Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umemuonea Ritz. Hakuuliza yeyeKila shilingi ina upande wa pili, hayo mazuri nakuachia wewe Ritz.
Du ulikuwa unaenda ymca vp rungwe wakati wa disco toto dj jhone p pantalaki na cris fabi?Ni katika miaka kumi ya Mwinyi ndipo watu wakaanza kuvaa mitumba inayotazamika. Kabla ya hapo nadiriki kabisa kusema kwamba tulikuwa tunavaa marapurapu. Lakini katika miaka michache ya uongozi wa Mwinyi kinadada wakaanza kupendeza, mafuta ya nywele kwa ajili ya vichwa vya kinamama yakaanza kupatikana madukani.
Nakumbuka kabla Mwinyi hajaingia kwenye uongozi, mimi na watoto wenzangu tuliokuwa tunaenda disco toto pale YMCA tulikuwa tunapenda kusimama karibu na meza ya DJ marehemu Kalikali, lengo haswa lilikuwa ni kuzishangaa nywele zake, alikuwa ameweka madawa kichwani (kama Didier Drogba).
Sasa sisi kwa sababu hatukuwa tumezoa kuona nywele zimepakwa mafuta, tukawa tunacheza muziki karibu yake ili tutazame kichwa chake kwa karibu. Na jamaa alikuwa anawapata sana warembo kwa sababu ya nywele zake kuwa zimepakwa madawa.
Tulizoea enzi zile kutumia mafuta ya nazi vichwani, kunyolewa kwa viwembe chini ya miembe. Kwa kweli Mzee Mwinyi alileta rukhsa ya kufanya biashara, na watu wakaanza kupendeza. Saloon za kinamama zilianza miaka ya mzee Mwinyi. Mitumba ilishamiri enzi zile. Magari aina ya corolla yakawa mengi haswa yakimilikiwa na wahindi.
Mungu amempa umri mkubwa mzee Mwinyi naamini ni kwa sababu ya ubinadamu wake.
Ndugu yangu acha tu, enzi zile za rungwe oceanic, iliyokuwa mali ya Marehemu Mzee Mwakitange. Petty Ray Kasambula na volkswagen yake, nikiisikia tu usiku wa manane najua jamaa anatoka mbowe kupiga muziki. Alikuwepo Marehemu Choggy Sly, alikuwepo mtu anakwenda disco pale YMCA na mwamvuli mkononi akiigiza mbwembwe za wamarekani.Du ulikuwa unaenda ymca vp rungwe wakati wa disco toto dj jhone p pantalaki na cris fabi?
Hahahahahaha!! Mkuu umekumbusha mbali sana unakumbuka hii.Ni katika miaka kumi ya Mwinyi ndipo watu wakaanza kuvaa mitumba inayotazamika. Kabla ya hapo nadiriki kabisa kusema kwamba tulikuwa tunavaa marapurapu. Lakini katika miaka michache ya uongozi wa Mwinyi kinadada wakaanza kupendeza, mafuta ya nywele kwa ajili ya vichwa vya kinamama yakaanza kupatikana madukani.
Nakumbuka kabla Mwinyi hajaingia kwenye uongozi, mimi na watoto wenzangu tuliokuwa tunaenda disco toto pale YMCA tulikuwa tunapenda kusimama karibu na meza ya DJ marehemu Kalikali, lengo haswa lilikuwa ni kuzishangaa nywele zake, alikuwa ameweka madawa kichwani (kama Didier Drogba).
Sasa sisi kwa sababu hatukuwa tumezoa kuona nywele zimepakwa mafuta, tukawa tunacheza muziki karibu yake ili tutazame kichwa chake kwa karibu. Na jamaa alikuwa anawapata sana warembo kwa sababu ya nywele zake kuwa zimepakwa madawa.
Tulizoea enzi zile kutumia mafuta ya nazi vichwani, kunyolewa kwa viwembe chini ya miembe. Kwa kweli Mzee Mwinyi alileta rukhsa ya kufanya biashara, na watu wakaanza kupendeza. Saloon za kinamama zilianza miaka ya mzee Mwinyi. Mitumba ilishamiri enzi zile. Magari aina ya corolla yakawa mengi haswa yakimilikiwa na wahindi.
Mungu amempa umri mkubwa mzee Mwinyi naamini ni kwa sababu ya ubinadamu wake.
Mzee Mwinyi alikuwa akimsikiliza Nyerere wala habishani naye wala hagombani naye lakini inapokuja kwenye kufanya maamuzi anafanya maamuzi kwa jinsi yeye anavyoona inafaa!
Ritz, huwa nawatazama hawa watoto wa smart phones nawaona hawana ujanja wowote. Acha tu yaani, tunaongelea enzi hizo za watoto wa Oysterbay kufanya sherehe halafu sisi watoto wa upanga mashariki tunakwenda kwa miguu kwenye nyumba ya mtu fulani. Party ikimalizika kulikuwa hakuna mambo ya boda boda au bajaji, watu wakanyaga kwa miguu taratibu kutoka mitaa ya Obay, wanavuka salender Brigde wanakunja kushoto kuitafuta Aga Khan, wakivuka Gymkhana, yanakuwepo makundi mawili, mmoja linaelekea shaaban robert na jingine linakuwa ni la watoto wa mirambo na ohio kwenye maghorofa ya Railways.
