DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 551
...Dah, hata harufu yake naikumbuka.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
...Dah, hata harufu yake naikumbuka.
Kukusanya kodi wapi tufahamishe tupate darsa kidogo.KIkubwa alichofeli ni KUKUSANYA KODI na ndipo ilimbidi Mkapa alipoingia aanzishe TRA.
RUKSA RUKSA ilikuwa RUKSA kwlei kweli watu walikuwa wanahela mbaya na vitu vilipatikana kwelikweli.( Mfano w ahili ni show ya Kanda Bongo Man ndani ya Kilimanjaro Hotel Miaka hiyo ya 90 kiingilio ilikuwa 100,000/= na bado ilijaza)
Nyerere alimpiga dongo sana kuwa anashahuriwa na Mkewe au tuseme wake zake.
...NMC hiyo! Huo mkate ulikuwa lulu, kwa sie wengine!home mkinywa chai na mkate wa siha/boflo mnaoneka matajiriii hakika kipindi hicho sitokaa nikisahau
viongozi wa hii nchi wapowapo tu. mambo tunayowasifia yametokea kingekewa na siyo by design. kuingia kwenye demokrasia na kubadili sera za uchumi ni kutokana na mashinikizo ya WB na IMF. hao ndiyo ditch designers, wakina Mwinyi ni ditch diggers tu, wafuata upepo. hatuna viongozi wenye maono. kidogo Nyerere alikuwa nayo.Kisiasa, Uongozi wa Mwinyi ulifanikiwa katika mambo makuu mawili; kufunguliwa kwa milango ya demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari. Dhana ya demokrasia, japo haikutumika katika chaguzi za kipindi chake, lakini angalau miaka miwili kabla ya kuondoka madarakani nchi ilifungua mlango wa demokrasia ambapo siasa za vyama vingi zilianza wakati yeye akiwa madarakani.Kwa pamoja na Uhuru wa Vyombo vya habari, nchi ikajenga mazingira mapya kutoka yale ya utawala usiokosolewa kuja utawala uliokosolewa hadharani. Kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa demokrasia ya Rais kuchorwa na kusemwa vibaya.
Vijana wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam wao walifikia hatua mbaya zaidi pale walipoifuja demokrasia hiyo kwa kuchora picha za matusi dhidi ya Rais Ali Hassan. Kama tutakavyoona katika kipengele cha elimu, Mwinyi alileta nafuu kubwa ya maisha ya Wanataaluma Chuoni hapo.
Japo wanataaluma walianza kuonesha mfano mbaya wa matumizi ya uhuru wa kujieleza ambao haukuwepo enzi za Nyerere lakini bado Mwinyi hakufunga mlango wa demokrasia.
Kwa mara kwanza tangu miaka ya 1960, Watanzania wakaanza kushuhudia majukwaa ya upinzani dhidi ya Chama tawala na serikali. Ukizungumzia mwanzo wa mageuzi ya kisiasa basi lazima utayakuta ndani ya kipindi cha Mwinyi.
Kama kuna eneo lililoung’arisha mapema utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi basi lilikuwa ni lile la Uchumi. Mwinyi aliaswa na wataalamu wa uchumi kuwa aachane kabisa na fikra zilizoshindwa na Mwalimu Nyerere kama alitaka kufanikiwa katika eneo hili.
Legacy?!? ni IPI?! Labda ya kuiporomosha nchi na Mkapa kuja kuiinua. Ni kama JK alivyoiangusha na sasa JPM anavyohaha kuiinua.
na amini kabisa kama mngevaa matairi ya magari miguuni na kujifunga kaniki na mawingu na waume zenu kuvaa zile nguo za kaki zisizo na kola na kupanga foleni kwenye duka moja (tu) la kijiji kununua mche moja wa sabuni, kipimo kimoja cha mafuta ya taa, kiberiti kimoja na kipakti kimoja cha chumvi (tena isiyo na iodine) wala msingeandika haya.Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
...Hapa tukubaliane tu, Mzee wetu kwenye suala la kodi, hakujishughulisha kihivyo. Serikali ilifika wakati ikawa imekauka fedha, ila mtaani, imejaa tele.Kukusanya kodi wapi tufahamishe tupate darsa kidogo.
kabla ya kuingia mzee ruxa bidhaa zilipatikana kwa tabu sana,nadhani ni baada ya mwinyi kukubaliana na mpango wa National economy Recovery programme ndo nchi iliianza kurecover,ikifuatiwa na ule mpango wa structual Adjustiment Programme,Foleni zilikuwa za kusukumana kwani watu walikuwa wengi kuliko bidhaa. Ndiyo kusema, wengine walirudi nyumbani mikono mitupu baada ya jitihada za kusukumana ili kulifikia dirisha la duka kushindikana. Wengine walizirai kwenye foleni! Ugumu hasa ulikuwa katika kupata sukari au mchele uliokuja kwa nadra.
Teh teh teh
Tulishaliona hilo siku nyingikwa ninavyoona na kulinganisha awamu kuanzia Nyerere hadi magufuli naona kunatokea circles
yaani Kubana(Nyerere)-Huria(Mwinyi)-Kubana(Mkapa)-Huria(Kikwete)-Kubana(Magufuli)
ila historia ya Mwinyi imefichwa kidogo sasa naomba wadau mfunguke vizuri plz
Mbatia na genge lake waliongoza harakati za kumchora mzee ruksaKisiasa, Uongozi wa Mwinyi ulifanikiwa katika mambo makuu mawili; kufunguliwa kwa milango ya demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari. Dhana ya demokrasia, japo haikutumika katika chaguzi za kipindi chake, lakini angalau miaka miwili kabla ya kuondoka madarakani nchi ilifungua mlango wa demokrasia ambapo siasa za vyama vingi zilianza wakati yeye akiwa madarakani.Kwa pamoja na Uhuru wa Vyombo vya habari, nchi ikajenga mazingira mapya kutoka yale ya utawala usiokosolewa kuja utawala uliokosolewa hadharani. Kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa demokrasia ya Rais kuchorwa na kusemwa vibaya.
