Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

mkuu,mbona utawala huu una viashiria vyote vya uko mliko kuwa!hivi tukianza kupanga foleni,wala chipsi na chili sosi wataweza kupimana ubavu na wala miogo,sembe,magimbi na ugari wa muhogo?ee Mungu epushia mbali!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji123] [emoji123]
 
...Hapa tukubaliane tu, Mzee wetu kwenye suala la kodi, hakujishughulisha kihivyo. Serikali ilifika wakati ikawa imekauka fedha, ila mtaani, imejaa tele.

...Kimsingi nakubaliana na hoja yako ya kufufua uchumi, ila, kodi ilipaswa kukusanywa kwa kiasi fulani.
Angekusanya kodi kutoka kwa kina nani hao wafanyabiashara walikuwa wapi wakuwabana walipe kodi kipindi hicho.

Sukari, mchele, sabuni za kufulia na kuogea, sigara, dawa za mswaki vyote vikapatikana kwa mwendo wa kuruka. Si hivyo tu, bali ilifika mahala hata magodaoni ya Shirika la Ugawaji yakaishiwa kabisa, na kubaki na maharage yasiyowiva hata ukitia maji mara kumi na mbili!.

Karibu bidhaa zote za viwanda ziliadimika kwa sababu hatukuwa na uzalishaji wa kutosha wa ndani, na mipaka ilifungwa kisiasa na kuzuia bidhaa za nje. Sekta ya Umma aliyotumia Nyerere kuzalisha bidhaa ilifeli vibaya.

Viwanda vyote havikudumu kwa sababu ya kukosa tija. Wananchi walivaa nguo mbovu, na za viraka au kama zilivyoitwa wakati ule ‘midabwada’. Walivaa makatambuga kama yale ya wamasai kwa sababu ya kukosekana kwa viatu.
 
kuhusu legacy sijui kitu kwani zamani tulikuwa tunapigia kivuri, yeye wa enzi za kupiga kura za kivuli vuli.
 
Poleni sana wazee wetu mmetoka mbali sana tunaomba jpm asiturudishe kwenye zama hizo mlizopitia vijana wengi tutakufa kwa mawazo
 
viongozi wa hii nchi wapowapo tu. mambo tunayowasifia yametokea kingekewa na siyo by design. kuingia kwenye demokrasia na kubadili sera za uchumi ni kutokana na mashinikizo ya WB na IMF. hao ndiyo ditch designers, wakina Mwinyi ni ditch diggers tu, wafuata upepo. hatuna viongozi wenye maono. kidogo Nyerere alikuwa nayo.
Haukuwepo wakati wa utawala wa Nyerere wala wa Mwinyi ndiyo maana unasema hayo yote kirahisi.

Taifa lilihitaji mtu wa aina ya Mwinyi mapema. Laiti Mwinyi ndio angeanza mwaka 1961, Tanzania ingekuwa mbali sana kimaendeleo, na ingezitimulia vumbi nchi jirani ikiwemo Kenya inayoonekana kutushinda kwa kila kitu isipokuwa siasa za majukwaani.

Muda mfupi tu baada ya Mwinyi kuingia madarakani na kubadili mtazamo wetu wa kiuchumi, mambo yakaanza kubadilika kiasi cha kuwashangaza watu. Magenge ya ulanguzi yakatoweka baada ya bidhaa kupatikana kwa wingi.
 
Kama Nyerere of all the People alikubali Mtanzania avae nguo za Mtumba ( nguo aliyokwisha vaa mzungu) basi ujue utawala wake ulikuwa umeelemewa!. Mzee Ruksa alikuwa hana jinsi isipokuwa kuufungua uchumi!
 
Wa Tanzania ni watu wasiyo tabirika au wakutegemewa tunapenda kulalama na kuteta baadae

raisa wa kwanza JKN kaongoza kwa uwezo wake wote...
rais wa pili AHM kaongoza kwa uwezo wake wote...
rais wa tatu BWM kaongoza kwa uwezo wake wote...
rais wa nne JMK kaongoza kwa uwezo wake wote...
rais wa tano JPM Anatuongoza kwa juhudi zake zote...

Yapo mazuri ,mema faida na karaha na mbaya...
 
Yaani nashangaa mazuri yote hayo mnayosema kuhusu uyo mzee
Maana sijaona serekari hata mashuleni kufundisha historia ya uyo MTU
Yaani alivyosahauliwa utafikiri aliipeleka nchi kuzimu
 
Kama Nyerere of all the People alikubali Mtanzania avae nguo za Mtumba ( nguo aliyokwisha vaa mzungu) basi ujue utawala wake ulikuwa umeelemewa!. Mzee Ruksa alikuwa hana jinsi isipokuwa kuufungua uchumi!
Rukhsa ya Rais Mwinyi ikawa na manufaa makubwa kuliko shari ya kufunga mipaka aliyokuwa nayo mtangulizi wake.
 
