Sheria za kimataifa zina kitu kiitwacho SOVEREIGNTY, ambayo ni nguvu ya dola kufanya mambo yake bila kuingiliwa na dola jingine, AU Kiingereza tunasema, "The ability to exercise state functions without interference of the third party". Tanzania ni nchi huru, A Sovereign State. Lakini, Sovereignty yake imegawanyika (Divisible) kwasababu Tanzania kama Dola kuu ndani yake kuna Dola jingine mwanachama, Zanzibar. Msomi nguli wa Sheria za kimataifa wa karne iliyopita Prof Herch Lauterpatch anayaita madola ya namna hii Composite States, ambayo huwa yanakuwa na uwezo wa kujiendesha yenyewe na kujiamulia mambo mengine yenyewe.

Hili kwenye sheria za kimataifa tunaliita INTERNAL SOVEREIGNTY, ambapo dola mwanachama linakuwa na uwezo wa kuendesha mambo yake ya msingi kama katiba inavyosema bila kuingiliwa na dola kuu. Sasa kitendo cha kukubali kwamba KATIBA YA MWAKA 1977, ina mambo ya muungano (Union Matters) na mambo yasiyokuwa ya muungano (Non-Union Matters) ni kukiri kabisa uwepo wa Tanganyika kama dola hai. Kuiita Tanganyika, Tanzania Bara na kusema itaamuliwa na Serikali Kuu hakuondoi ukweli wa uwepo wa Tanganyika.

====================================================

TANGANYIKA iko kisheria na haiwezi kuuwawa na KATIBA YA TANZANIA, kwasababu bila Tanganyika hakuna Tanzania. Tanganyika na Zanzibar kupitia ARTICLES OF THE UNION/ACTS OF THE UNION ndiyo zinaipa uhalali Tanzania kuwepo, siyo KATIBA. This is a very simple Legal Logic.

Hivi hamjiulizi maswali marahisi kabisa: KWANINI MZEE NYERERE na CCM wake walitumia na wanaendelea kutumia nguvu kubwa kuficha Mkataba wa Muungano (Articles of the Union). Kwasababu wanafahamu ukweli, kwamba pindi mambo yatakapokuwa wazi hawatakuwa na chao hapa. Hivyo kuendelea kupumbaza watanganyika ni kuwavalisha uhusika mwingine (UTANZANIA) ambao utawalazimisha wakumbatiane na WAZANZIBARI kiutendaji.

UTANGANYIKA unafichwa kwasababu, kanuni rahisi kabisa ambayo mkoloni aliitumia duniani kote ili kufanikiwa kutawala watu, ni kuhakikisha unafuta historia yake na kukijaza kizazi kipya kujichukia wenyewe. Hii ni mbinu ya kikoloni ambayo imefanikiwa kufanya kazi kwa asilimia 10000000000% kwenye akili za watanganyika.

LEO HII, wanaoongoza kwa kulilia na kulazimisha huu MUUNGANO uendelee kuwepo ni WATANGANYIKA. Wao wanasema usivunjike ila twende kwenye serikali MOJA ilhali ukweli mchungu ni kwamba upande wa pili wa MUUNGANO, wazanzibari hata hawawachukulii ninyi kama ndugu, isitoshe binadamu.

=======================================================

KISIASA ni rahisi sana kuuongelea huu MUUNGANO, lakini ukizingatia UKWELI, utafahamu kwamba Tanzania ilivunjika miaka ya 60's na kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni geresha tu. Ndiyo maana kuna wakati Ndugu Tundu Lissu aliwahi kusema kwamba "Zanzibar ni koloni la Tanganyika" jambo ambalo lilitukera wengi hata ambao siyo wafuasi wa Muungano. Kuchonganisha watanganyika na wazanzibari wa kawaida unapata faida gani ???

Kiukweli ukiuliza watanganyika wa kawaida wananufaikaje na muungano ambao hawakuubariki unabakia na ukakasi. Kusema kwamba Zanzibari ni Koloni la Tanganyika ni kuleta taharuki na chuki baina ya watu wa kawaida. Baadaye huyohuyo Lissu akaanza kudai kwamba "Mzanzibari anauza mali za Tanganyika", ghafla Zanzibar siyo koloni tena.

Niliwaza sana na kufikia hitimisho kwamba, MKAKATI WA NYERERE unaendelea kufanya kazi, kwasababu MFUMO WA MUUNGANO umewachanganya akili watu kama Lissu. Matatizo yanayoendelea hapa, siyo UTANZANIA au UZANZIBARI, bali ni mfumo ulioachwa unaowapa nguvu watawala kufanya wanachojitakia. Mali za Tanganyika zimeuzwa tangu Mwinyi, Mkapa na Kikwete, huyu Samia anaendelea kufanya alichoona watangulizi wake wanafanya. HAKUNA JIPYA

=========================================================

HITIMISHO: Watanganyika hawawezi kupata mabadiliko ilhali hawataki UKWELI.