Vijana wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam wao walifikia hatua mbaya zaidi pale walipoifuja demokrasia hiyo kwa kuchora picha za matusi dhidi ya Rais Ali Hassan. Kama tutakavyoona katika kipengele cha elimu, Mwinyi alileta nafuu kubwa ya maisha ya Wanataaluma Chuoni hapo.
Japo wanataaluma walianza kuonesha mfano mbaya wa matumizi ya uhuru wa kujieleza ambao haukuwepo enzi za Nyerere lakini bado Mwinyi hakufunga mlango wa demokrasia.
Kwa mara kwanza tangu miaka ya 1960, Watanzania wakaanza kushuhudia majukwaa ya upinzani dhidi ya Chama tawala na serikali. Ukizungumzia mwanzo wa mageuzi ya kisiasa basi lazima utayakuta ndani ya kipindi cha Mwinyi.
Kama kuna eneo lililoung’arisha mapema utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi basi lilikuwa ni lile la Uchumi. Mwinyi aliaswa na wataalamu wa uchumi kuwa aachane kabisa na fikra zilizoshindwa na Mwalimu Nyerere kama alitaka kufanikiwa katika eneo hili.
angekusanyaje kodi wakati amekuta serikali haina hela na wananchi hawana hela? cha kwanza alichofanya Mwinyi kupitia kushauriwa na akina Prof. Lipumba ni kuwajaza mahela wananchi. katika miaka 10 aliwawezesha sana wananchi kujijenga kiuchumi na kila aliyeweza alipiga hatua kimaendeleo kadiri alivyojituma. Na ndipo alipokuja Mkapa na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji kodi kama vile TRA, VAT nk kwa sababu tayari wananchi walishawezeshwa kiuchumi. kwa hiyo Mwinyi asingeweza kukusanya kodi hasa pale mwanzoni mwa uongozi wake kwa sababu wananchi hawakuwa na kitu kabisa....Hapa tukubaliane tu, Mzee wetu kwenye suala la kodi, hakujishughulisha kihivyo. Serikali ilifika wakati ikawa imekauka fedha, ila mtaani, imejaa tele.
...Kimsingi nakubaliana na hoja yako ya kufufua uchumi, ila, kodi ilipaswa kukusanywa kwa kiasi fulani.
Mkuu nakubaliana nawe!! lakini wakati huo TZ ilikuwa inatoka ktk Comminiisum/inatoka ICU yaani mgonjwa bado yupo wodini..hivyo Dokta huumba miiko na matibabu kwa dawa chungu !!Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
sio kweli kuwa Mkapa alikuta watu wachache amabo ni taxable bali walikuwa wengi tu wa kutosha.Wanaomlaumu Mwinyi kutokusanya Kodi, Ni Tax base gani iliyokuwepo baada ya Mwinyi kuingia Madarakani?, kulikuwa kuna viduka vya Wahindi tu.
Alichokifanya Mwinyi ni kuwawezesha wananchi wawe na kipato, ili wenye kuanzisha biashara waanze, Then unatoa Tax Incentive kwa kutowatoza kodi ili Biashara zikomae, then Ukishapata watu wa kutosha wa kuwatoza kodi Unaanza kuwatoza kodi.
Mkapa alipoingia Madarakani angalau aliwakuta watu wachache ambao ni Taxable, ambao walipata utajiri wao kipindi cha Mwinyi. Mzee Mwinyi hakuwa na Privilege hii, alikuta nchi hohehahe na wananchi hohehahe Angekusanya kodi kutoka kwa nani?
Legacy ingine ni kumuibua JK toka Masasi akiwa Katibu wa CCM Wilaya kumteua Naibu Waziri maana alishasahaulika kama si yale mafuriko ya Masasi na J S Warioba kumuombea msamaha..........Alipokea kijiti cha uongozi wakati nchi ikiwa katika hali ngumu mno kiuchumi.
Sijui kama ulikuwepo kipindi hicho mkuu.
Kama ungekuwepo sijui kama ungeandika hayo uliandika labda kama unaleta ubishi na ushabiki sawa.
kipindi mwinyi anachukua nchi asilimia 90 ya mashirika yalikuwa ni ya umma na yalikuwa yanakufa,watu walikuwa wanamzunguka nyerere na kuyamaliza mashirika ya umma kwahiyo ukusanyaji kodi usingekuwa mkubwa kama wa awamu zilizofuata,...Hapa tukubaliane tu, Mzee wetu kwenye suala la kodi, hakujishughulisha kihivyo. Serikali ilifika wakati ikawa imekauka fedha, ila mtaani, imejaa tele.
...Kimsingi nakubaliana na hoja yako ya kufufua uchumi, ila, kodi ilipaswa kukusanywa kwa kiasi fulani.
kipindi cha mkapa sawa walikuwa wameshaanza kukomaa kulipa kodi,kipindi cha mwinyi hao kina barheresa walikuwa bado ndo wanaanza kumiliki mashine za kawaida tu za kusaga nafaka,sio kweli kuwa Mkapa alikuta watu wachache amabo ni taxable bali walikuwa wengi tu wa kutosha.