comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,950
Open door was brilliant sana , yaani kwa kweli neema ndogo na kubwa zilionekana, Live long ex- president
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Legacy?!? ni IPI?! Labda ya kuiporomosha nchi na Mkapa kuja kuiinua. Ni kama JK alivyoiangusha na sasa JPM anavyohaha kuiinua.
Nina hakika hukiwepo kipindi chake usingeliandika hivi. waulize wazee wako waliopitia enzi za mwl na za mzee ruksa halafu ndio uje hapa. Hakuna raisi aliepita kipindi kigumu cha kuongoza nchi kama yeye. Wanaolalamika kiwa alishusha uchumi.watuambie aliushusha kutokea wapi?kwa sababu uchumi tayari ulikuwa taabani!Alkua anaambiwa na WB na IMF Nate anatimiza so hapakuwa na ujuzi wala ubunifu kupigia mfano!! Ruhusu demokrasia- sawa! ruhusu soko huria-sawa! nk. nk. Kuhusu legacy may be that but for me there was nothing best in particular!
Mungu akupe maisha marefu na afya tele mzee wetu mzee ruksa iliikuta nchi iliyokuwa hohe hae inchi imejichokea na sera na siasa muflis za ujamaa kila kitu foleni na hata ukiunga foleni huna hakika ya kupata bidhaa lakini ukaja ukaufungua mlango wa ruksa hakika ruksa ikaifaa sana nchi yetu.
Kipindi kile nchi ilihitaji kiongozi mwenye haiba yako ukaamua kwenda kinyume na asili ya ujamaa ili inchi ipone hakika baadhi ya mazuri ambayo tunayashuhudia hadi leo yalitokana na jasho lako.
Uliyafanya haya kwa ujasiri japo haiba yako yaonekana ya upole ila ulifanikiwa kuivusha nchi katika kipindi kigumu kweli kweli.
Nakumbuka ukituaga kwenye hutuba yako mwaka 1995 ukatuambia"MABAYA YANGU NIACHIENI LAKINI MAZURI YANGU TUGAWANE".hakika ni kweli leo mazuri yako tunagawana hatuungi tena foleni kupata mafuta,mkate unga wala sukari.
Hongera sana mzee ruksa mola aendelee kukupa afya njema na miaka mingi zaidi.
Unaambiwa hakukua na habari kuwa nimeota kumbe umeangalia tv chumbani peke yakoWengi hapa wameweza kuona tv wakati wa Mzee Mwinyi.
Kila kiongozi kama binadamu anayo mazuri yake na mabaya yake
You have tried to your best to answer the question Bila KUJITOA ufahamu. That is maturity [emoji106] [emoji817] [emoji818]Kisiasa, Uongozi wa Mwinyi ulifanikiwa katika mambo makuu mawili; kufunguliwa kwa milango ya demokrasia na Uhuru wa Vyombo vya Habari. Dhana ya demokrasia, japo haikutumika katika chaguzi za kipindi chake, lakini angalau miaka miwili kabla ya kuondoka madarakani nchi ilifungua mlango wa demokrasia ambapo siasa za vyama vingi zilianza wakati yeye akiwa madarakani.Kwa pamoja na Uhuru wa Vyombo vya habari, nchi ikajenga mazingira mapya kutoka yale ya utawala usiokosolewa kuja utawala uliokosolewa hadharani. Kwa mara ya kwanza ikashuhudiwa demokrasia ya Rais kuchorwa na kusemwa vibaya.
Vijana wa Chuo Kukuu cha Dar es Salaam wao walifikia hatua mbaya zaidi pale walipoifuja demokrasia hiyo kwa kuchora picha za matusi dhidi ya Rais Ali Hassan. Kama tutakavyoona katika kipengele cha elimu, Mwinyi alileta nafuu kubwa ya maisha ya Wanataaluma Chuoni hapo.
Japo wanataaluma walianza kuonesha mfano mbaya wa matumizi ya uhuru wa kujieleza ambao haukuwepo enzi za Nyerere lakini bado Mwinyi hakufunga mlango wa demokrasia.