Ma-DJ wakali kabisa wa enzi hizo walikua pamoja katika show Club Africana. DJ Meb, Neagre Jay, DJ Choggy Sly (RiP) , DJ John Peter Pantalakis, mratibu wao Nassoro Born City (RiP), DJ Kalikali (RiP) na DJ Eddy Sally (RiP) ... Masiku yamepita.Du ulikuwa unaenda ymca vp rungwe wakati wa disco toto dj jhone p pantalaki na cris fabi?
Rits umenikumbusha hao watu hasa marehem Nassor boncity na usimsahau seyduu.Ma-DJ wakali kabisa wa enzi hizo walikua pamoja katika show Club Africana. DJ Meb, Neagre Jay, DJ Choggy Sly (RiP) , DJ John Peter Pantalakis, mratibu wao Nassoro Born City (RiP), DJ Kalikali (RiP) na DJ Eddy Sally (RiP) ... Masiku yamepita.
Mimi ninayokumbuka wakati wa Mwinyi ni haya;
Mengine nawaachia...
- Rukhsa, nchi kugeuzwa kokoro
- Kaburi la Azimio la Arusha
- Kupotea kwa tausi viwanja vya Ikulu na Karimjee
- Kushuka kwa hadhi ya Ikulu
- First Lady kuitwa shemeji
- Kuzuka kwa mihadhara ya kidini
- Mgogoro wa Loliondo na Waarabu
- Mwanzo wa biashara ya Wanyama
- Ukwepaji wa kodi kushika kasi
- Mwanzo wa kuingia mikataba mibovu
- Kuzaliwa kwa IPTL, hadi leo inatutafuna.
- Kutothaminiwa kwa wasomi na wataalamu
- CCM kutekwa na wafanyabiashara na walanguzi.
- Kampuni za mfukoni na utapeli kushika kasi
- Nchi kuendeshwa kwa mtindo wa yupo yupo
Phillipo,Ritz, huwa nawatazama hawa watoto wa smart phones nawaona hawana ujanja wowote. Acha tu yaani, tunaongelea enzi hizo za watoto wa Oysterbay kufanya sherehe halafu sisi watoto wa upanga mashariki tunakwenda kwa miguu kwenye nyumba ya mtu fulani. Party ikimalizika kulikuwa hakuna mambo ya boda boda au bajaji, watu wakanyaga kwa miguu taratibu kutoka mitaa ya Obay, wanavuka salender Brigde wanakunja kushoto kuitafuta Aga Khan, wakivuka Gymkhana, yanakuwepo makundi mawili, mmoja linaelekea shaaban robert na jingine linakuwa ni la watoto wa mirambo na ohio kwenye maghorofa ya Railways.
Watu walikuwa wanazifuata party za usiku kwa miguu, lakini walikuwepo wezi wa magari ya baba, wanavizia wazee wamelala, wanaenda gereji wanalisukuma gari taratibu mpaka kwenye kona ya mtaa halafu ndio linawashwa. Mwenye gari mara nyingi hana hela ya mafuta, anafanya kuwaambia marafiki zake wachange ili waweze kwenda na kurudi nyumbani bila ya baba kushtukia mchezo asubuhi ya siku inayofuata.
Sahimtz,Rits umenikumbusha hao watu hasa marehem Nassor boncity na usimsahau seyduu.
Mwinyi aliiporomosha nchi yeye alikuwa yupo bize kusafir kwenda arabuni kuoa huku nchi ikididimia kiuchumi
Hovyooooooooo sana uyu mzee wa ruksa kama sio mkapa kufunga mkanda Leo hi tungekuwa Sawa na Zimbabwe
Mkapa alitengeneza uchumi baada ya kuharibiwa na Mwinyi baadae mkwere akaja na kuanza kutumbua mpaka Sasa nch imeoza
Unapo sema mzee mwinyi kaharibu nchi labda ungetupa takwimu za nchi alipo ikuta.Mwinyi aliiporomosha nchi yeye alikuwa yupo bize kusafir kwenda arabuni kuoa huku nchi ikididimia kiuchumi
Hovyooooooooo sana uyu mzee wa ruksa kama sio mkapa kufunga mkanda Leo hi tungekuwa Sawa na Zimbabwe
Mkapa alitengeneza uchumi baada ya kuharibiwa na Mwinyi baadae mkwere akaja na kuanza kutumbua mpaka Sasa nch imeoza
Duh hii rohombaya yako imezidi sasaMwinyi aliiporomosha nchi yeye alikuwa yupo bize kusafir kwenda arabuni kuoa huku nchi ikididimia kiuchumi
Hovyooooooooo sana uyu mzee wa ruksa kama sio mkapa kufunga mkanda Leo hi tungekuwa Sawa na Zimbabwe
Mkapa alitengeneza uchumi baada ya kuharibiwa na Mwinyi baadae mkwere akaja na kuanza kutumbua mpaka Sasa nch imeoza
Forodhani primary school. Enzi za kwenda kutazama basketball pale gymkhana ambapo sasa hivi pamejengwa hotel ya serena.Phillipo,
Utaniliza daah! Nakumbuka Kulikuwa na dala dala likiitwa Scaba Scuba la watoto wa mjini lilikuwa la mwisho kuondoka lakini la kwanza kufika mjini.
Toto disco Msasani na kukimbilia basi la mwisho pale kawe, Mbowe Club, YMCA, Chezimba, Mawingu club.
Mzee wapi hiyo Olimpio au Bunge hahahaha.