Yaani nashangaa mazuri yote hayo mnayosema kuhusu uyo mzee
Maana sijaona serekari hata mashuleni kufundisha historia ya uyo MTU
Yaani alivyosahauliwa utafikiri aliipeleka nchi kuzimu
historia si ndo hii tunayoandika hapa?.
Au unataka ya darasani?
Subiri miaka ijayo outomatically hiyo historia itaingia kwenye mitaala
 
Yaani nashangaa mazuri yote hayo mnayosema kuhusu uyo mzee
Maana sijaona serekari hata mashuleni kufundisha historia ya uyo MTU
Yaani alivyosahauliwa utafikiri aliipeleka nchi kuzimu
historia si ndo hii tunayoandika hapa?.
Au unataka ya darasani?
Subiri miaka ijayo outomatically hiyo historia itaingia kwenye mitaala
 
Wanaomlaumu Mwinyi kutokusanya Kodi, Ni Tax base gani iliyokuwepo baada ya Mwinyi kuingia Madarakani?, kulikuwa kuna viduka vya Wahindi tu.

Alichokifanya Mwinyi ni kuwawezesha wananchi wawe na kipato, ili wenye kuanzisha biashara waanze, Then unatoa Tax Incentive kwa kutowatoza kodi ili Biashara zikomae, then Ukishapata watu wa kutosha wa kuwatoza kodi Unaanza kuwatoza kodi.

Mkapa alipoingia Madarakani angalau aliwakuta watu wachache ambao ni Taxable, ambao walipata utajiri wao kipindi cha Mwinyi. Mzee Mwinyi hakuwa na Privilege hii, alikuta nchi hohehahe na wananchi hohehahe Angekusanya kodi kutoka kwa nani?
Viwanda vya nguo vilikuwepo bana
 
Mwinyi alifanya economic reforms na kuja na open up policy kwa kufungua milango ya kiuchumi Tanzania. Hili lilifanywa na nchi nyingi kipindi hicho japo Tanzania ilichelewa sana. China kwa mfano Deng Xiaoping miaka ya 1978 alileta sera hii baada ya Chairman Mao Zedong kufariki, na hii ndio inasemwa kuwa ndio Turning point ya uchumi wa China ambayo ilijenga misingi ya maendeleo waliyonayo leo.

Hivyo wakati Mwinyi akifungua milango hii kwa nia njema, huwenda hakuwa na wasimamizi na watekelezaji wazuri na bobevu lakini hii ilikuwa ni turufu kubwa sana ambayo pengine leo tungekuwa tunazungumza mengine. Wakati China ikitengeneza uchumi wa kibepari wenye sifa za kisoshalisti Tanzania sisi tuliingia katika uchumi wa kibepari moja kwa moja!

Legacy ya mzee ruhusa ni kubwa sana kwa sababu aliichukua nchi ikiwa katika kipindi kigumu mno cha uchumi uliokufa kabisa kuliko raisi yoyote aliyefuatia baada yake. Ni kama vile alipewa "yatima" amlee ambae hana "nguo" wala "chakula" wala "pakulala".

Alijitahidi mno. na ni kipindi hiki ndipo biashara zilianza kuibuka na bidhaa zikapatikana hasa zile bidhaa msingi ambazo wakati wa nyuma zilipangiwa foleni asubuhi mpaka jioni, kuanzia sukari , nguo, dawa ya meno nk.

Kila zama na kitabu chake, kulinganishi kipindi chake na sasa kisha eti kumkosoa kuwa hakufanya kitu ni kutokumtendea haki. Alifanya kwa nafasi yake na kutokana na changamoto za wakati wake. Na laiti waliomsaidia wangemuunga mkono na pia waliofuatia kama wangeboresha zaidi pale alipoachia kwa kuweka sera endelevu na miapango ya mda mrefu, Tanzania ingekuwa "China" ya leo!

Hongera mzee Mwinyi ulifanya yako kwa wakati wako.
 
Viwanda vya nguo vilikuwepo bana
Viwanda vyote havikudumu kwa sababu ya kukosa tija.

Ni kweli viwanda kama Mwatex, Mutex vilikuwepo mwisho wa mwezi wafanyakazi badala ya kupewa mishahara wanapewa carton za kanga na vitege wakauze ili wapate pesa soko hamna wananchi hawana vipato.

Mipaka ilifungwa kisiasa na kuzuia bidhaa za nje. Sekta ya Umma aliyotumia Nyerere kuzalisha bidhaa ilifeli vibaya hamna wa kumuuzia.
 
Mungu akupe maisha marefu na afya tele mzee wetu mzee ruksa iliikuta nchi iliyokuwa hohe hae inchi imejichokea na sera za ujamaa kila kitu foleni na hata ukiunga foleni huna hakika ya kupata bidhaa lakini ukaja ukaufungua mlango wa ruksa hakika ruksa ikaifaa sana nchi yetu.
Kipindi kile nchi ilihitaji kiongozi mwenye haiba yako ukaamua kwenda kinyume na asili ya ujamaa ili inchi ipone hakika baadhi ya mazuri ambayo tunayashuhudia hadi leo yalitokana na jasho lako.
Uliyafanya haya kwa ujasiri japo haiba yako yaonekana ya upole ila ulifanikiwa kuivusha nchi katika kipindi kigumu kweli kweli.

Nakumbuka ukituaga kwenye hutuba yako ukatuambia "MABAYA YANGU NIACHIENI LAKINI MAZURI YANGU TUGAWANE". Hakika ni kweli leo mazuri yako tunagawan.

Hongera sana mzee ruksa mola aendelee kukupa afya njema na miaka mingi zaidi.
 
Back
Top Bottom