UKWELI huanzia pale tunapofahamu tatizo lilianzia kwa nani na lini. Tukishalifahamu hili ndiyo tunaanza kuchunguza historia ya kipindi chote hichi na kuweza kutengeneza dawa yake, na jinsi ya kufanya matibabu

JAPO, naamini Tanganyika haiwezi kubadilishwa na kizazi cha 1940-1950's, 1960-1980's. Walau watakaoweza kubadilisha Tanzania ni wale wa kizazi kipya cha 1990's kuendelea mbele. Hawa ndiyo wako radhi kuusikia ukweli kama ulivyo na ndiyo wahanga wakubwa wa UJINGA na UFEDHULI uliofanywa na vizazi vilivyopita.

Binafsi huwa naamini mabadiliko yatakuja, ila yatakuja kwa maumivu makali sana. Tena sanaaa. Tanzania ambayo mlikuwa mnaifahamu ilishajifia tayari, na kilichotokea 29 Oktoba 2025 ilitakiwa iwe UAMSHO TOSHA kwamba kama watawala wanaweza kuua watoto wenu kwa maelfu bila kuwajibika na kutupa maiti zao kama wanyama, na kuendelea kuwasimanga marehemu na wafiwa, basi fahamu fika hapo HAKUNA NCHI.

MKIENDELEA KUBISHA na KUSHUPAZA SHINGO, siku nyingine mtaendelea kushuhudia misiba mikubwa mpaka akili ziwakae sawa na mchukue hatua. UKWELI ni kwamba nchi yetu ina msingi mbaya ambao bila kurekebisha hatuwezi kufika popote. Lazima tuanze kukubali ukweli huu ndiyo mengine yafuate.

ENIWEI sijui kama tutaelewana......
​
Asante Sana hii nasubiria kusoma Weekend.
 
@MALCOMLUMBA ujanja mwingi mbele Giza ndo kilimkuta Nyerere
Ukiangalia vizuri harakati zote za Mwl ilikuwa ni kukilinda Chama, alipenda chama kuliko Nchi

Kuna watu wanadai eti alisaidia Nchi za kusini mwa Afrika kupata Uhuru, wasichoelewa malengo ya Mwl ni kutaka kuwa Rais wa Afrika nzima, alijifunza hizi mambo huko Ulaya mashariki na walimpa support kubwa ni vile tu malengo hayakutimia
 
Mzee Nyerere kabla hajafariki alihujumu mchakato wa kidemokrasia katika ngazi za kichama na ngazi za kitaifa, kulazimisha Mzee Mkapa awe Raisi na CCM iendelee kubaki madarakani kimabavu ilhali ilikuwa ishapoteza mwelekeo. Aliwadhuru watu waliopingana na mawazo yake. Kina Kolimba na Kombe walipoteza maisha kisa Nyerere's Fragile EGO.
You must be out of your mind; totally out of order.

State the basis of such wild imaginations.

I was almost going to give you the benefit of the doubt in some of your rabid imaginations; but this is totally out of the whack!
 
HOJA KUU, ambayo huwa ina mashiko ni kwamba Mzee Nyerere miaka ya 1961-1964 alikuwa na mahusiani mazuri na U.K na USA. Baada ya The Cuban Missile Crisis 1962, wao ndiyo walimshurutisha na kumshawishi aivute Zanzibari ili kuzuia UKOMUNISTI wa USSR
Kuna ugumu gani kujuwa kuwa Karume na wenzake walikuwa na hofu kubwa juu ya waliowapindua na kutafuta mwavuli kwa Tanganyika.
Na hata kama hilo halitoshi, huwezi kuelewa kuwa enzi hizo swala la kuungana lilikuwa ni ajenda muhimu katika nchi za kiaafrica? Hujawahi kusikia lengo la kutaka kuwepo muungano wa nchi za Afrika mashariki?
Kuna ajabu gani ya Tanganyika kuungamna na Zanzibar wakati huo kwa lengo hilo hilo?
 
Baada ya miaka 50. Wasaouth Africa wataenda kunya ktk kaburi la Mandela kama halitakuwa na ulinzi. He betrayed all of his fellow fighters compromising with the oppressor in the question of land and so many others. Time will tell.
Dah!
You really have the audacity of telling it as it is!

Mandela alikuwa 'mishandled' mara tu alipotoka gerezani. Alidakwa na kundi lililomvuruga akili. Hili ni kundi lililokuwa limejiandaa vyema sana kumwondoa kwenye reli.
Wengi ndani ya kundi hilo walikuwa ni watu toka nje ya Afrika Kusini.
 
Dah!
You really have the audacity of telling it as it is!

Mandela alikuwa 'mishandled' mara tu alipotoka gerezani. Alidakwa na kundi lililomvuruga akili. Hili ni kundi lililokuwa limejiandaa vyema sana kumwondoa kwenye reli.
Wengi ndani ya kundi hilo walikuwa ni watu toka nje ya Afrika Kusini.
Sure he compromised alot of issues. Wapo mpka waliosema he was cloned kwa kuwa walimuona mtu wa misimamo tofauti. Kwa kuzidi kumchanganya akafanyiwa birthday London na akapewa kombe la dunia. Akajiona king kumbe wazungu wanazidi kumdidimiza.
 
Back
Top Bottom