Kwa mara kwanza tangu miaka ya 1960, Watanzania wakaanza kushuhudia majukwaa ya upinzani dhidi ya Chama tawala na serikali. Ukizungumzia mwanzo wa mageuzi ya kisiasa basi lazima utayakuta ndani ya kipindi cha Mwinyi.
Kama kuna eneo lililoung’arisha mapema utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi basi lilikuwa ni lile la Uchumi. Mwinyi aliaswa na wataalamu wa uchumi kuwa aachane kabisa na fikra zilizoshindwa na Mwalimu Nyerere kama alitaka kufanikiwa katika eneo hili.
Hakuwa na zuri?Mimi ninayokumbuka wakati wa Mwinyi ni haya;
Mengine nawaachia...
- Rukhsa, nchi kugeuzwa kokoro
- Kaburi la Azimio la Arusha
- Kupotea kwa tausi viwanja vya Ikulu na Karimjee
- Kushuka kwa hadhi ya Ikulu
- First Lady kuitwa shemeji
- Kuzuka kwa mihadhara ya kidini
- Mgogoro wa Loliondo na Waarabu
- Mwanzo wa biashara ya Wanyama
- Ukwepaji wa kodi kushika kasi
- Mwanzo wa kuingia mikataba mibovu
- Kuzaliwa kwa IPTL, hadi leo inatutafuna.
- Kutothaminiwa kwa wasomi na wataalamu
- CCM kutekwa na wafanyabiashara na walanguzi.
- Kampuni za mfukoni na utapeli kushika kasi
- Nchi kuendeshwa kwa mtindo wa yupo yupo
Mkuu Ritz naomba legacy ya aliempa kijiti Mzee ruksa nakusudia legacy ya Nyerere.Alipokea kijiti cha uongozi wakati nchi ikiwa katika hali ngumu mno kiuchumi.
Sijui kama ulikuwepo kipindi hicho mkuu.
Kama ungekuwepo sijui kama ungeandika hayo uliandika labda kama unaleta ubishi na ushabiki sawa.
Nilitaka kushangaa usingejitokeza kwenye huu uzi haya mbona umeyasahu.Mimi ninayokumbuka wakati wa Mwinyi ni haya;
Mengine nawaachia...
- Rukhsa, nchi kugeuzwa kokoro
- Kaburi la Azimio la Arusha
- Kupotea kwa tausi viwanja vya Ikulu na Karimjee
- Kushuka kwa hadhi ya Ikulu
- First Lady kuitwa shemeji
- Kuzuka kwa mihadhara ya kidini
- Mgogoro wa Loliondo na Waarabu
- Mwanzo wa biashara ya Wanyama
- Ukwepaji wa kodi kushika kasi
- Mwanzo wa kuingia mikataba mibovu
- Kuzaliwa kwa IPTL, hadi leo inatutafuna.
- Kutothaminiwa kwa wasomi na wataalamu
- CCM kutekwa na wafanyabiashara na walanguzi.
- Kampuni za mfukoni na utapeli kushika kasi
- Nchi kuendeshwa kwa mtindo wa yupo yupo
Mkuu wangu Legacy ya Nyerere inaitaji uzi wake nakushauri fungua uzi tutakuja kuchangia kiduchu.Mkuu Ritz naomba legacy ya aliempa kijiti Mzee ruksa nakusudia legacy ya Nyerere.
Leo upo sawa sanaMkuu wangu Legacy ya Nyerere inaitaji uzi wake nakushauri fungua uzi tutakuja kuchangia kiduchu.
Sawa mkuuMkuu wangu Legacy ya Nyerere inaitaji uzi wake nakushauri fungua uzi tutakuja kuchangia kiduchu.
Kula like[emoji106] [emoji106] miaKipindi cha mzee ruksa vijana wakaanza kupanda ndege kwenda dubai kuchukua mzigo na kuleta mjini kufanya biashara.
Akina mama wakafurika Zanzibar kuchukua mali.
Mwaka 1994 Watanzania tukaangalia world cup kwenye TV zetu wenyewe!, acheni bhana Mzee Ruksa jembe